Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili ili kutumika kama sadaka ya dhambi kwa wanadamu, akiwaokoa kutoka kwa dhambi. Katika siku za mwisho Mungu amepata mwili tena ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa. Kwa nini Mungu anahitaji kuwa mwili mara mbili ili kufanya kazi ya kumwokoa wanadamu? Na kuna umuhimu gani wa Mungu kuwa mwili mara mbili?
Jibu:
Ni kwa nini lazima Mungu apate mwili mara mbili kufanya kazi ya kuwaokoa wanadamu? Tunapaswa kuelewa vizuri kwanza: Kuhusu wokovu wa wanadamu, kupata mwili kwa Mungu mara mbili kuna maana ya kina na kubwa. Kwa sababu kazi ya wokovu, haijalishi kama tunazungumza kuhusu ukombozi au hukumu na utakaso katika siku za mwisho, haiwezi kutekelezwa na mwanadamu. Inahitaji Mungu kupata mwili na kutekeleza kazi hiyo Mwenyewe. Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu, yaani, Roho wa Mungu alijivika mwili mtakatifu na usio na dhambi, na alipigiliwa misumari msalabani kutumika kama dhabihu ya dhambi, Akamkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi yake. Ndiyo. Sote tunalifahamu hili. Lakini kuhusu kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, kwa nini Anapata mwili kama Mwana wa Adamu kuonekana na kufanya kazi? Wengi wana wakati mgumu kulielewa hili.