XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
Kwa nini kila hatua mpya ya kazi ya Mungu hukabiliwa na uasi mkali na lawama ya ulimwengu wa kidini? Chanzo cha msingi ni nini?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Naye akaanza kuzungumza nao kwa kutumia mifano. Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu, naye akalizingira kwa ugo, naye akachimba mahala pa shinikizo ya zabibu, naye akaunda mnara, naye akalipanga kwa wakulima, na kuenda katika nchi ya mbali. Na kwa majira yake akamtuma mtumishi kwa wakulima wale, ili aweze kupata matunda ya shamba hilo la mizabibu kutoka kwa wakulima. Nao wakamkamata, na kumpiga, na kumtoa humo bila chochote. Na tena akamtuma mtumishi mwingine; nao wakamtupia mawe, na kumjeruhi kichwani, na kumwondoa humo kwa aibu.
Na tena akamtuma mwingine; nao wakamwua, na wengine wengi; wakiwapiga wengine, na kuwaua wengine. Kwa sababu alikuwa na mwana mmoja, aliyempenda sana, alimtuma pia kwao mwisho, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wakulima hao waliambiana, Huyu ndiye mrithi; njooni, acha tumwue, na urithi wake utakuwa wetu. Nao wakamchukua, na kumwua, na kumtupa nje ya shamba la mizabibu. Bwana wa shamba hilo la mizabibu atafanyaje basi? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, naye atawapa wengine lile shamba la mizabibu” (Marka 12:1-9).
“Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, na wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu. … Hivyo kuanzia siku hiyo walishauriana pamoja ili wamuue” (Yohana 11:47-48, 53).
Maneno Husika ya Mungu:
Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu.
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Kwa imani yao, yote yanayohitajika kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kuhifadhi sheria, na iwapo watatubu na kukiri dhambi zao, dhamira ya Mungu milele itaridhika. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu.
kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na masuala mapya, hivyo pana kazi mpya, na hivyo basi kuwepo na kazi iliyopitwa na wakati. Hapana ukinzani kati ya kazi mpya na ya zamani, ila zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi. Ni haki kusema kuwa katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa dhana mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu kwa mwanadamu ambapo mwanadamu ana kila aina ya dhana kumhusu Mungu—na matokeo yake ni kuwa wengi wa watu wa kidini wanaomhudumia Mungu wamegeuka kuwa adui Zake. Kwa hivyo, kadiri dhana za watu ya kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda Mungu wa zamani ambaye Amejaa mvi na Asiyepiga hatua. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6,000. Hawawezi kusaidika.
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee kudhibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi” wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru—je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki?
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita. Kila hatua inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua ya mwisho ambayo haiondolewi. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima huwa mpya na kamwe si kuukuu, Mungu mara kwa mara anaonyesha kipengele cha tabia Yake ambayo haijawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ikiwa wazoefu wakongwe wa kidini hufanya juu chini kukinzana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hii, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Na hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa tena, hata kufanya kazi ambayo huonekana kwa mwanadamu kuhitilafiana na kazi iliyofanywa awali, kuwa kinyume nayo. Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko—lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Leo, je, nyote hamjafuata katika kanuni hizi? … Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanadamu wajinga na wapumbavu mara nyingi huchukua ubinadamu wa kawaida wa Kristo kama dosari. Haijalishi jinsi Anavyofichua na kuonyesha nafsi ya uungu Wake, mwanadamu bado hawezi kukiri kwamba Yeye ni Kristo. Na zaidi kwamba Kristo Anaonyesha utii Wake na unyenyekevu, ndivyo wanadamu wengi wajinga humchukua Kristo kwa mzaha. Kuna hata wale ambao huelekeza Kwake mtizamo wa kutengwa na dharau, ilhali kuweka wale “wanadamu wakubwa” wa picha ya kujidai juu ya meza na kuwaabudu. Upinzani wa binadamu dhidi ya, na uasi wa Mungu huja kutokana na ukweli kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hutii mapenzi ya Mungu, vile vile kutokana ubinadamu wa kawaida wa Kristo; hapa ndipo kuna chanzo cha upinzani wa binadamu na uasi wake kwa Mungu. Kama Kristo hangekuwa mwenye umbo la ubinadamu wala nia ya kutafuta mapenzi ya Mungu Baba kutoka katika mtazamo wa kiumbe aliyeumbwa, lakini badala yake kumiliki ubinadamu mkuu, basi kuna uwezekano hakungekuwa na uasi katika mwanadamu yeyote. Sababu ya binadamu kuwa tayari kuamini katika Mungu Asiyeonekana mbinguni ni kwa sababu Mungu mbinguni hana ubinadamu na Yeye hana sifa ya kiumbe hata moja. Hivyo binadamu siku zote humchukua Yeye kwa heshima kubwa, lakini anayo tabia ya dharau kwa Kristo.
kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu asiyeonekana na kushikika anapendwa na kukaribishwa na wote. Kama Mungu ni Roho tu ambayo haionekani kwa mwanadamu, ni rahisi sana kwa mwanadamu kumwamini Mungu. Mwanadamu anaweza kuzipa uhuru fikra zake mwenyewe, anaweza kuchagua taswira yoyote anayotaka kama taswira ya Mungu ili kujifurahisha mwenyewe na kujifanya mwenyewe awe na furaha. Kwa njia hii, mwanadamu anaweza kufanya chochote kile kinachompendeza zaidi Mungu wake mwenyewe, na kile ambacho Mungu huyu angempenda akifanye, bila aibu yoyote. Aidha, mwanadamu huyu anaamini kwamba hakuna ambaye ni mwaminifu zaidi anayejitolea kwa Mungu kuliko yeye, na kwamba wengine wote ni mbwa wa Mataifa, na wasiokuwa waaminifu kwa Mungu. Inaweza kusemekana kwamba hiki ndicho kinachotafutwa na wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya kidhahania na ambayo imejikita katika mafundisho; wanavyovitafuta vinafanana, tofauti ikiwa ndogo tu. Ni kwamba tu taswira za Mungu katika fikra zao ni tofauti, lakini viini vyao kimsingi vinafanana.
Mwanadamu hasumbuliwi na imani yake ya kutojali katika Mungu, na anamwamini Mungu kwa namna anavyotaka. Hii ni moja ya “haki na uhuru wa mwanadamu,” ambao hakuna mtu anayeweza kuuingilia kwa sababu mwanadamu anamwamini Mungu wake mwenyewe na wala si Mungu wa mtu yeyote yule; ni mali yake binafsi, na takribani kila mtu anamiliki aina hii ya mali binafsi. Mwanadamu anaichukulia mali hii kama hazina ya thamani, lakini kwa Mungu hakuna kitu ambacho ni duni au hakina thamani zaidi ya hiki, maana hakuna kiashiria cha wazi cha upinzani kwa Mungu kuliko mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu mwenye mwili ndiyo Mungu amefanyika mwili ambaye ana umbo la kugusika, na ambaye anaweza kuonekana na kuguswa na mwanadamu. Yeye si Roho asiyekuwa na umbo, bali mwili ambao unaweza kuhusiana na kuonekana kwa mwanadamu. Hata hivyo, Miungu mingi ambayo watu wanaamini kwayo ni miungu isiyo na mwili na umbo maalumu, na ambayo haifungwi na umbo maalumu. Kwa njia hii, Mungu mwenye mwili amekuwa adui wa wengi wanaomwamini Mungu, na wale ambao hawawezi kuukubali ukweli wa Mungu mwenye mwili, vilevile, wamekuwa maadui wa Mungu. Mwanadamu amejawa na dhana si kwa sababu ya namna anavyofikiri, au kwa sababu ya uasi wake, bali ni kwa sababu ya mali hii binafsi ya mwanadamu. Ni kwa sababu ya mali hii watu wengi hufa, na ni Mungu huyu asiye dhahiri, ambaye hawezi kuguswa, hawezi kuonwa, na ambaye hayupo hakika ambaye huangamiza maisha ya mwanadamu. Maisha ya mwanadamu yanapotea si kwa sababu ya Mungu mwenye mwili, sembuse na Mungu wa mbinguni, bali ni Mungu wa fikra za mwanadamu mwenyewe.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa “Kristo wa kweli.” Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.
kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati wowote ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale wasio na kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu.
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. …
Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele ya Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akampiga Yesu misumari juu ya msalaba na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa ya kuchukiza na wa hali ya chini. Kama mwanadamu angekuwa na ubinadamu kidogo, hangekuwa mkatili kiasi hicho katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa hivyo katika utendeaji wake wa mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo, hangekuwa mwenye “shukrani” kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa katika mwili, lakini yeye hawezi kumshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi nzuri kiasi hicho, na badala yake analaani kuja kwa Mungu, au kupuuza kabisa ukweli wa Mungu aliyepata mwili, na inaonekana anapinga hali hii na anachoshwa nayo. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukua kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake bila kujali—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu.
kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni