Kwa miaka elfu mbili, imani ya mwanadamu katika Bwana imekuwa imetegemezwa Biblia, na kuja kwa Bwana Yesu hakukuikanusha Biblia ya Agano la Kale. Baada ya Mwenyezi Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, kila mtu anayemkubali Mwenyezi Mungu atalenga kula na kunywa maneno ya Mwenyezi Mungu na aitasoma Biblia mara chache tena. Kile ninachopenda kufuatilia ni, baada ya mtu kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ni mtazamo gani sahihi hasa mtu anafaa kuwa nao kwa Biblia, na mtu anafaa kuitumia kwa jinsi gani? Imani ya mtu katika Mungu inafaa itegemezwe nini ili mtu aitembee njia ya imani katika Mungu na kupata wokovu wa Mungu?
Jibu:
Biblia ni kumbukumbu halisi ya hatua za kwanza mbili za kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, ambazo zinahitimisha uongozi na ukombozi wa wanadamu baada ya kuumbwa kwa mbingu na dunia na vitu vyote, pamoja na wanadamu. Kutokana na kuisoma Biblia, kila mmoja anaweza kuona jinsi Mungu aliwaongoza wanadamu wakati wa Enzi ya Sheria na kuwafundisha kuishi mbele Zake na kumwabudu Yeye. Tunaweza kuona pia jinsi Mungu aliwakomboa wanadamu wakati wa Enzi ya Neema na kuwasamehe dhambi zao zote zilizopita huku akiwapa amani, furaha, na kila aina ya neema. Watu hawawezi tu kuona kwamba Mungu alikuwa amewaumba wanadamu, bali pia kwamba Yeye alikuwa amewaongoza kwa uthabiti na halafu akawakomboa.