7.30.2019

Ni nini lengo na umuhimu wa Mungu kuwa mwili nchini China ili kufanya kazi katika siku za mwisho?

XIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Uhimu wa Mungu Kuwa Mwili Nchini China Katika Siku za Mwisho

Ni nini lengo na umuhimu wa Mungu kuwa mwili nchini China ili kufanya kazi katika siku za mwisho?


Maneno Husika ya Mungu:
Kila hatua ya kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu wote, na inawalenga wanadamu wote. Ingawa ni kazi Yake katika mwili, bado inaelekezwa kwa binadamu wote; Yeye ni Mungu wa binadamu wote, na ni Mungu wa viumbe vyote vilivyoumbwa na ambavyo havijaumbwa. Ingawa kazi Yake katika mwili ipo ndani ya mawanda finyu, na kusudi la kazi hii pia lina mipaka, kila wakati Anapokuwa mwili kufanya kazi Yake, Yeye huchagua chombo cha kazi Yake ambacho ni wakilishi na ambacho kina uwakilishi mkubwa; Hachagui kikundi cha watu wa kawaida na wasiosifika kwa ajili ya kuwafanyiza kazi, lakini badala yake huwachagua kama wawakilishi wa kazi Yake kundi la watu wenye uwezo kuwa wahusika wa kazi Yake katika mwili. Kundi hili la watu linachaguliwa kwa sababu ya mawanda ya kazi Yake katika mwili ni finyu, na wamejiandaa mahususi kwa ajili ya Kufanyika Kwake kuwa mwili, na limechaguliwa hasa kwa ajili ya kazi Yake katika mwili. Uchaguzi wa Mungu wa walengwa wa kazi Yake si usio na msingi, bali kulingana na kanuni: Mlengwa wa kazi anapaswa kuwa na manufaa katika kazi ya Mungu mwenye mwili, na anapaswa kuwa na uwezo wa kuwawakilisha wanadamu wote. Kwa mfano, Wayahudi waliweza kuwawakilisha binadamu wote katika kupokea wokovu binafsi wa Yesu, na Wachina wanaweza kuwawakilisha wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu mwenye mwili. Kuna msingi kwa Wayahudi kuwa wawakilishi wa binadamu wote, na kuna msingi kwa uwakilishi wa Wachina wa wanadamu wote katika kuukubali ushindi binafsi wa Mungu. Hakuna kinachofichua maana ya ukombozi kuliko kazi ya ukombozi iliyofanywa miongoni mwa Wayahudi, na hakuna kinachofichua uhakika na mafanikio ya kazi ya ushindi kuliko kazi ya ushindi iliyofanywa miongoni mwa Wachina.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama kazi ya awamu hii inahusu tu kufanya watu kuwa wakamilifu, basi inaweza kufanywa Uingereza, au Amerika, au Israeli; inaweza kufanywa kwa watu wa taifa lolote. Lakini kazi ya kushinda ni kuwa inachagua. Hatua ya kwanza ya kazi ya kushinda ni ya muda mfupi; aidha, itatumika kumdhalilisha Shetani na kuushinda ulimwengu mzima. Hii ndiyo kazi ya mwanzo ya kushinda. Mtu anaweza kusema kwamba kiumbe yeyote anayemwamini Mungu anaweza kufanywa kuwa kamili kwa sababu kukamilishwa ni kitu ambacho mtu anaweza kufikia tu baada ya mabadiliko ya muda mrefu. Lakini kushindwa ni tofauti. Kielelezo na mlengwa wa kushinda lazima awe yule anayebaki nyuma zaidi, akiishi kwenye giza totoro kabisa, na vilevile mwenye hadhi kidogo kabisa, na asiyekuwa radhi kumkubali Mungu zaidi, na asiyetii Mungu zaidi. Huyu ndiye aina ya mtu anayeweza kutoa ushuhuda wa kushindwa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kumshinda Shetani. Shabaha kuu ya kufanya watu kuwa wakamilifu, kwa upande mwingine, ni kuwapata watu wale. Ni kwa ajili ya kuwawezesha watu kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa ndio kazi ya kushinda imewekwa hapa, kwa watu kama ninyi. Lengo ni kuwafanya watu kutoa ushuhuda baada ya kushindwa. Watu hawa walioshindwa watatumika kufikia shabaha ya kumdhalilisha Shetani.
kutoka katika “Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikuwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. … Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili. Kwa kweli, mara baada ya kazi miongoni mwenu imekuwa ya mafanikio, hii itakuwa sawa na mafanikio katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa sababu Yangu kuwafanya mfano wa kuigwa na kielelezo.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wa Uchina hawajawahi kumwamini Mungu na hawajawahi kumhudumia Yehova, hawajawahi kumhudumia Yesu. Yote wanayofanya ni kusujudu, kufukiza uvumba, kuchoma sanamu ya Mungu ya karatasi, na kumwabudu Buddha. Wao wanaabudu sanamu tu—wote ni waasi mno, hivyo jinsi nafasi ya watu ilivyo ya chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kwamba kile Mungu hupata kutoka kwenu ni utukufu hata zaidi. … Kama uzao wa Yakobo ungezaliwa nchini China, katika kipande hiki cha ardhi, na wote walikuwa ninyi nyote, basi umuhimu wa kazi iliyofanyika kwenu ingekuwa nini? Shetani angesema nini? Shetani angesema: “Walikuwa wakikuogopa Wewe, Walikutii tangu mwanzo na hawana historia ya kukusaliti. Wao si wenye giza kabisa, wa hali ya chini kabisa, au walio nyuma zaidi kimaendeleo kati ya wanadamu.” Kati ya ulimwengu wote, watu wa Kichina ni watu walio nyuma zaidi kimaendeleo. Wamezaliwa na hali ya chini na uadilifu duni, ni wapumbavu na wenye ganzi, nao ni watovu wa adabu na waliofifia. Wameloweshwa na tabia za kishetani, wachafu na waasherati. Mnayo haya yote. Kwa mintarafu ya tabia hizi potovu, baada ya kazi hii kukamilika watu watazitupilia mbali na wataweza kutii kikamilifu na kufanywa kuwa kamili. Tunda tu kutoka kwa aina hii ya kazi ndilo huitwa ushuhuda kati ya viumbe!
kutoka katika “Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kufanya kazi sasa kwa uzao wa Moabu ni kuwaokoa wale ambao wameanguka katika giza zaidi. Ingawa walikuwa wamelaaniwa, Mungu yuko tayari kupata utukufu kutoka kwao. Hii ni kwa sababu hapo awali, wote walikuwa watu waliomkosa Mungu mioyoni mwao—kuwafanya tu kuwa wale wanaomtii na kumpenda Yeye ni ushindi wa kweli, na matunda hayo ya kazi ni ya thamani sana na yenye kuridhisha zaidi. Huku tu ni kupata utukufu—huu ndio utukufu ambao Mungu anataka kuupata katika siku za mwisho. Ingawa watu hawa ni wa nafasi ya chini, sasa wanaweza kupata wokovu mkubwa mno, ambao kwa kweli ni kupandishwa hadhi na Mungu. Kazi hii ni ya maana sana, na ni kwa njia ya hukumu ndipo Anawapata watu hawa. Yeye hawaadhibu kwa makusudi, lakini Amekuja kuwaokoa. Kama bado angekuwa Anafanya kazi ya kushinda katika Israeli wakati wa siku za mwisho ingekuwa ni bure; hata kama ingezaa matunda, haingekuwa na thamani yoyote au umuhimu wowote mkubwa, na Yeye hangeweza kupata utukufu wote. Anafanya kazi kwenu, yaani, wale ambao wameanguka katika maeneo yenye giza zaidi, wao walio nyuma zaidi kimaendeleo. Watu hawa hawakiri kuwa kuna Mungu na kamwe hawajapata kujua kwamba kuna Mungu. Viumbe hawa wamepotoshwa na Shetani hadi kiwango ambapo wamemsahau Mungu. Wamepofushwa na Shetani na hawajui kabisa kwamba kuna Mungu mbinguni. Katika mioyo yenu nyote mnaabudu sanamu, mnamwabudu Shetani—je, si ninyi ni watu wa hali ya chini zaidi, watu walio nyuma zaidi kimaendeleo? Ninyi ni wa hali ya chini kabisa ya mwili, mnakosa uhuru wowote wa kibinafsi, na mnapitia shida pia. Ninyi pia ni watu mlio katika ngazi ya chini kabisa katika jamii hii, bila hata uhuru wa imani. Huu ni umuhimu wa kufanya kazi kwenu.
kutoka katika “Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini kazi ya siku za mwisho inafanywa nchini China, mahali penye giza sana, iliyo nyuma zaidi kimaendeleo? Ni kufichua utakatifu na haki ya Mungu. Kwa ufupi, jinsi mahali palivyo penye giza zaidi ndipo panapoweza kutoa mwanga bora kwa utakatifu Wake. Ukweli ni kwamba kufanya yote haya ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Mnajua tu sasa kwamba Mungu aliye mbinguni ameshuka duniani na anasimama katikati yenu, na Amepewa umuhimu dhidi ya uchafu na uasi wenu, ili muanze kuwa na ufahamu wa Mungu—je, si hili linatia moyo pakubwa?
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utukufu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari.
kutoka katika “Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kufanya vile tu ndiko kunaweza kudhihirisha nguvu kuu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Mafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu. Kila mara Mungu Anapofanya kazi katika wakati fulani na kila mara anapofanya kazi Yake kwa kupitia mwili, huwa Anapokea utukufu na papo hapo huwapata Anaotaka kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu na hivi ndivyo anavyosimamia kazi Yake.
Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo anatukuzwa; nyingine ni kazi ya ushindi na ukamilifu katika nyakati za mwisho, ambayo kwayo pia Atapokea utukufu. Huu ni usimamizi wa Mungu. Hivyo basi, usichukulie kazi ya Mungu au agizo Lake kwako kuwa rahisi sana. Ninyi ndio warithi wa uzito wa milele wa utukufu wa Mungu, hili liliteuliwa na Mungu. Katika sehemu hizo mbili za utukufu wa Mungu, moja inafichuliwa ndani yako; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu Wake umepewa ili uwe urithi wako. Huku ndiko kutukuzwa kutoka kwa Mungu na mpango wake uliopangwa kitambo. Kutokana na ukuu wa kazi aliyoifanya Mungu katika nchi ambako joka kuu jekundu linaishi, kazi kama hii, ikipelekwa katika sehemu nyingine, ingezaa tunda zuri kitambo na ingekubaliwa na mwanadamu kwa urahisi. Na kazi kama hii ingekuwa rahisi sana kukubaliwa na viongozi wa dini wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwani kazi ya Yesu ni kama kielelezo. Ndio maana Hawezi kutekeleza hatua hii ya kazi ya utukufu mahali pengine; yaani, kwa kuwa kuna uungaji mkono kwa watu wote na utambulisho wa mataifa yote, hamna mahali ambapo utukufu wa Mungu unaweza “kupumzikia.” Na huu ndio umuhimu wa kipekee wa hatua hii ya kazi katika nchi hii.
kutoka katika “Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama anaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni wa ukoo wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya viumbe wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe wa Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Waisraeli ambao ni viumbe wa Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Waisraeli; Mungu awali alikuwa akifanya kazi nao kwa sababu walikuwa watu wapotovu kwa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni dhaifu wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Yudea. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Waisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kufanya kazi miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa hasa inaenda kinyume na dhana za binadamu; hawa watu ni wa chini zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mwanzoni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini zaidi. Kama sehemu ya viumbe, kumilikiwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Bwana wa viumbe, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.
… Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe wote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Waisraeli, kuwa Waisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Waisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. … Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.
kutoka katika “Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote” katika Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni