8.13.2018

Tamko la Arubaini na Sita

Tamko la Arubaini na Sita

Sijui jinsi watu wanavyoendelea katika kuyafanya maneno Yangu kuwa msingi wa kuweko kwao. Nimehisi wasiwasi kila mara kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu, lakini watu hawaonekani kuwa na fahamu yoyote kuhusu hili—na kutokana na hilo, hawajawahi kuyatilia maanani mambo Yangu, na hawajawahi kukuza kuabudu kokote kwa ajili ya mtazamo Wangu kuhusiana na mwanadamu.

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema

Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe

Mwenyezi Mungu, sasa kwa sababu tuko na Wewe, masumbuko yanabadilika kuwa furaha.
Kula, kunywa, kufurahia maneno Yako, tuko na Wewe kila siku.
Maji Yako ya uzima yanatustawisha, tuna ukarimu kwa vyote.
Jua ukweli, ingia katika ukweli, yote yanakutegemea Wewe.
Ndugu, acha tule, tunywe maneno ya Mungu.

8.12.2018

Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China"


Swahili Christian Movie Trailer | "Nyendo za Mateso ya Kidini Nchini China" 



Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani.

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. ...
Ikiwa hujui tabia ya Mungu, bila shaka utaanguka wakati wa majaribu, kwa kuwa hufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu kuwa wakamilifu, na ni kwa njia gani Huwafanya wakamilifu, na majaribu ya Mungu yakikushukia na yasilingane na mawazo yako, utashindwa kusimama imara.

8.11.2018

Kiini na Tabia ya Mungu Daima Vimekuwa Wazi kwa Binadamu

Kiini na Tabia ya Mungu Daima Vimekuwa Wazi kwa Binadamu

Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu, Amekuwa akifichua kwao
Kiini Chake na kile Alicho na Alicho nacho, bila kukoma, kila wakati.
Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,
Mungu huzungumza na kufanya kazi ili kuonyesha tabia Yake na kiini.
Havijawahi kufunikwa kamwe, havijawahi kufichika kamwe, vimeachiliwa bila kusita,
Kiini na tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki yake,
vinafichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu.

8.10.2018

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Tisa

Inaonekana kwamba katika mawazo ya watu, Mungu ni wa fahari sana naye Haeleweki. Ni kana kwamba Mungu haishi miongoni mwa wanadamu, kana kwamba anawadharau watu kwa sababu Yeye ni wa fahari sana. Mungu, hata hivyo, Huziseta fikira za wanadamu na kuzifuta zote, Akizika fikira zao zote ndani ya "makaburi" ambamo zinageuka kuwa majivu. Mtazamo wa Mungu kwa fikira za wanadamu ni sawa na mtazamo Wake kwa wafu, Akiwafafanua apendavyo.

8.09.2018

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?

Latest Swahili Gospel Film "Kubisha Hodi Mlangoni" | Je, Umesikia Sauti ya Mungu?


Utambulisho

      Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alitabiri, "Na usiku wa manane pakawa na kelele, Tazama, bwana harusi anakuja; tokeni nje mwende kumlaki" (Mathayo 25:6). "Tazama, nasimama mlangoni, na kubisha: mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja na yeye, na yeye pamoja na mimi" (Ufunuo 3:20).

8.08.2018

Ee Mwenyezi Mungu, Mpendwa Wangu Mzuri

Ee Mwenyezi Mungu, Mpendwa Wangu Mzuri

Mwenyezi Mungu, mpendwa wangu mzuri, Una moyo wangu.
Unapitia magumu, Unavumilia aibu, yote kwa ajili ya kutuokoa.
Unatoa maisha Yako kwangu, naona jinsi Ulivyo mzuri.
Unakuja duniani kutoka mbinguni, ukiwa mwenye mwili.
Uko hapa Ukiishi na sisi, lakini hakuna anayejua Wewe ni nani.

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba

Kwa kweli, maneno yote kutoka katika kinywa cha Mungu ni mambo ambayo wanadamu hawayajui; yote ni lugha ambayo watu hawajasikia, kwa hiyo inaweza kusemwa hivi: Maneno ya Mungu yenyewe ni siri. Watu wengi kwa kutojua wanaamini kwamba ni mambo tu ambayo watu hawawezi kutimiza kimawazo, mambo ya mbinguni ambayo Mungu anawawezesha watu kuyajua sasa, au ukweli kuhusu kile Mungu anachofanya katika ulimwengu wa kiroho ni siri.

8.07.2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu.

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.

Sifu Mafanikio ya Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu. Mungu, ukweli

 Sifu Mafanikio ya Kazi ya Mungu

Kazi kuu ya Mungu inabadilika upesi sana, ni ngumu kuielewa, ya kusadikisha kwa mwanadamu.
Tazama pale ulipo, sio kama awali, kila kitu ni kizuri na kipya.
Kila kitu kinafufuliwa, vyote kufanyunywa upya, vyote kubadilishwa.
Watu wa Mungu msifuni Mungu, kwa furaha nyingi, nyimbo za sifa zipae mawinguni kuelekea Kwake.

8.06.2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda.

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Kushinda

Maneno Husika ya Mungu:
Wanadamu kwa ajili ya kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma dhibiti kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu.