Kotekote katika enzi, kazi yote Niliyoifanya—kila hatua ya kazi hiyo—imekuwa na mbinu Zangu zinazofaa za kazi. Ni kwa sababu ya hili ndio watu Wangu wapendwa wamekuwa watakatifu zaidi na zaidi, na wa kufaa zaidi na zaidi kwa matumizi Yangu. Kwa sababu hiyo hiyo, hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kwamba kadri mbinu Zangu za kazi zinavyoongezeka, idadi ya watu inapungua, ambalo husababisha watu kuzama katika kutafakari. Bila shaka, Kazi Yangu leo sio tofauti na watu wengi wamejikuta tena katika kutafakari, kwa hiyo kwa sababu ya mabadiliko ya mbinu Zangu, kuna sehemu ya watu ambao watajiondoa.
Inaweza kuelezwa kwa njia hii: Hili lilikuwa limeamuliwa na Mimi kabla, lakini halikufanywa na Mimi. Kutoka wakati wa uumbaji hadi sasa, watu wengi sana wameanguka na wengi sana wamepoteza njia yao kwa sababu ya mbinu za kazi Yangu, lakini Sijali kuhusu vile watu walivyo, kama wanahisi Sina moyo wa kupenda au kama wanahisi Mimi ni mkatili mno, na haijalishi kama ufahamu wa watu ni sahihi au la, Naepuka kutoa maelezo. Hebu kwanza tuwe na ushirika juu ya suala kuu la mjadala huu ili kila mtu awe na ufahamu kamili, na ili aweze kuepuka mateso yoyote yasiyoelezeka. Sitawalazimisha watu kuteseka kimya kama bubu. Badala yake, Nitaelezea kila kitu wazi ili watu wasilalamike Kwangu, na siku moja watu wote watatamka sifa ya kweli katikati ya kuadibu. Je, Hilo litafaulu? Je, Hilo linakidhi mahitaji ya watu?
Katika utangulizi wa enzi ya kuadibu, Nitawaambia watu maana ya jumla ya "enzi” hiyo kwanza ili wasinikosee. Yaani, Nitafanya utaratibu wa kazi Yangu, ambao hautabadilishwa na yeyote, na Sitamsamehe kabisa mtu yeyote anayeubadilisha bali Nitamshutumu. Je, mtakumbuka hilo? Hilo lote ni onyo la kutangulia. Katika mbinu mpya watu wote lazima kwanza waelewe kwamba jambo la kwanza na la awali kutimiza ni kuwa na ufahamu wa hali zao wenyewe. Kabla ya kupata ufahamu fulani wa mtu mwenyewe, hakuna mtu atakayeruhusiwa kuzungumza ovyo ovyo kanisani, na hakika Nitawaadibu wale wanaokiuka hili. Kuanzia siku hii kwenda mbele, mitume wote wataorodheshwa katika makanisa na kuzuiwa kwenda huku na kule; hilo lilileta matokeo kidogo. Wote walionekana kutimiza wajibu wao lakini walikuwa kweli wakinidanganya. Bila kujali vile wakati uliopita ulikuwa, leo yote yanapita na hayapaswi kutajwa tena. Tangu sasa na kuendelea, neno "mtume" litafutwa na kamwe halitatumiwa tena, kwa hiyo watu wote waweze kushuka kutoka kwa nafasi zao na wajijue. Hili bila shaka ni kwa ajili ya wokovu wao. "Cheo" si taji, ni neno la kutaja mtu tu. Je, mnaelewa maana Yangu? Wale ambao wanaongoza makanisa bado wataishi maisha ya kanisa ndani ya makanisa yao wenyewe, na bila shaka, hii si kanuni ngumu. Ikilazimu wanaweza kutembelea makanisa kwa uratibu wa mitume wengine wa zamani. Jambo muhimu zaidi ni kwamba ushirika wa makanisa lazima uongezwe ila kama hakuna washirika wa makanisa wanaoishi kweli maisha ya kanisa. Hata hivyo, lazima Nisisitize kwamba lazima nyote muungane ili mjijue na kuasi lile joka kubwa jekundu. Hii ni nia Yangu. Kiasi ambacho watu wanazungumza si muhimu, badala yake ni muhimu sana kwamba watu Wangu wote waweze kuja pamoja kama kitu kimoja, ambayo ni njia pekee ya kushuhudia kweli. Zamani, kila mtu alisema alijielewa, lakini Nimetamka maneno yasiyohesabika, na ni kiasi gani ambacho mmejielewa? Kadri cheo cha mtu kilivyo juu zaidi, ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi yeye kujiweka kando. Zaidi ya hayo, kadri matumaini ya mtu yalivyo makuu, ndivyo atakavyoteseka wakati wa kuadibu. Huu ni wokovu Wangu wa wanadamu—je, mnaelewa? Msichukulie hili juujuu tu. Kufanya hivyo ni duni sana na hakuna thamani; Je, mnaelewa maana ya msingi? Kama watu katika kanisa wanaweza kweli kujifahamu, hili linadhihirisha kwamba mtu wa aina hii ananipenda Mimi kweli. Ni kama msemo, "Msipomega mkate na watu huwezi kuelewa shida zao." Mnayaelewaje maneno haya? Mwishowe, Nitawafanya watu wote wapate kujifahamu wakati wa kuadibu, na kufanya waimbe na kucheka wakati wa kuadibu. Je, kweli utakuwa na imani ya kuniridhisha? Kwa hiyo unapaswa kufanya nini katika utendaji wako? Kuanzia sasa kuendelea, shughuli za kila kanisa zitashughulikiwa na watu wanaofaa katika kanisa hilo, na mitume wataishi tu maisha ya kanisa. Hiyo inaitwa "kuyapitia maisha." Je, mnaelewa?
Kabla ya kuadibu kuwajia wanadamu rasmi, Nitafanya kwanza "kazi ya salamu" kwa watu ili mwisho wao wote waniridhishe. Hata kwa wale ambao wataondoka, lazima wateseke na kumaliza ushuhuda wao kabla ya kuondoka, la sivyo Sitawasamehe. Hii inaonyesha hali Yangu ya kutovumilia makosa ya watu, na hali Yangu ya kufanikisha kile Ninachosema. Kwa hiyo, inatimiza maneno kutoka kinywa Changu "Namaanisha kile Ninachosema, na kile Ninachomaanisha kitafanikishwa, na kile Ninachofanikisha kitadumu milele." Maneno yanapotoka kinywani Mwangu, ndivyo Roho Wangu pia anaanza kazi Yake. Ni nani angethubutu kwa hiari kucheza na "mwanaserere" ulio mikononi mwake? Watu lazima wakubali kuadibu Kwangu kwa staha na kwa utiifu, na ni nani anayeweza kukuepuka? Je, Kunaweza kuwa na njia nyingine ila Mimi? Leo Nimekuruhusu uwe juu ya dunia, na ufurahi. Kesho Nitakuruhusu kwenda mbinguni na utasifu. Siku baada ya hiyo, Nitakuweka chini ya ardhi ambapo utaadibiwa. Je, hayo yote siyo matakwa ya kazi Yangu? Ni nani asiyepatwa na taabu, na ni nani asiyepokea baraka kwa ajili ya matakwa Yangu? Je, mnaweza kuwa tofauti? Kama watu Wangu duniani, mnapaswa kufanya nini kwa ajili ya matakwa Yangu, kwa ajili ya mapenzi Yangu? Je, inawezekana kwamba mnalitukuza jina Langu takatifu kwa vinywa vyenu lakini ndani ya mioyo yenu mnanichukia sana? Kunifanyia kazi, kuridhisha moyo Wangu, pamoja na kujielewa wenyewe na kuasi joka kubwa jekundu si kazi rahisi na lazima mlipe gharama ili kufanya hivyo. Ninaposema "gharama" mnalielewaje hilo? Sitalijadili hivi sasa kwa kuwa Siwapi watu majibu ya moja kwa moja. Badala yake, Nawaruhusu wote kulifikiria wenyewe, na baadaye, watumie vitendo na tabia zao kujibu maswali Yangu kwa kweli. Je, mnaweza kufanya hilo?
Aprili 27, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni