XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
Matokeo ya mtu anayemwamini Mungu katika dini na ambaye hupitia mchafuko na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo ni yapi? Mtu anaweza kuokolewa na Mungu kama anamwamini Mungu kwa njia hii?
“Wao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwelekeza kipofu, wote wawili wataanguka ndani ya shimo” (Mathayo 15:14).
“Kwa kuwa viongozi wa watu hawa wanawafanya wapotoke; nao wanaoongozwa na hao watu wameangamizwa” (Isaya 9:16).
“Watu wangu wanateketezwa kwa ajili ya ukosefu wa maarifa…. Walivyokuwa wakizidishwa, ndivyo walivyokuwa wakitenda dhambi dhidi Yangu: kwa hiyo nitabadili utukufu wao uwe aibu. Wanakula dhambi ya watu Wangu, nao hupendezwa na udhalimu wao. Na itakuwa, jinsi watu walivyo, ndivyo jinsi kuhani alivyo: na mimi nitawaadhibu kwa sababu ya njia zao, na kuwalipiza kwa sababu ya vitendo vyao” (Hosea 4:6-9).