Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo jina-la-Mungu. Onyesha machapisho yote

4.16.2019

Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?


Maneno Husika ya Mungu:

      Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu angeshikilia ukweli kwamba "Yehova ni Mungu" na "Yesu ni Kristo," ukweli ambao unazingatiwa kwa kipindi kimoja, basi mwanadamu hataweza kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. 

4.14.2019

Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe


Maneno Husika ya Mungu:

Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. 

4.12.2019

Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:

       Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye anakuhitaji wewe, kiumbe, kuamua jina lake? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu.