Unasema kwamba watu wanaomwamini Mungu wanapaswa kuikubali kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, na ni hapo tu ndipo wanapoweza kutakasiwa tabia yao potovu na wao wenyewe kuokolewa na Mungu. Lakini sisi, kwa mujibu wa mahitaji ya Bwana, hutenda unyenyekevu na uvumilivu, kuwapenda adui zetu, kuibeba misalaba yetu, kuviacha vitu vya dunia, na sisi hufanya kazi na kuhubiri kwa ajili ya Bwana na kadhalika. Hivyo si haya yote ni mabadiliko yetu? Daima tumetafuta kwa njia hii, kwa hiyo hatuwezi kupata utakaso, unyakuo na kuingia katika ufalme wa mbinguni?
Jibu:
Tunaweza kuwapenda adui zetu, kubeba msalaba, kushinda mwili wetu, na kueneza injili ya Bwana. Hizi ni tabia chanya zinazotokana na imani yetu kwa Bwana, na kuweza kutenda kwa njia hii kunaashiria kuwa imani yetu kwa Bwana ni ya kweli. Tabia hizi nzuri zinaweza kuonekana kuwa sahihi kwa wengine na kana kwamba ziko sambamba na neno la Mungu, lakini haimaanishi kwamba tunayaweka maneno ya Mungu katika vitendo na kufuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, wala haimaanishi kwamba tumeacha asili yetu ya dhambi na kutakaswa. Tunapokuwa tunaangalia tabia nzuri za wengine hatuwezi tu kuangalia kuonekana kwao kwa nje; lazima pia tuangalie nia zao na madhumuni ya hatimaye.