6.26.2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tatu

Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu


Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake. Basi Mungu hutumia kiwango gani katika kuasisi matokeo ya binadamu? Kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya binadamu—hii ndiyo inaingiliana zaidi na dhana za watu.

6.25.2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu


Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi?

6.24.2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tano


Majaliwa ya Binadamu Yanaamuliwa na Mwelekeo Wake Kwa Mungu


      Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo.

6.23.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia


Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo.

6.22.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Pili


Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Nilipata dondoo hizi mahususi kama nyenzo za marejeleo ili kuwasaidia kujua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Hapa Nitayashiriki nanyi ili muweze kuona ni aina gani ya tabia na kiini cha Mungu ambacho kimefichuliwa kupitia kwa kazi Yake ya kitambo lakini watu hawajui kukihusu.

6.21.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Sehemu ya Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia



Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.

Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. Mungu alimruhusu Nuhu kujenga safina ili kuokoa familia yake ya wanane, kuwaruhusu kuweza kuishi, ili kuwa babu wa kizazi kifuatacho cha wanadamu. Sasa hebu tuyasome maandiko.

6.20.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne


3) Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu.

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

6.19.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Pili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli


Katika kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.

Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.

6.18.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne


Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si makaragosi Yake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi.

6.17.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa wanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

6.16.2019

"Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tatu"


Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye.

6.15.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli

Kuhusu Ayubu


      Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!


Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake


      Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: "hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu."