8.16.2018

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili.

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili.

Maneno Husika ya Mungu:
Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake.

Sura ya 9


       Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. 

8.15.2018

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:


Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili.

Hebu Tuone ni Nani Anayemshuhudia Mungu Vema Zaidi

Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo

Hebu Tuone ni Nani Anayemshuhudia Mungu Vema Zaidi

Mwenyezi Mungu wa kweli, nakupenda. Naimba wimbo wa sifa,
nikicheza ngoma ya furaha na changamfu, kwa ajili Yako tu, Mwenyezi Mungu.
Tunaweza kukusifu Wewe kama leo—haya Mungu ameamua kabla.
Mungu wa kweli Ametushinda; sote tunakuja kumsifu Yeye.
Kila mtu njoo na mcheze, njoo muimbe wimbo wa furaha wa kusifu.
Ukiniuliza mimi mbona nacheza hivyo, moyo wangu unapenda, unampenda Mungu!

8.14.2018

Wimbo wa Kifuasi cha Dhati


Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki) from Kanisa la Mwenyezi Mungu on Vimeo.
Wimbo wa Kifuasi cha Dhati
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.
Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.
Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote.
Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

8.13.2018

Tamko la Arubaini na Sita

Tamko la Arubaini na Sita

Sijui jinsi watu wanavyoendelea katika kuyafanya maneno Yangu kuwa msingi wa kuweko kwao. Nimehisi wasiwasi kila mara kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu, lakini watu hawaonekani kuwa na fahamu yoyote kuhusu hili—na kutokana na hilo, hawajawahi kuyatilia maanani mambo Yangu, na hawajawahi kukuza kuabudu kokote kwa ajili ya mtazamo Wangu kuhusiana na mwanadamu.

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, sasa kwa sababu tuko na Wewe, masumbuko yanabadilika kuwa furaha.
Kula, kunywa, kufurahia maneno Yako, tuko na Wewe kila siku.
Maji Yako ya uzima yanatustawisha, tuna ukarimu kwa vyote.
Jua ukweli, ingia katika ukweli, yote yanakutegemea Wewe.
Ndugu, acha tule, tunywe maneno ya Mungu.

8.12.2018

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"


Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China" 



Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. ...
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara.

8.11.2018

Kiini na Tabia ya Mungu Daima Vimekuwa Wazi kwa Binadamu

Kiini na Tabia ya Mungu Daima Vimekuwa Wazi kwa Binadamu

Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu, Amekuwa akifichua kwao
Kiini Chake na kile Alicho na Alicho nacho, bila kukoma, kila wakati.
Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,
Mungu huzungumza na kufanya kazi ili kuonyesha tabia Yake na kiini.
Havijawahi kufunikwa kamwe, havijawahi kufichika kamwe, vimeachiliwa bila kusita,
Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,
vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

8.10.2018

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Inaonekana kwamba katika mawazo ya watu, Mungu ni wa fahari sana naye Haeleweki. Ni kana kwamba Mungu haishi miongoni mwa wanadamu, kana kwamba anawadharau watu kwa sababu Yeye ni wa fahari sana. Mungu, hata hivyo, Huziseta fikira za wanadamu na kuzifuta zote, Akizika fikira zao zote ndani ya "makaburi" ambamo zinageuka kuwa majivu. Mtazamo wa Mungu kwa fikira za wanadamu ni sawa na mtazamo Wake kwa wafu, Akiwafafanua apendavyo.

8.09.2018

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?


Utambulisho

      Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6). "Tazama, nasimama mlangoni, na kubisha: mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja na yeye, na yeye pamoja na mimi" (Ufunuo 3:20).