10.23.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.

Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, unajua una nafsi za aina gani? Je, una uwezo wa kuhisi nafsi yako? Unaweza kugusa nafsi yako? Je, unaweza kuhisi roho yako inafanya nini? Hujui, siyo? Kama unaweza kuhisi au kugusa kitu fulani kama hicho, basi ni roho mwingine aliye ndani yako akifanya kitu kwa nguvu—akikufanya utende na kusema vitu. Hilo ni jambo lililo nje yako, lisilo la asili kwako. Wale wenye pepo mbaya watakuwa na ufahamu wa kina wa hili.

10.22.2019

Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

10.21.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtumishi mwema na mtumishi muovu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu.

10.20.2019

Kuna tofauti ipi kati ya ngano na magugu?


Maneno Husika ya Mungu:
Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetni haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu.

10.19.2019

Kumfuata mtu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni.

10.18.2019

Kumfuata Mungu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

      Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno halisi ya Mungu: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno halisi ya Mungu. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno halisi ya Mungu, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu.

10.17.2019

Asiyeamini ni nini?





Maneno Husika ya Mungu:

      Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini.

10.16.2019

Unafiki ni nini?







Maneno Husika ya Mungu:
Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli. Hali yake ya kweli imefichwa ndani ya moyo wake; haionekani. Watu wasipofuatilia ukweli, kama hawaelewi ukweli, basi maarifa yao ya kidini na nadharia ambazo wamepata zinakuwa nini? Je, zinakuwa maneno ya mafundisho ambayo watu huzungumzia mara nyingi? Watu hutumia haya yanayodaiwa kuwa mafundisho sahihi kujifanya na kujionyesha kuwa wazuri.

10.15.2019

Kiongozi wa uongo au mchungaji wa uongo ni nini? Je, kiongozi wa uongo au mchungaji wa uwongo anaweza kutambuliwaje?



Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu.

10.14.2019

Kristo wa uongo ni nini? Kristo wa uongo anaweza kutambuliwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.
kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena.

10.13.2019

Mpinga Kristo ni nini? Mpinga Kristo anaweza kutambuliwaje?


Maneno Husika ya Mungu:
Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu.