Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Pili
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
Kwa roho yoyote, kupata kwake mwili mpya na nafasi anayochukua—nafasi yake ni ipi katika haya maisha—atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni.