Kotekote katika enzi, kazi yote Niliyoifanya—kila hatua ya kazi hiyo—imekuwa na mbinu Zangu zinazofaa za kazi. Ni kwa sababu ya hili ndio watu Wangu wapendwa wamekuwa watakatifu zaidi na zaidi, na wa kufaa zaidi na zaidi kwa matumizi Yangu. Kwa sababu hiyo hiyo, hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba kadri mbinu Zangu za kazi zinavyoongezeka, idadi ya watu inapungua, ambalo husababisha watu kuzama katika kutafakari. Bila shaka, Kazi Yangu leo sio tofauti na watu wengi wamejikuta tena katika kutafakari, kwa hiyo kwa sababu ya mabadiliko ya mbinu Zangu, kuna sehemu ya watu ambao watajiondoa.
31. Mimi Sistahili Kumwona Kristo
Huanbao Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning
Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo,