6.18.2019

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I Uendelezo wa Sehemu ya Nne


Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si makaragosi Yake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi. Wala Hahisi kwamba kuokoa binadamu, kuwatosheleza, na kuwapatia kila kitu, ni kutoa mchango mkuu kwa binadamu. Anamkimu tu mwanadamu kimyakimya na kwa unyamavu, kwa njia Yake mwenyewe na kupitia kwa kiini Chake na kile Anacho na alicho. Haijalishi ni toleo kiasi kipi na ni msaada kiasi kipi ambao wanadamu wanapokea kutoka kwa Yeye, Mungu siku zote hajawahi kufikiri kuhusu au kujaribu kutaka sifa yoyote. Hii inaamuliwa na kiini cha Mungu, na pia hasa ni maonyesho ya kweli pia ya tabia ya Mungu. Na ndio maana, haijalishi kama iko kwa Biblia au kitabu chochote kingine, hatujawahi kumpata Mungu akionyesha fikira Zake, na hatujawahi kumpata Mungu akifafanua au akitangazia wanadamu ni kwa nini Anafanya mambo haya, au ni kwa nini Anamjali sana mwanadamu, ili kumfanya mwanadamu kumshukuru Yeye au kumsifu Yeye. Hata wakati Amejeruhiwa, wakati moyo Wake umo katika maumivu makali, Hajawahi kusahau jukumu Lake kwa mwanadamu au wasiwasi Wake kwa mwanadamu, huku haya yote yakiendelea, Anavumilia madhara na maumivu akiwa pekee katika ukimya. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu anaendelea kumkimu mwanadamu kama Anavyofanya siku zote. Ingawaje mwanadamu mara nyingi humsifia Mungu au huwa na ushuhuda Kwake, hakuna kati ya tabia hii ambayo imedaiwa na Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kunuia mambo yoyote mazuri Anayomfanyia binadamu yeye pia naye kumfanyia vivyo hivyo kama ishara ya shukrani au ili iweze kuonekana kwamba anafanyiwa mazuri aliyofanya. Kwa mkono mwingine, wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu, wale wanaomfuata Mungu kwa kweli, wanaomsikiliza Yeye, na walio waaminifu Kwake yeye, na wale wanaomtii Yeye—hawa ndio watu ambao mara nyingi watapokea baraka za Mungu, na Mungu atawakabidhi baraka hizo bila kusita. Isitoshe, baraka ambazo watu hupokea kutoka kwa Mungu mara nyingi zinazidi kufikiria kwao na pia zinazidi kitu chochote ambacho binadamu wanaweza kubadilishana na yale waliyofanya au gharama waliyolipia. Wakati mwanadamu anafurahia baraka za Mungu, Je, yupo yeyote anayejali ni nini Mungu anafanya? Je, yupo yeyote anayeonyesha wasiwasi wowote kuhusu vile ambavyo Mungu anahisi? Je, yupo yeyote anayethamini maumivu ya Mungu? Jibu la uhakika la maswali haya ni: La! Je, mwanadamu yeyote, akiwemo Nuhu, anaweza kuthamini yale maumivu ambayo Mungu alikuwa akihisi wakati huo? Je, mtu yeyote anaweza kufahamu ni kwa nini Mungu alianzisha agano kama hilo? Hakuna anayeweza! Mwanadamu hathamini maumivu ya Mungu si kwa sababu hawezi kuelewa maumivu ya Mungu, na si kwa sababu ya nafasi iliyopo kati ya Mungu na mwanadamu au tofauti kati ya hadhi yao; badala yake, ni kwa sababu mwanadamu hata hajali kuhusu hisia zozote za Mungu. Mwanadamu anafikiria Mungu yuko huru—Mungu hahitaji watu wa kujali kuhusu Yeye, kumwelewa au kumwonyesha namna anavyomfikiria. Mungu ni Mungu, hivyo Hana maumivu, hana hisia; Hatakasirika, Hahisi huzuni, hata Halii. Mungu ni Mungu, hivyo Hahitaji maonyesho yoyote ya kihisia na Hahitaji faraja yoyote ya kihisia. Kama Hahitaji mambo haya katika hali fulani, basi Atatatua mwenyewe na Hatahitaji usaidizi wowote kutoka kwa mwanadamu. Lakini kinyume chake ni kuwa, ni wale binadamu wanyonge, wanaohitaji tulizo, toshelezo, himizo la Mungu na hata pia kwake Yeye kuweza kutuliza hisia zao wakati wowote mahali popote. Fikira kama hiyo inajificha ndani kabisa ya mioyo ya mwanadamu: Binadamu ndiye mnyonge; wanahitaji Mungu ili awatunze kwa kila njia, wanastahili utunzaji wote wanaopokea kutoka kwa Mungu, na wanafaa kudai kutoka kwa Mungu chochote kile wanachohisi kinafaa kuwa ni chao. Mungu ndiye mwenye Nguvu; Anacho kila kitu, na Anahitaji kuwa mlezi wa mwanadamu na Anayetoa baraka. Kwa sababu Yeye tayari ni Mungu, Yeye Mwenyezi na Hahitaji katu chochote kutoka kwa mwanadamu.

Kwa vile binadamu hatilii maanani ufunuo wowote wa Mungu, hajawahi kuhisi huzuni, maumivu au furaha ya Mungu. Lakini kinyume chake ni kwamba, Mungu anajua maonyesho yote ya binadamu kama vile anavyojua sehemu ya kiganja cha mkono Wake. Mungu hutosheleza mahitaji ya kila mtu siku zote na pahali pote, akiangalia fikira zinazobadilika za kila mmoja na hivyo basi kuwatuliza na kuwahimiza, na kuwaongoza na kuwaangazia. Kuhusu mambo yote ambayo Mungu amemfanyia mwanadamu, na gharama zote Alizolipia kwa sababu yao, watu wanaweza kupata kifungu kutoka kwa Biblia au kutoka kwa chochote ambacho Mungu amesema mpaka sasa kinachoelezea waziwazi kwamba Mungu atadai kitu kutoka kwa binadamu? La! Kinyume cha mambo, haijalishi ni vipi watu wanapuuza kufikiria kwa Mungu, Bado Anawaongoza kwa marudio wanadamu, Anamkimu kwa kurudia mwanadamu na kumsaidia, kuwaruhusu kufuata njia za Mungu ili waweze kupokea hatima nzuri ambayo Amewatayarishia. Inapokuja kwa Mungu, kile Anacho na alicho, neema Yake, rehema Yake, na tuzo Zake zote, zitakabidhiwa bila ya kusita kwa wale wanaompenda na kumfuata Yeye. Lakini hajawahi kufichua kwa mtu yeyote maumivu aliyopitia Yeye au hali ya akili Yake, na katu halalamiki kuhusu yeyote ambaye hamtilii Yeye maanani au hajui mapenzi Yake. Anavumilia tu haya yote kimyakimya, akisubiria siku ambayo mwanadamu ataweza kuelewa.

Kwa nini Nasema mambo haya hapa? Ni nini mnachoona kutoka kwa mambo haya Niliyosema? Kuna kitu katika kiini na tabia ya Mungu ambacho ndicho rahisi zaidi kupuuza, kitu ambacho kinamilikiwa tu na Mungu na wala si mtu yeyote, wakiwemo wale wengine wanafikiria kwamba ni watu wakubwa, watu wazuri, au Mungu wa kufikiria kwao. Kitu hiki ni nini? Ni kule kutokuwa na nafsi kwa Mungu. Tunapozungumzia kutokuwa na nafsi, unaweza kufikiria kwamba pia wewe huna nafsi, kwa sababu inapokuja kwa watoto wako, haujadiliani juu ya bei na wao na wewe ni mkarimu sana kwao, au unafikiria kwamba wewe huna nafsi sana inapokuja kwa wazazi wako. Haijalishi ni nini unafikiria, angaa unayo dhana ya neno "kutokuwa na nafsi" na unalifikiria kama neno zuri, na kwamba kuwa mtu asiye na nafsi ni jambo la kipekee. Wakati huna nafsi, unafikiri kuwa wewe ni mkubwa. Lakini hakuna mtu anayeweza kuona kutokuwa na nafsi kwa Mungu miongoni mwa viumbe wote, miongoni mwa watu, hafla, na vitu, na kupitia kazi ya Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Kwa sababu binadamu ni mchoyo sana! Kwa nini Ninasema hivyo? Mwanadamu anaishi katika ulimwengu wa uyakinifu. Unaweza kumfuata Mungu, lakini huoni wala kushukuru namna ambavyo Mungu anakukimu, anavyokupenda na anavyoonyesha kwamba anakujali. Kwa hivyo unaona nini? Unaona watu wako wa ukoo wanaokupenda au kukupenda sana. Unayaona mambo ambayo ni ya manufaa kwa mwili wako, unajali kuhusu watu na vitu unavyopenda. Huku ndiko kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakodaiwa. Watu kama hao "wasiokuwa na nafsi" hata hivyo, huwa hawajali katu kuhusu Mungu anayewapa maisha. Kinyume na Mungu, kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakuwa cha nafsi na yenye uchoyo. Kutokuwa na nafsi ambako binadamu anasadiki katika ni ulio mtupu na usio halisi, uliotiwa madoa, usiolingana na Mungu, na usiohusika na Mungu. Kutokuwa na nafsi kwa binadamu ni kwa ajili yake, huku kutokuwa na nafsi kwa Mungu ni ufunuo wa kweli wa kiini Chake. Ndipo hasa kutokana na kujitolea nafsi kwa Mungu ndipo binadamu anapokea mfululizo usiosita wa ujazo kutoka kwake. Huenda msiathirike sana na mada hii Ninayozungumza kuhusu leo na unaweza kuwa tu unatikisa kichwa chako kwa kukubaliana nami, lakini wakati unapojaribu kufurahia moyo wa Mungu katika moyo wako, utaweza kwa kutojua kugundua: Miongoni mwa watu wote, masuala, na mambo unaweza kuhisi katika ulimwengu huu ni kutokuwa na nafsi tu kwa Mungu ambako ni kweli na dhabiti, kwa sababu ni upendo wa Mungu tu kwako ndio ambao hauna masharti na hauna madoa. Mbali na Mungu, kutokuwa na kile kinachodaiwa kutokuwa na nafsi wa mtu mwingine ni bandia, cha juujuu, kisicho na msingi; kina kusudio, nia fulani, kinatekeleza shughuli ya masikilizano, na hakiwezi kupimwa kamwe. Mnaweza hata kusema kwamba ni ki chafu, na cha kudharauliwa. Je, mnakubali?

Ninajua hamjazoeana na mada hizi na mnahitaji muda kidogo ili ziweze kuingia ndani yenu kabla muweze kuelewa kwa kweli. Kwa kadri mnavyokuwa kwamba hamjazoeana na masuala na mada hizi, ndipo inapothibitisha zaidi kwamba mada hizi zinakosekana katika mioyo yenu. Kama Singetaja mada hizi, yupo yeyote kati yenu ambaye angeweza kujua kidogo kuzihusu? Nasadiki hamngewahi pata kuyajua. Hii ni ya hakika. Haijalishi ni kiasi kipi mnachoweza kufahamu au kuelewa, kwa ufupi, mada hizi Ninazozungumzia ndizo ambazo watu wanakosa sanasana na wanazofaa kujua kuhusu zaidi. Mada hizi ni muhimu kwa kila mmoja—ni zenye thamani na ndiyo maisha, na ni mambo ambayo lazima mmiliki vizuri kwa safari ijayo. Bila ya maneno haya kama mwongozo, bila ya uelewa wako wa tabia ya Mungu na kiini, siku zote utabakia na alama ya kiulizo inapokuja kwa Mungu. Unawezaje kusadiki kwa Mungu kwa njia bora kama hata humwelewi Yeye? Hujui chochote kuhusu hisia Zake, mapenzi Yake, hali ya akili Yake, kile Anachofikiria, nini kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni, na nini kinachomfanya Yeye kuwa na furaha, hivyo unawezaje kuweka moyo wa Mungu katika fikira?

Kila wakati Mungu anapokuwa amekasirika, Anakumbana na mwanadamu ambaye hamtilii maanani kamwe, mwanadamu anayemfuata Yeye na anayedai kumpenda Yeye lakini anapuuza kabisa hisia Zake. Moyo Wake utakosaje kuumia? Katika kazi ya usimamizi ya Mungu, Anaitekeleza kwa dhati kazi Yake na Anaongea na kila mmoja Anawatazama bila kizuizi chochote au kujificha, lakini kinyume chake ni kuwa, kila mtu anayemfuata Yeye anatenganishwa na Yeye, na hakuna aliye radhi kujishughulisha na kuwa karibu na Yeye, kuelewa moyo Wake, au kutilia maanani hisia Zake. Hata wale wanaotaka kuwa wandani wa Mungu hawataki kuwa karibu na Yeye, kutilia maanani moyo Wake, au kujaribu kumwelewa Yeye. Wakati Mungu anashangilia na ana furaha, hakuna yeyote yule wa kushiriki katika furaha hiyo na Yeye. Wakati Mungu anakosa kueleweka na watu, hakuna mtu wa kutuliza moyo Wake ulio na majeraha. Wakati moyo Wake unaumia, hakuna hata mtu mmoja aliye radhi kumsikiliza Yeye na kuwa mwandani Wake. Katika hii maelfu ya miaka ya usimamizi wa kazi ya Mungu, hakuna mtu anayeelewa hisia za Mungu, hakuna hata mtu anayefahamu au kutambua hisia Zake, tupilia mbali hata yeyote ambaye angesimama kando ya Mungu ili kushiriki katika furaha na huzuni Zake. Mungu ni mpweke. Yeye ni pweke! Mungu ni mpweke si tu kwa sababu wanadamu waliopotoka wanampinga Yeye, lakini zaidi kwa sababu wale wanaofuatilia kuwa wa kiroho, wale wanaotafuta kumjua Mungu na kumwelewa Yeye, na hata wale walio radhi kujitolea maisha yao yote kwake Yeye, pia hawajui fikira Zake, na hawaielewi tabia Yake na hisia Zake.

Mwishoni mwa hadithi ya Nuhu, tunaona kwamba Mungu alitumia mbinu isiyo ya kawaida kuelezea hisia Zake wakati huo. Mbinu hii ni maalumu sana, na ni kuweka agano na binadamu. Ni mbinu inayotangaza mwisho wa matumizi ya gharika na Mungu katika kuangamiza ulimwengu. Kutoka nje, kuweka agano kunaonekana kuwa jambo lililo la kawaida sana. Si jambo lolote zaidi ya kutumia maneno kufunga wahusika ili wasitende vitendo vitakavyokiuka agano, ili kusaidia kutimiza kusudio la kulinda maslahi ya pande zote mbili. Kwa umbo, ni jambo la kawaida sana, lakini kutoka kwa motisha zilizopo na maana ya Mungu kufanya kitu hiki, ni ufunuo wa kweli wa tabia ya Mungu na hali Yake ya akili. Endapo utayaweka maneno haya kando na kuyapuuza, kama Sitawahi kukuambia ukweli wa mambo, basi binadamu hawatawahi kwa hakika kujua kufikiria kwa Mungu. Pengine katika kufikiria kwako Mungu anatabasamu wakati anapofanya agano hili, au pengine maonyesho Yake ni ya kumakinika, lakini haijalishi ni aina gani iliyo maarufu zaidi ya maonyesho Aliyonayo Mungu katika kufikiria kwa watu, hakuna mtu anayeweza kuona moyo wa Mungu au maumivu Yake, na hata upweke Wake. Hakuna mtu anayeweza kumfanya Mungu kumwamini au anayestahili kuaminiwa na Mungu, au kuwa mtu Anayeweza kueleza fikira Zake au kuwa mwandani Wake wa kuambia maumivu Yake. Ndiyo maana Mungu hakuwa na chaguo ila kufanya kitu kama hicho. Kwa juujuu, Mungu alifanya jambo rahisi la kuwaaga binadamu wale wa awali, kuhitimisha hali ya kale ilivyokuwa na kufikia hitimisho halisi katika kuangamiza Kwake kwa ulimwengu akitumia gharika. Hata hivyo, Mungu alikuwa ameyazika maumivu kutoka muda huu ndani kabisa ya moyo Wake. Kwa wakati ambao Mungu hakuwa na yeyote wa kuita mwandani, aliunda agano na wanadamu, akiwaambia kwamba asingeuangamiza ulimwengu kwa gharika tena. Wakati upinde wa mvua unapojitokeza ni kukumbusha watu kwamba, kitu kama hicho kiliwahi kufanyika, kuwapa onyo watu dhidi ya kufanya maovu. Hata katika hali hiyo ya maumivu, Mungu hakusahau kuwahusu wanadamu na bado akaonyesha kujali kwingi sana kwao. Je, huu si upendo na kutokuwa na nafsi kwa Mungu? Lakini nao watu wanafikiria nini wakati wanapoteseka? Kwani huu si wakati ambao wanamhitaji Mungu zaidi? Katika nyakati kama hizi, siku zote watu humkokota Mungu katika mambo yao ili Mungu aweze kuwapa tulizo. Haijalishi ni lini, Mungu hatawahi kuwavunja moyo watu wake, na siku zote Atawaruhusu watu kutoka katika changamoto zao na kuishi katika mwangaza. Ingawaje Mungu anawakimu wanadamu, ndani wa moyo wa binadamu, Mungu si chochote wala lolote ila tembe ya kumhakikishia tu mambo, dawa ya tulizo. Wakati Mungu anateseka, wakati moyo Wake una majeraha, kuwa na kiumbe aliyeumba au mtu yeyote wa kuwa mwandani wake au wa kumtuliza Yeye kwa kweli kwake Mungu ni tamanio tu la kibadhirifu asiloweza kutegemea. Siku zote binadamu hatilii maanani hisia za Mungu, hivyo Mungu siku zote haulizii wala hatarajii kuwa kuna mtu anayeweza kumtuliza Yeye. Anatumia mbinu Zake mwenyewe kueleza hali Yake. Watu hawafikirii kwamba ni jambo kubwa kwa Mungu kupitia mateso fulani, lakini unapojaribu tu kuelewa Mungu kwa kweli, unapoweza kushukuru kwa dhati, nia nzuri za Mungu katika kila kitu anachofanya, ndipo unapoweza kuhisi ukubwa wa Mungu na kutokuwa na nafsi kwake. Ingawaje Mungu aliunda agano na wanadamu kutumia upinde wa mvua, hakuwahi kuambia yeyote kwa nini alifanya hivi, kwa nini alianzisha agano hili, kumaanisha hakuwahi kuambia mtu fikira Zake halisi. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufahamu kina cha upendo ambao Mungu anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake mwenyewe, na hakuna pia mtu anayeweza kutambua ni kiasi kipi cha maumivu moyo Wake uliteseka wakati Alipoangamiza binadamu. Hivyo basi, hata kama Angeambia watu namna Anavyohisi, hawawezi kumwamini. Licha ya kuwa katika maumivu, angali Anaendelea na hatua inayofuata ya kazi Yake. Siku zote Mungu Anautoa upande wake bora zaidi na mambo bora zaidi kwa wanadamu huku yeye Mwenyewe Akistahimili kimyakimya mateso yote. Mungu kamwe hafichui mateso haya. Badala yake, Anayavumilia na kusubiri kwa kimya. Ustahimilivu wa Mungu si wa kimya tu, usio na hisia, au usio na suluhu, wala si ishara ya unyonge. Ni kwamba upendo na kiini cha Mungu siku zote yamekuwa bila nafsi. Huu ni ufunuo wa kiasili wa kiini na tabia Yake na maonyesho halisi wa utambulisho wa Mungu kama Muumba wa kweli.

Baada ya kusema hayo, baadhi ya watu wanaweza kufasili vibaya kile Ninachomaanisha. Je kufafanua hisia za Mungu kwa maelezo kama hayo, kwa hali ya hisia nyingi sana, inanuia kuwafanya watu kuhisi masikitiko kwa Mungu. Kulikuwa na nia kama hiyo? (La!) Kusudio la pekee la Mimi kusema maneno haya ni kuwafanya kujua Mungu kwa njia bora zaidi, kuelewa kila sehemu Yake, kuelewa hisia Zake, kutambua kiini na tabia ya Mungu, kwa uthabiti na kwa kidogo kidogo, iliyoelezewa kupitia kwa kazi Yake, kinyume na vile inavyotumiwa kupitia kwa maneno matupu ya binadamu, barua na mafundisho yao ya kidini, au kufikiria kwao. Hivi ni kusema, Mungu na kiini cha Mungu kwa kweli vipo—si tu uchoraji, havijafikiriwa, havijajengwa na binadamu, na bila shaka havijabuniwa na wao. Je, mnatambua hii sasa? Kama mnaitambua, basi maneno Yangu leo yametimiza shabaha yao.

Tulizungumzia mada tatu leo. Nina imani kila mmoja amepata pakubwa kutoka kwenye ushirika huu kuhusu mada hizi tatu. Ninaweza kusema kwa hakika kwamba, kupitia kwa mada hizi tatu, fikira za Mungu Nilizofafanua au kiini cha Mungu na tabia Nilizotaja vyote vimeweza kugeuza fikira na uelewa wa watu kuhusu Mungu, na hata kupindua imani za kila mmoja kwa Mungu, na zaidi, kupindua picha ya Mungu inayopendwa na kila mmoja katika mioyo yao. Haijalishi ni nini, Natumai kwamba kile mmejifunza kuhusu tabia ya Mungu katika sehemu hizi mbili za Biblia ni cha manufaa kwenu, na Natumai kwamba baada ya nyinyi kurudi mtajaribu kukitafakari zaidi. Kikao cha leo kinahitimishwa hapa. Kwaheri!


Novemba 4, 2013

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Tufuate: Neno la Mungu | "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II Uendelezo wa Sehemu ya Kwanza"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni