Unashuhudia kuwa katika siku za mwisho Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa, lakini baada ya kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ninaona kwamba baadhi yayo humhukumu na kumlaani mwanadamu. Kama Mungu humhukumu na kumlaani mwanadamu, si basi mwanadamu atapatwa na adhabu? Na unawezaje kusema kwamba aina hii ya hukumu huwatakasa na kuwaokoa wanadamu?
Jibu:
Katika siku za mwisho, Mungu huonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili kuunda kikundi cha washindi, kundi la wale ambao ni wenye moyo mmoja na akili moja na Mungu. Hii iliamuliwa na Mungu alipoumba ulimwengu. Unaweza kusema kuwa tayari Mungu amelifanya kundi la washindi, kwamba wote wamefanyika kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kwamba wametoka katika taabu za mateso ya kikatili ya Chama Cha Kikomunisti cha China. Ni ukweli kwamba tayari Mungu amefanya jambo hili; hakuna mtu anayeweza kulipinga. Kuna watu wengine ambao wanaona kwamba baadhi ya maneno ya Mungu yana shutuma na laana ya watu na wao hukuza mawazo. Huu ni upumbavu. Hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni kiti cheupe cha enzi cha hukumu kilichotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo.