8.19.2018

Tamko la Arubaini na Saba

Tamko la Arubaini na Saba

Ili kuwafanya wanadamu wawe wakomavu katika maisha na kuwafanya wanadamu na Mimi tuweze kutimiza matokeo katika udhanifu wetu wa pamoja, Nimewaendeka wanadamu kila mara, Nikiwakubalia kupata chakula na riziki kutoka kwa neno Langu na kupokea utele Wangu kutoka kwake.

8.18.2018

Sura ya 14

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ukweli, Mungu

       Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. 

Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa

Kwa kuwa Mungu alimwokoa mwanadamu, Atamwongoza;
kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa;
kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi.
Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu, kwa kuwa Anamsimamia mtu,
Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.

8.17.2018

Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"


Mungu Amekuja Mungu Ametawala | "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"


1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
2. Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi

1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho

Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.

8.16.2018

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili.

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

Umuhimu wa Mungu Kupata Mwili.

Maneno Husika ya Mungu:
Mwili huu ni muhimu sana kwa mwanadamu kwa sababu ni mwanadamu hata zaidi ni Mungu, kwa sababu Anaweza kufanya kazi ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya, na kwa sababu Anaweza kumwokoa mwanadamu aliyepotoka, ambaye anaishi pamoja na Yeye duniani. Ingawa Anafanana na mwanadamu, Mungu mwenye mwili ni wa muhimu sana kwa mwanadamu kuliko mtu yeyote wa thamani, kwa maana Anaweza kufanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na Roho wa Mungu, ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe, na ni mwenye uwezo zaidi kuliko Roho wa Mungu kuweza kumpata mwanadamu kabisa. Kwa sababu hii, ingawa mwili huu ni wa kawaida, mchango Wake kwa wanadamu na umuhimu Wake katika uwepo wa mwanadamu kunamfanya Awe wa thamani zaidi, na thamani halisi na umuhimu wa mwili huu hauwezi kupimwa na mwanadamu yeyote. Ingawa mwili huu hauwezi kumwangamiza Shetani moja kwa moja, Anaweza kutumia kazi Yake kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, na kumfanya Shetani kutii kikamilifu katika utawala Wake.

Sura ya 9


       Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. 

8.15.2018

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:


Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili.

Hebu Tuone ni Nani Anayemshuhudia Mungu Vema Zaidi

Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo

Hebu Tuone ni Nani Anayemshuhudia Mungu Vema Zaidi

Mwenyezi Mungu wa kweli, nakupenda. Naimba wimbo wa sifa,
nikicheza ngoma ya furaha na changamfu, kwa ajili Yako tu, Mwenyezi Mungu.
Tunaweza kukusifu Wewe kama leo—haya Mungu ameamua kabla.
Mungu wa kweli Ametushinda; sote tunakuja kumsifu Yeye.
Kila mtu njoo na mcheze, njoo muimbe wimbo wa furaha wa kusifu.
Ukiniuliza mimi mbona nacheza hivyo, moyo wangu unapenda, unampenda Mungu!

8.14.2018

Wimbo wa Kifuasi cha Dhati


Upendo wa Mungu Huushinda Moyo wa Mwanadamu | "Wimbo wa Kifuasi cha Dhati" (Video Rasmi ya Muziki) from Kanisa la Mwenyezi Mungu on Vimeo.
Wimbo wa Kifuasi cha Dhati
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.
Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli.
Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote.
Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana.
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili.

8.13.2018

Tamko la Arubaini na Sita

Tamko la Arubaini na Sita

Sijui jinsi watu wanavyoendelea katika kuyafanya maneno Yangu kuwa msingi wa kuweko kwao. Nimehisi wasiwasi kila mara kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu, lakini watu hawaonekani kuwa na fahamu yoyote kuhusu hili—na kutokana na hilo, hawajawahi kuyatilia maanani mambo Yangu, na hawajawahi kukuza kuabudu kokote kwa ajili ya mtazamo Wangu kuhusiana na mwanadamu.

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, sasa kwa sababu tuko na Wewe, masumbuko yanabadilika kuwa furaha.
Kula, kunywa, kufurahia maneno Yako, tuko na Wewe kila siku.
Maji Yako ya uzima yanatustawisha, tuna ukarimu kwa vyote.
Jua ukweli, ingia katika ukweli, yote yanakutegemea Wewe.
Ndugu, acha tule, tunywe maneno ya Mungu.

8.12.2018

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"


Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China" 



Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.