Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hushikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na watu wengi huwatii na kuwafuata—huu ni ukweli. Unasema kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hawaukubali ukweli wa Mungu kuwa amekuwa mwili, kwamba hawaamini ukweli ulioonyeshwa na Mungu mwenye mwili na kwamba wanaitembea njia ya Mafarisayo, na tunakubaliana na jambo hili. Lakini kwa nini unasema kuwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote ni Mafarisayo wanafiki, kuwa wote ni wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kwamba wataingia katika maangamizo mwishoni? Hatuwezi kukubali jambo hili kwa wakati huu. Tafadhali shiriki unachotegemeza dai hili, kwamba watu hawa hawawezi kuokolewa na kwamba ni lazima wote waingie katika maangamizo.
Jibu:
Asili ya jinsi watu katika jamii ya kidini wanavyomkana Mungu zinaweza tu kufichuliwa na kuchanguliwa baada ya kuja kwa Kristo mwenye mwili. Hakuna wanadamu wapotovu wanaoweza kuutambua ukweli na asili ya jamii ya kidini ya kumkana Mungu, kwa sababu wanadamu wapotovu hawana ukweli. Wanaweza tu kudhibitiwa, kuchanganywa, na kuchezewa na wachungaji wa uwongo na pepo wapinga Kristo ili kujiunga nao katika kufanya uovu, na kuwa watumishi na washiriki wa Shetani katika kumkana Mungu. Hili ni jambo la kawaida. … Hebu tuone jinsi, wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alivyoufichua ukweli na asili ya jinsi pepo wabaya wapinga Kristo katika jamii ya kidini walivyomuasi Mungu daima: