4.03.2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Tatu


       Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya Nuhu kukubali maagizo ya Mungu na kujenga safina na kuishi katika siku zile husika Mungu alitumia gharika ili kuangamiza ulimwengu, familia yake nzima ya wanane ilinusurika. Mbali na familia ya Nuhu ya wanane, wanadamu wote waliangamizwa, na viumbe wote nchini wakaangamizwa. Kwa Nuhu, Mungu alimpa baraka, na akasema baadhi ya mambo kwake na watoto wake wa kiume. Mambo haya yalikuwa yale ambayo Mungu alikuwa akimpa yeye na pia baraka zake kwake yeye. Hizi ndizo baraka na ahadi Mungu humpa yule ambaye anaweza kumsikiliza Yeye na kuyakubali maagizo Yake, na pia namna anavyotuza watu.

4.02.2019

Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

 Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu



(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria

Maneno Husika ya Mungu:

       Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. Waisraeli, ambao ni kizazi cha Nuhu na Adamu, ndio waliokuwa msingi wa kazi ya Yehova ulimwenguni.

4.01.2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)


Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe; Sifanyi ishara za ajabu na maajabu, lakini kila pahali hujaa kazi Zangu za ajabu. Njia iliyoko mbele itakuwa angavu mno. Ufunuo Wangu wa kila hatua ndio njia Ninayowaonyesha, mpango Wangu wa usimamizi. Hiyo ni kusema, baadaye ufunuo utakuwa mwingi zaidi na wazi zaidi. Hata katika Ufalme wa Milenia, katika siku zijazo zisizo mbali sana, ni lazima mwendelee kulingana na ufunuo Wangu na mwendo Wangu. 

3.31.2019

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu


1. Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu
Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake.  

3.30.2019

Neno la Mungu | "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" (Official Video)


Neno la Mungu | "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" (Official Video)


Mwenyezi Mungu anasema, "Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote.

3.29.2019

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

 Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. 

3.28.2019

Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Mungu huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni za kipekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
Na hakuna awezaye kubadili dhana au mawazo Yake,
au kumshawishi Ajaribu njia tofauti.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!

3.27.2019

Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

 Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu" (YN. 1:1-2).

"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).

"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu" (YN. 14:6).

"Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai" (YN. 6:63).

Maneno Husika ya Mungu:

Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

3.26.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile.

3.25.2019

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu" (EBR 9:28).

"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu" (YN. 1:1).

Maneno Husika ya Mungu:

Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. 

3.24.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”


Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”.

Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?


(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi.