6.19.2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Nane


Kanisa la Mwenyezi MunguTamko la Thelathini na Nane

Kotekote katika uzoefu wa wanadamu umbo Langu halijakuwepo, wala kuwepo kwa uongozi wa maneno Yangu, na kwa hiyo Nimemuepuka mwanadamu kwa umbali kila mara na kisha Nikaondoka kwake. Nadharau uasi wa wanadamu. Sijui kwa nini. Inaonekana Nimemchukia mwanadamu tangu mwanzo, na bado Nahisi huruma kubwa kwake. Na kwa hiyo mwanadamu ananiangalia na mioyo miwili, kwani Nampenda mwanadamu, na pia Namchukia mwanadamu. Ni nani kati yao huonyesha ufahamu halisi wa upendo Wangu? Na ni nani anaweza kuelewa chuki Yangu? Machoni Pangu, mwanadamu ni kitu kilichokufa, bila uhai, kama kwamba ni sanamu za udongo zinazosimama miongoni mwa vitu vyote. Wakati mwingine, kutotii kwa wanadamu huipa msukumo hasira Yangu kwao. Nilipoishi miongoni mwa wanadamu, wangenipa tabasamu hafifu Nilipofika ghafla, kwa sababu walikuwa daima wananitafuta kwa makusudi, kama kwamba Nilikuwa Nacheza nao duniani. Hawakunizingatia kwa dhati, na kwa sababu ya mtazamo wao Kwangu Sikuwa na budi ila "kustaafu" kutoka kwa "wakala" wa wanadamu. Bado, Nataka kutangaza kwamba ingawa "Nimestaafu," "pensheni" Yangu haiwezi kupungua kwa senti moja. Kwa sababu ya "ukubwa wa cheo" Changu katika "wakala" wa wanadamu, Naendelea kudai malipo kutoka kwao, malipo ambayo Nawadai. Ingawa mwanadamu ameniacha, angewezaje kuepuka fumbato Langu? Nililegeza fumbato Langu kwake kwa kiasi fulani, kumruhusu kujiingiza katika tamaa zake za mwili, na hivyo alithubutu kuwa jeuri, bila kizuizi, na inaweza kuonekana kuwa hakunipenda kweli, kwa vile aliishi katika mwili. Yawezekana kwamba upendo halisi unatakiwa kupatikana kutoka kwa mwili? Yawezekana kwamba yote Niombayo kwa mwanadamu ni "upendo" wa mwili? Kama huu kwa hakika ungekuwa ukweli, basi mwanadamu angekuwa na thamani gani? Wote ni takataka isiyo na thamani! Zisingekuwa "nguvu Zangu za mwujiza" za kudumu, Ningekuwa Nimemwacha mwanadamu zamani sana—hata ni kwa nini kusumbuka kukaa pamoja naye na kukubali "dhuluma" ya mwanadamu? Lakini Nilivumilia. Nilitaka kufikia msingi wa shughuli za mwanadamu. Nitakapomaliza tu kazi Yangu duniani Nitapaa juu mbinguni ili kumhukumu "bwana" wa vitu vyote; hii ni kazi Yangu ya msingi, kwa maana tayari Nimemdharau mwanadamu sana. Ni nani asingemchukia adui yake? Nani asingemwangamiza adui yake? Mbinguni, Shetani ni adui Yangu, duniani, mwanadamu ni adui Yangu. Kwa sababu ya muungano kati ya mbingu na dunia, vizazi tisa vyao vinapaswa kuchukuliwa kuwa na hatia kwa ushirikiano, na hakuna atakayesamehewa. Nani aliwaambia wanipinge? Ni nani aliwaambia waniasi? Ni kwa nini mwanadamu hawezi kujifundua kwa asili yake ya kale? Kwa nini mwili wake daima huongezeka ndani yake? Yote haya ni ushahidi wa hukumu Yangu kwa mwanadamu. Ni nani anayethubutu kutoshindwa na ukweli? Nani anayethubutu kusema hukumu Yangu imeathiriwa na hisia? Mimi ni tofauti na mwanadamu, kwa hiyo Nimeondoka kwake, kwa maana Mimi si mwanadamu hasa.
Kila kitu Ninachofanya kina madhumuni; wakati mwanadamu "anapofichua" “ukweli” Kwangu, Namsindikiza kwenye “uwanja wa kuua,” kwa kuwa hatia ya wanadamu inatosha kustahili kuadibu Kwangu. Na kwa hiyo Siwaadibu watu bila kutambua; badala yake, kuadibu Kwangu juu yao daima kunafaa ukweli wa dhambi zao. La sivyo wanadamu hawangeinama kamwe na kukubali hatia yao Kwangu kwa sababu ya uasi wao. Watu wote wanainamisha vichwa vyao kwa kusita kwa sababu ya hali ya sasa, lakini mioyo yao bado haijaridhika. Nawapa watu "bari" kunywa, na kwa hiyo viungo vyao ndani yao huonekana wazi mbele ya "lenzi"; uchafu na kinyaa ndani ya tumbo la mwanadamu bado hayajafutwa. Aina mbalimbali za uchafu hububujika kupitia mishipa yao, kwa hiyo sumu ndani yao inakua. Kwa kuwa mwanadamu ameishi namna hii kwa muda mrefu ameizoea na haioni kuwa ya ajabu. Kutokana na hilo, viini vya maradhi ndani yao hukomaa, kuwa asili yao, na kila mtu huishi chini ya utawala wao. Ndiyo sababu watu wanafanana na farasi mwitu, wakikimbia huku na huko kila mahali. Hata hivyo, wao kamwe hawalikubali hili kikamilifu lakini wanaashiria tu kwa vichwa vyao ili kuonyesha kwamba "wameridhika." Ukweli ni kwamba mwanadamu hatilii neno Langu maanani. Kama angelichukua neno langu kama dawa, basi "angefuata amri za daktari," na angeruhusu dawa itibu ugonjwa ndani yake. Hata hivyo, moyoni Mwangu, mwenendo wake hauwezi kutimiza tamaa hii, na hivyo Naweza tu "kusalimu amri," na kuendelea kuongea naye. Kama anasikia au la, Ninafanya tu wajibu Wangu. Mwanadamu hayuko radhi kufurahia baraka Zangu na angepitia maumivu makali ya jahanamu, hivyo siwezi kufanya chochote zaidi kuliko kukubali ombi lake. Hata hivyo, ili jina Langu na Roho Wangu visiaibishwe jahanamu, Nitamfundisha nidhamu kwanza na kisha "Nitii" matakwa yake, na kufanya hivyo ili aweze kupata "furaha ya dhati." Siko radhi kumruhusu mwanadamu aniaibishe Mimi chini ya bendera Yangu wakati wowote au mahali popote, ndiyo maana Namfundisha nidhamu mara kwa mara. Bila kizuizi cha maneno makali Ninayonena, mwanadamu angewezaje kusimama mbele Yangu leo? Je, watu hawaepuki dhambi tu kwa sababu wanaogopa Nitaondoka? Je, si kweli kwamba hawalalamiki tu kwa sababu wanaogopa kuadibu? Ni mapenzi ya nani ambayo ni kwa ajili ya mpango Wangu tu? Watu wote wanadhani kwamba Mimi ni uungu unaokosa "ubora wa akili," lakini ni nani anayeweza kuelewa kwamba Naweza kubaini kila kitu katika ubinadamu? Ni kama wanavyosema watu kabisa, "Kwa nini kugonga msumari kwa nyundo kubwa?" Mwanadamu "ananipenda", si kwa sababu upendo wake Kwangu Mimi ni wa asili, lakini kwa sababu anaogopa kuadibu. Nani kati ya wanadamu alizaliwa akinipenda? Ni nani ananitendea kama kwamba Mimi ni moyo wake mwenyewe? Na kwa hiyo Najumlisha hili na neno la hekima kwa ulimwengu wa binadamu: Miongoni mwa wanadamu, hakuna yeyote anayenipenda.
