6.17.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,ukweli

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa wanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli


Kisha, hebu tuangalie kile Mungu alimfanyia Ibrahimu. Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: "Umchukue mwana wako sasa, mwana wako wa pekee Isaka, unayempenda, na uende hadi nchi ya Moria; na huko umtoe kwa sadaka ya kuteketezwa juu ya mojawapo ya milima ambayo nitakuambia." Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa minajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kupata mtoto, Mungu alimwomba amtoe mwana wake—haiwezekani! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio halisi la Mungu lilikuwa nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Katika mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya "kuunda tatizo pasipo na tatizo." Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji mengi sana. Ingawaje alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: "Naye Ibrahimu akaamka asubuhi mapema, na kuweka tandiko kwa punda wake, akawachukua vijana wake wawili pamoja naye, naye Isaka mwana wake, na akapasua kuni kwa sababu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, na akaondoka, na kuenda pahali ambapo alikuwa ameambiwa na Mungu" (Mwa 22:3). "Na wakafika pahali hapo ambapo Mungu alikuwa amemwambia; naye Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, na kuziweka kuni kwa mpango, na kumfunga Isaka mwana wake, naye akamlaza juu ya madhabahu kwa zile kuni. Na Ibrahimu akanyosha mbele mkono wake, na kukichukua kisu ili amchinje mwana wake" (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake, na kukichukua kisu ili kumwua mtoto wake, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili kumwua mtoto wake—hilo lilionyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu—utiifu uleule ambao Yeye Alitamani.

Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kupangilia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni ukosefu wa mwafaka huu na kutofahamu ndiyo majaribio ya Mungu na mtihani wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kushibisha mahitaji ya Mungu. Hapo tu, wakati Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na wanadamu—kwa Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na hakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawaje lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi furaha, Alihisi upendo wa binadamu kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati huu ambao Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili kumwua Isaka, Mungu alimsimamisha? Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumpa Isaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Yaweza kusemekana kwamba matokeo haya yalimtosheleza Mungu na kwamba ndiyo ambayo Mungu alitaka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawaje, katika miktadha tofauti, Mungu anatumia njia tofauti za kupima kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya "kutokuwa na masharti" ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeachana na ile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii yaonyesha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado hajapata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumuua mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Ni jambo la kiasili, hivyo basi, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli? Tutaachia hapa kwa mada hii. Halafu, tutasoma "Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu."

3. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu


Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Huu ni ukamilifu wa maelezo ya baraka za Mungu kwa Ibrahimu. Ingawaje ni fupi, maudhui yake ni mengi: Yanajumuisha sababu ya, na usuli wa, zawadi ya Mungu kwa Ibrahimu, na kile ambacho Alimpa Ibrahimu. Unao pia mhemko wa furaha na msisimko Aliotumia Mungu kutamka maneno haya, pamoja na haraka ya tamanio Lake la kupata wale wanaoweza kusikiliza maneno Yake. Katika haya, tunaona upendo wa Mungu kwa, na wema Wake kwa, wale wanaotii maneno Yake na kufuata amri Zake. Hivyo, pia, tunaiona gharama Anayolipia ili kupata watu, na utunzaji na fikira Anazotumia kuweza kuwapata. Zaidi ya hayo, kifungu hicho, kilicho na maneno "Mimi nimeapa kujipitia," kinatupa hali ya nguvu ya machungu na maumivu Aliyoyapitia Mungu, na Mungu pekee, usiri wa kazi hii ya mpango wa usimamizi. Ni kifungu cha kuchokonoa fikira, na kile ambacho kilikuwa na umuhimu maalum kwa, na ilikuwa na athari nyingi ajabu kwa wale waliokuja baadaye.

Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake

Je, baraka aliyopewa Ibrahimu na Mungu tuliyoisoma hapa ni kubwa? Ilikuwa kubwa vipi? Kunayo sentensi moja muhimu hapa: "Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa," ambayo inaonyesha kwamba Ibrahimu alizipokea baraka ambazo hazikupewa tena kwa mwingine aliyekuja kabla au baadaye. Wakati, alipoulizwa na Mungu, Ibrahimu alimrudisha mwana wake wa pekee—mtoto wake pekee wa kiume na mpendwa Isaka—kwa Mungu (dokezo: Hapa hatuwezi kutumia neno "tolewa sadaka"; tunafaa kusema alimrudisha mtoto wake kwa Mungu), Mungu naye hakumruhusu tu Ibrahimu kutoa Isaka, lakini pia Alimbariki. Ni kwa ahadi gani Alimbariki Ibrahimu? Ahadi ya kuzidisha watoto wake. Na walizidishwa mara ngapi? Maandiko yanatuelezea rekodi hii: "mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa." Mungu Aliyatamka maneno haya katika muktadha upi? Hivi ni kusema, ni vipi ambavyo Ibrahimu alipokea baraka za Mungu? Alizipokea kama vile tu Mungu anavyosema kwenye maandiko: "kwa kuwa umeitumikia sauti yangu." Yaani, kwa sababu Ibrahimu alikuwa amefuata amri ya Mungu, kwa sababu alikuwa amefanya kila kitu ambacho Mungu alikuwa amesema, kuomba na kuamuru bila ya malalamiko hata kidogo, hivyo Mungu akatoa ahadi hiyo kwake. Kunayo sentensi moja muhimu katika ahadi hii ambayo inagusia fikira za Mungu wakati huo. Je, mmeiona? Huenda hamkutilia maanani sana maneno ya Mungu kwamba "Mimi nimeapa kujipitia." Yale yanamaanisha ni kwamba, wakati Mungu alipoyatamka maneno haya, Alikuwa anajiapisha Mwenyewe. Watu huapa kwa yapi wakati wanapokula kiapo? Wanaapa kwa Mbingu, hivi ni kusema, wanakula kiapo na jina la Mungu na kuapa kwa jina la Mungu. Huenda watu wasiwe na uelewa mwingi wa hali hiyo ambayo Mungu Alijiapisha mwenyewe, lakini mtaweza kuelewa Nitakapowapatia maelezo sahihi. Kukabiliwa na mtu ambaye aliweza tu kuyasikia maneno Yake lakini kutoelewa moyo Wake kwa mara nyingine kulimfanya Mungu kuhisi mpweke na mwenye upungufu. Katika hali ya kukata tamaa—na, yaweza kusemekana, kwa nadhari—Mungu alifanya kitu cha kiasili sana: Mungu aliuweka mkono Wake kwenye moyo wake na kutamka ahadi ya zawadi kwa Ibrahimu kwake Yeye Mwenyewe, na kutokana na haya binadamu akamsikia Mungu akisema "Mimi nimeapa kujipitia." Kupitia vitendo vya Mungu, unaweza kujifikiria wewe mwenyewe. Unapoweka mkono wako juu ya moyo wako, na kujizungumzia, unalo wazo wazi kuhusu kile unachosema? Je, mwelekeo wako ni wa uaminifu? Unaongea waziwazi, kwa kutumia moyo wako? Hivyo, tunaona hapa kwamba wakati Mungu alipomzungumzia Ibrahimu, Alikuwa mwenye bidii na wa ukweli. Wakati huohuo alipokuwa Akiongea naye Ibrahimu na Akimbariki, Mungu alikuwa pia Akijizungumzia Mwenyewe. Alikuwa Akijiambia: Nitambariki Ibrahimu na kuuzidisha uzao wake kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani, kwa sababu alitii maneno Yangu na ndiye Niliyemchagua. Wakati Mungu aliposema "Mimi nimeapa kujipitia," Mungu Aliamua kwamba ndani ya Ibrahimu Angezalisha wateule wa Israeli, na baadaye Angewaongoza watu hawa kusonga mbele sambamba na kazi Yake. Yaani, Mungu angekifanya kizazi cha Ibrahimu kufanya kazi ya usimamizi wa Mungu, na kazi ya Mungu na ile iliyoonyeshwa na Mungu ingeanza na Ibrahimu, na kuendelea katika vizazi vya Ibrahimu, na hivyo kuthamini tamanio la Mungu la kuokoa binadamu. Mnasemaje, hiki si kitu kilichobarikiwa? Kwa binadamu, hakuna baraka kubwa zaidi kuliko hii; hii, inaweza kusemekana, ndiyo baraka kubwa zaidi. Baraka aliyopata Ibrahimu haikuwa kuzidishwa kwa uzao wake, lakini ilikuwa Mungu kutimiza usimamizi Wake, agizo Lake na kazi Yake kwa vizazi vya Ibrahimu. Hii inamaanisha kwamba baraka alizopata Ibrahimu hazikuwa za muda, lakini ziliendelea kwa kadri mpango wa usimamizi wa Mungu ulipoendelea. Wakati Mungu alipoongea, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, tayari Alikuwa ameamua. Je, mchakato wa uamuzi huu ulikuwa kweli? Ulikuwa halisi? Mungu aliamua kwamba, kuanzia hapo kuendelea, jitihada Zake, gharama Aliyolipia, kile Anacho na alicho, kila kitu Chake, na hata maisha Yake yangekabidhiwa Ibrahimu na vizazi vya Ibrahimu. Na ndivyo pia Mungu alivyoamua kwamba, kuanzia kwenye kundi hili la watu, Angeonyesha vitendo Vyake, na kumruhusu binadamu kuiona hekima, mamlaka na nguvu Yake.

Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika

Wakati huohuo Alipokuwa akijizungumzia Mwenyewe, Mungu alizungumza pia na Ibrahimu, lakini mbali na kusikiliza baraka ambazo Mungu alimpa, Ibrahimu aliweza kuyaelewa matamanio ya kweli ya Mungu katika maneno Yake yote wakati huo? Hakuweza! Na hivyo, kwa wakati huo, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, moyo Wake ulikuwa bado pweke na wenye huzuni. Hakukuwepo hata na mtu mmoja wa kuweza kuelewa au kufahamu kile Alichonuia na Alichopangilia. Wakati huo, hakuna—akiwemo Ibrahimu—aliyeweza kuongea na Yeye kwa ujasiri, isitoshe hakuna yule aliyeweza kushirikiana na Yeye katika kufanya kazi ambayo lazima Angefanya. Juujuu, Mungu alikuwa Amempata Ibrahimu na Alipata mtu ambaye angetii maneno Yake. Lakini kwa hakika, maarifa ya mtu huyu kuhusu Mungu yalikuwa kidogo mno. Hata ingawaje Mungu alikuwa amembariki Ibrahimu, moyo wa Mungu ulikuwa bado hujatosheka. Inamaanisha nini kwamba Mungu hakuwa ametosheka? Inamaanisha kwamba usimamizi Wake ulikuwa tu umeanza, inamaanisha kwamba watu Aliotaka kupata, watu Aliotamani kuona, watu Aliopenda, walikuwa bado mbali na Yeye; Alihitaji muda, Alihitaji kusubiri, Alihitaji kuwa na subira. Kwani kwa wakati huo, mbali na Mungu Mwenyewe, hakuna yeyote yule aliyejua kile Alichohitaji au kile Alichotaka kupata, au kile Alichotamani. Na hivyo basi, Kwa wakati huohuo aliokuwa akihisi sana furaha Mungu pia alihisi kuwa mwenye uzito wa moyo. Bado Hakusitisha hatua Zake, na Aliendelea kupanga hatua inayofuata ya kile ambacho lazima Afanye.

Mnaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu ya yeye kusikiliza maneno ya Mungu. Ingawaje, juujuu, hali hii yaonekana ya kawaida na suala ambalo bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa binadamu kwake Yeye, na hutunzwa mno na uelewa wa binadamu kuhusu Yeye na uaminifu wake Kwake. Mungu anathamini kiasi kipi uaminifu huu? Huenda msielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimwomba Ibrahimu kumkabidhi mtoto wake Kwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kiasi kipi? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Uradhi na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mikono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa "sadaka" ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kusubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilionyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kushinda na Yeye kumchukulia Yeye kwa uaminifu, kumtunza Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, yalikuwa tu ni matakwa, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Yeye alikuwa mtu aliyepungukiwa pakubwa na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa binadamu: kumjua Mungu, kuweza kushuhudia Mungu, na kuwa na akili sawa na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kufanya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kufahamu na kujua tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Kwa vile nimeyasema haya, mnatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua hakina uzito sana—lakini kitajitokeza kwa utaratibu!

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Tufuate: Neno la Mungu | "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Sehemu ya Tatu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni