Ingawa wachungaji na wazee wa kanisa wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na wanaitembea njia ya Mafarisayo wanafiki, tunamwamini Bwana Yesu, sio wachungaji na wazee wa kanisa, kwa hiyo unawezaje kusema kwamba sisi pia tunaitembea njia ya Mafarisayo? Je, hatuwezi kuokolewa kwa kumwamini Mungu ndani ya dini?
Jibu:
Kuna watu wengi katika dini ambao wanaamini na kuabudu bila kufikiria na kufuata Mafarisayo. Kwa hiyo kama njia wanayoenda ni njia ya Mafarisayo ni dhahiri mara tu unapofikiri juu yake. Unathubutu kusema kuwa unaabudu na kuwalinda Mafarisayo katika moyo wako lakini huna uhusiano na dhambi zao? Unathubutu kusema kuwa unawafuata Mafarisayo wanafiki, lakini wewe si kama wao, mtu anayepinga Mungu? Je, bado hatuwezi kung’amua swali rahisi kama hilo? Aina ya mtu unayefuata ni aina ya njia unayotembea. Ikiwa unawafuata Mafarisayo basi uko kwenye njia ya Mafarisayo. Ukitembea njia ya Mafarisayo basi wewe kiasili ni aina hiyo ya mtu kama Mafarisayo.