Kwa vile Nataka kukamilisha kazi Yangu duniani, Nimeharakisha mwendo wa kazi Yangu kwa njia hii ili mwanadamu asije akarushwa mbali na Mimi, mbali sana kiasi cha kuanguka ndani ya bahari isiyo na mipaka. Ni kwa sababu Nimemwambia uhalisi wa mambo mapema ndio maana amejihadhari kwa kiasi fulani. Isingekuwa kwa ajili ya hili, ni nani angeweza kuinua matanga anapokuwa karibu kukabiliwa na upepo mkali na mawimbi? Watu wote wanafanya kazi ya kuwa macho. Ni kama kwamba Nimekuwa "jambazi" machoni pao. Wanaogopa kwamba Nitawanyang’anya vitu vyote vilivyo ndani ya nyumba zao, na hivyo wote wanasukuma "milango" yao kwa nguvu zote wanazoweza kukusanya, wakiwa na hofu kubwa sana kwamba Nitaingia ghafla. Ninapowaona wakiwa na tabia kama panya wenye hofu, Naondoka kimya. Katika mawazo ya wanadamu, inaonekana kuwa "ufunuo" unakuja ulimwenguni, na kwa hiyo wote wanakimbia kwa mchafukoge, wakitishwa sana. Ni wakati huo tu ndio Naweza kuona pepo wakizurura duniani. Sina budi ila kucheka, na katikati ya sauti ya kicheko Changu mwanadamu anashangaa na kuogopa. Hapo ndipo Natambua ukweli, na kwa hiyo Nazuia tabasamu Yangu, na Sikagui dunia tena, badala yake Narudia mpango Wangu wa awali. Sitawachukulia tena wanadamu kama mfano ambao hutumikia kama sampuli ya utafiti Wangu, kwa sababu wao ni masalio tu. Mara tu Ninapowatupa, hawana matumizi yoyote tena—wao ni chembe za taka. Wakati huu, Nitawaondoa kabisa na kuwatupa motoni. Katika akili ya mwanadamu, hukumu Yangu, uadhamu, na ghadhabu vina rehema Yangu na wema Wangu. Lakini hajui hata kidogo kwamba Nimeipuuza udhaifu wake kwa muda mrefu, na kwamba Nilifuta rehema Yangu na huruma Yangu kitambo sana, na ndiyo maana yuko katika hali waliyo ndani sasa. Hakuna mtu anayeweza kunijua, wala hawezi kuyaelewa maneno Yangu au kuuona uso Wangu, wala hawezi kufahamu maana ya mapenzi Yangu. Je, hii siyo hali ya sasa ya mwanadamu? Basi, mtu anawezaje kusema kuwa Nina huruma au wema? Sijali kuhusu udhaifu wake, na Sizingatii kasoro zake. Je, hii bado ni rehema Yangu na huruma? Na bado ni upendo Wangu kwake? Watu wote huamini kwamba Mimi huchuja hotuba Yangu kwa ajili ya desturi, na kwa hiyo hawaamini maneno Ninayosema. Lakini ni nani anayeelewa "Kwa kuwa hii ni enzi tofauti rehema na huruma Zangu hazipo sasa; lakini Mimi daima ni Mungu Afanyaye Anavyosema"? Mimi Niko miongoni mwa wanadamu, na katika akili za watu wananiona kama Aliye Juu Zaidi, na kwa hiyo mwanadamu anaamini kwamba Napenda kusema kwa kutumia hekima Yangu. Hivyo, mwanadamu daima huchukulia neno Langu kwa shaka. Lakini ni nani anayeweza kuelewa sheria zinazounga mkono hotuba Yangu? Nani anayeweza kuelewa asili ya maneno Yangu? Nani anayeweza kufahamu kile Ninachotaka kufanikisha kwa kweli? Nani anaweza kubaini utondoti wa hitimisho la mpango Wangu wa usimamizi? Nani anayeweza kuwa msiri Kwangu? Katika vitu vyote, ni nani isipokuwa Mimi anayeweza kuelewa ni nini hasa Ninachofanya? Na ni nani anayeweza kujua lengo Langu kuu?
Aprili 30, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni