Tamko la Hamsini
Mwenyezi Mungu alisema, Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe. Najua kwamba hakuna yeyote kati yenu yuko tayari kuweka jitihada yoyote na kugharimika muda wowote kuhusu hili, kwa hivyo hamuwezi kupata ujuzi wowote. Mnaharibu muda wenu wote katika kula, kunywa na kustarehe.