4.18.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?


Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.   Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii kwa moyo wake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi inayofanywa na Mungu daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya vitendo kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. … Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Kwa kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kusalimisha na kuweka kando dhana zenu. Kila hatua inapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu. Kama nyinyi ni wazembe, hakika mtakuwa wamoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayevuruga kazi ya Mungu. … Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa kwa awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wanatii Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima kwa utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haijakubaliwa na Mungu.

kutoka katika "Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Kufuata njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu ni kuingia katika njia sahihi ya kazi halisi ya Roho Mtakatifu; pia ni kufuata njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea. Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya maneno, na kila kitu kinanenwa kutoka kwa maneno Yake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya maneno Yake, maneno Yake halisi. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu.

kutoka katika "Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili

Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake.

kutoka katika "Kuhusu Desturi ya Sala" katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kuupata uridhisho wa Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanaongozwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. … Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi, sifa za kuhitimu, ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia mapungufu yako. Unapoutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kuingia kwa undani zaidi kwenye upande mzuri, na kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa yako mwenyewe na mapungufu, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na katika hali isiyo ya kukaa tu, utaingia kikamilifu, na hii itamaananisha kuwa wewe ni mtu sahihi.

kutoka katika "Ni muhimu sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.

kutoka katika "Jinsi ya Kuujua Uhalisi" katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. … Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza.

kutoka katika "Ni muhimu sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Wewe ni usiye na hila na uko wazi, radhi kujijua, na radhi kuweka ukweli katika vitendo. Mungu anaona kuwa uko radhi kujijua na uko radhi kuweka ukweli katika vitendo, kwa hivyo unapokuwa mnyonge na hasi, Anakupa nuru mara mbili, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa radhi zaidi kujitubia mwenyewe, na kuwa na uwezo zaidi wa kutenda mambo ambayo unapaswa kutenda. Ni kwa njia hii tu ndipo moyo wako unakuwa na amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida anatilia maanani kumjua Mungu, ambaye anatilia maanani kujijua yeye mwenyewe, ambaye anayatilia maanani matendo yake atakuwa na uwezo wa kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, kupokea mara kwa mara ushauri na nuru kutoka kwa Mungu.

kutoka katika "Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili ya mwanadamu, na kujielewa mwenyewe; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata utiifu wa makusudi. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. …

… Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Kitawaathiri vipi ndugu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu. Kwa njia hii mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri.

kutoka katika "Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje" katika Neno Laonekana katika Mwili

Ushirika wa Mtu:

Roho Mtakatifu hufanya kazi kulingana na maneno ya Kristo, na hufanya kazi pia kulingana na watu kukubali na kumtii Kristo. Ni ikiwa tu watu watamkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo wanaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa watu humpinga Kristo au kuasi dhidi ya Kristo, basi hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama imani ya mtu kwa Mungu inaweza kuwaletea wokovu inaamuliwa na kama anaweza kweli kumkubali na kumtii Kristo au la. Kazi ya Roho Mtakatifu imejitegemeza kikamilifu kwa mtu kukubali na kumtii Kristo. Katika Enzi ya Neema, kazi ya Roho Mtakatifu ilifanywa kulingana na watu kukubali Bwana Yesu, kumtii Yeye, na kumwabudu Yeye. Katika Enzi ya Ufalme, kazi ya Roho Mtakatifu inafanywa kulingana na watu kukubali Mwenyezi Mungu, kumtii Mwenyezi Mungu, na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Roho Mtakatifu hufanya kazi pia kulingana na maneno ya Mwenyezi Mungu, ili kuwaleta waumini katika maneno ya Mungu na kuwafanya wafikie wokovu na ukamilifu. Huu ni msingi na kanuni ya kazi ya Roho Mtakatifu. Viongozi wengi wa dini wamekufa kama adhabu ya kumpinga au kumlaumu Kristo. Watu wengi wa kidini wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, wakianguka katika giza kupitia kukataa kwao kumkubali Kristo wa siku za mwisho. Katika nyumba ya Mungu, watu wengi wamechakaa katika maisha na kukata tamaa kwa sababu ya fikra zao za kudumu juu ya Kristo, na bado wengi wengine wameondolewa kwenye kazi ya Roho Mtakatifu kwa kumwamini tu Roho wa Mungu na si Kristo. Mambo haya yote yamesababishwa na watu kutomkubali au kumtii Kristo. Iwapo muumini ana kazi ya Roho Mtakatifu au la huamuliwa kikamilifu na mtazamo wake kwa Kristo. Ikiwa mtu anamwamini tu Mungu wa mbinguni, na hamtii Kristo, hatapokea kazi ya Roho Mtakatifu kamwe. Kwa sasa bado kuna watu wengi katika makanisa mbalimbali ambao humwamini tu Roho Mtakatifu lakini hawamwamini Kristo, na hivyo hupoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna wengi ambao huamini tu maneno ya Kristo, lakini hawamtii Kristo, na kwa hivyo wanachukiwa na Mungu. Kwa hivyo, kumkubali Kristo na kumtii Kristo ni ufunguo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ni iwapo tu mtu humkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo atafikia wokovu na kukamilishwa. Kwa uwazi, kazi za Roho Mtakatifu katika kila enzi zina misingi na kanuni zake. Nani ajuaye kuna watu wangapi bado hawaoni umuhimu wa kumtii Kristo. Roho Mtakatifu hufanya kazi kikamilifu kulingana na maneno ya Kristo. Ikiwa watu hawawezi kuyakubali maneno ya Kristo, na wanaendelea kushikilia fikra kuyahusu na wakayapinga, basi hawawezi kabisa kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengi huomba tu katika jina la Mwenyezi Mungu, lakini hawatii kazi ya Kristo, na hawakubali kabisa maneno ya Kristo. Watu kama hawa ni wapinga Kristo, na hawawezi kabisa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu.

kutoka katika "Matokeo Ambayo Yanaweza Kufanikishwa na Ufahamu Halisi wa Ukweli" katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha

Jinsi watu wanavyoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu pia ni suala muhimu. Hupaswi kufikiri kuwa utapata kazi ya Roho Mtakatifu kwa kusoma neno la mungu bila kujali. Mtu anapaswa kuwa na moyo unaotafuta ukweli. Moyo wa mtu unapaswa kuwa sahihi, anapaswa kutafuta ukweli, kusoma neno la Mungu, kuomba Mungu kwa uaminifu na hamu. Ni wakati huo tu ambapo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Mtu hawezi kuwa na msisimuko wa mara moja au kuwa na hamu, au shauku ya muda mfupi ya kusoma neno la Mungu na aweze kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Ni lazima awe mtu anayefaa, mtu anayetafuta ukweli, na makusudi yao yanapaswa kuwa sahihi. Kulingana na maneno ya Mungu, mtu wa aina hii huwa na njaa na kiu ya haki, na mtu tu wa aina hii anaweza kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Watu ambao hutenda maovu hawawezi kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Watu ambao huishi na mawazo kuhusu Mungu, ambao huishi na tabia ya kuasi, ambao huishi kwa njia mbaya, hawatapokea kwa njia rahisi kazi ya Roho Mtakatifu iwapo hawatafuta ukweli. Kuishi na tabia ya uasi kwa Mungu kunamaanisha nini? Inamaanisha kuwa kilindini cha moyo wao wako katika hali ya kumpinga Mungu. Moyo wao hauko sahihi, unampinga Mungu, una mgogoro na Mungu, unalalamika kuhusu Mungu, au haupendi ukweli. Katika hali hizi chache zisizo za kawaida, mtu hawezi kupokea kazi ya Roho mtakatifu kwa urahisi, na hiki ni kipengele muhimu. Yaani, iwapo kila wakati unaishi maisha yako katika hali ya kumuasi Mungu au kuishi katika hali ya kumpinga Mungu, hutapokea kazi ya Roho Mtakatifu kwa urahisi. Roho Mtakatifu huchunguza sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mtu. Tulikuwa tukisema, "Mungu huchunguza kilindini mwa moyo wa mtu," hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa Roho huchunguza kilindini mwa moyo wa mtu, si hiyo ni kweli? Hivyo Roho Mtakatifu huchunguza ndani ya moyo wa mtu yeyote katika hali zote, akitafuta kujua mtazamo wake ni wa aina gani na kuona iwapo anautafuta ukweli. Mungu anaweza kuona hili kwa wazi zaidi. Hivyo, ni lazima mtazamo wako uwe sahihi ili kutafuta ukweli. Akili yako inatafuta ukweli, inatamani ukweli na inatamani kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Iko tayari kutenda ukweli na ina hamu ya ukweli ili kusuluhisha matatizo. Wakati huu, Roho Mtakatifu atakupa nuru.

kutoka katika "Jinsi Mtu Anapaswa Kutafuta Ukweli" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (I)

Sasa, tunaweza kuona kwamba Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake hasa kuwaongoza watu kuingia katika neno la Mungu na kuuelewa ukweli. Ni vipengele vipi kuingia katika neno la Mungu kunavihusisha? Kuingia katika neno la Mungu hakumaanishi kwamba mtu anasoma sentensi moja mahsusi, anaizingatia kidogo na kisha ana uelewa kidogo. Hii si sawa na kuingia katika neno la Mungu. Ni jambo tofauti kabisa. Jambo muhimu zaidi ni kuingia katika neno la Mungu kupitia uzoefu. "Uzoefu" huu unahusisha tajriba anuwai. Sio kipengele kimoja tu cha uzoefu. Kuna vipengele vingi kwa uzoefu huu. Kutimiza wajibu wa mtu pia ni kupitia neno la Mungu. Kuweka ukweli katika matendo ni kupitia neno la Mungu. Hasa kupitia aina mbalimbali za majaribu na usafishwaji hata zaidi ni kupitia neno la Mungu. Bila kujali ni chini ya mazingira gani au hali, almradi unapitia neno la Mungu, utaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa mfano, tunapokabiliwa na majaribu, sisi humwomba Mungu ili kutafuta nia za Mungu. Matokeo yake, Roho Mtakatifu hutupa nuru ili tuweze kuyaelewa makusudi ya Mungu. Hivi ndivyo kwa sababu inahusiana na kuingia katika neno la Mungu. … Aidha, katika mfanyiko tendani wa kutimiza wajibu wetu, na katika uzoefu wa maisha yetu ya kila siku, bila kujali ni hali gani, almradi tutafute ukweli, tutafute nia za Mungu na kumwomba Mungu, tutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu yuko hapo kutuongoza kuingia katika neno la Mungu na ukweli. Kuna baadhi ya watu ambao wana uzoefu mkubwa kuhusiana na kipengele hiki. Bila kujali ni hali gani inayowakumba, wao humwomba Mungu. Bila kujali ni watu wa aina gani wanaokutana nao, wao humwomba Mungu na kumuuliza Mungu awape nuru na kuwapa hekima na akili. Wao humwomba Mungu kuwaongoza. Almradi watu hupitia kazi ya Mungu kwa njia hii, wataelewa mambo mengi ya neno la Mungu. Watajua jinsi wanavyopaswa kutenda katika hali thabiti, dhahiri. Watajua jinsi ya kuliweka katika matumizi mazuri. Hii ndiyo njia ya kuingia katika neno la Mungu.

kutoka katika "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni