7.30.2018

Tamko la Hamsini

Tamko la Hamsini

Mwenyezi Mungu alisema, Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe. Najua kwamba hakuna yeyote kati yenu yuko tayari kuweka jitihada yoyote na kugharimika muda wowote kuhusu hili, kwa hivyo hamuwezi kupata ujuzi wowote. Mnaharibu muda wenu wote katika kula, kunywa na kustarehe.

7.28.2018

Mungu Anapata Mwili ili Tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu

Mungu Anapata Mwili ili Tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu

I
Wakati wa kupata mwili huku kwa Mungu duniani,
Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu.
Kazi hii yote ina kusudi moja—kumshinda ibilisi Shetani.
Atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu,
pia kupitia kukufanya mkamilifu. 

7.27.2018

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa.

7.26.2018

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


    Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi.

7.25.2018

Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.

7.24.2018

Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo, Kanisa, Yesu, Roho Mtakatifu

 Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Tong Xin    Mkoa wa Fujian
Nilizaliwa vijijini. Nilitoka kwa nasaba ya wakulima wanyenyekevu na zaidi ya hayo familia yetu ilikuwa na watu wachache, kwa hiyo mara nyingi tulikuwa tunadhulumiwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 13, kulikuwa na mtoto aliyepigwa na mtu fulani kutoka nje ya kijiji chetu. Wanakijiji walimlaumu kwa uongo baba yangu kwa kuchochea hilo na wakasema walitaka kupekua nyumba yetu na kuchukua ngawira mali yetu, kuchukua nguruwe wetu na hata kumpiga baba yangu.

7.23.2018

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

7.22.2018

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu


Utambulisho

Kwamba Mungu amekuwa mwili
hutikisa ulimwengu wa kidini,
inavuruga utaratibu wa kidini,
na inakoroga roho za wale
wanaongoja kuonekana kwa Mungu.

Tamko la Kwanza

Tamko la Kwanza

Mwenyezi Mungu alisema, Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli.

7.21.2018

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

7.20.2018

Nilifurahia karamu kubwa

Umeme wa Mashariki, Mungu, Kristo, wokovu

Nilifurahia karamu kubwa

Xinwei    Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo.

7.19.2018

Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu”

Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu

Ukilibadilisha au kulikanganya neno la Mungu Mwenyewe, basi hiyo ni sawa na uasi wa Mungu, kukufuru dhidi Yake na usaliti. Hii ni sawa tu na malaika mkuu kusema:"Mungu, Unaweza kuumba mbingu na ardhi na vitu vyote na Unaweza kufanya miujiza, lakini pia mimi ninaweza. Unapanda juu kwenye kiti cha enzi, na hivyo hivyo mimi pia napanda. Unatawala mataifa yote, Ninatawala mataifa yote pia. Wewe ulimuumba mwanadamu ilhali mimi ninawatawala!" Je, hii si ya hali sawa? Wengine wana mtazamo fidhuli kuhusu mipangilio ya kazi kutoka juu.