7.15.2018

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,siku za mwisho

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na inapita maarifa ya mwanadamu.

7.14.2018

24. Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

24. Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe.
Ni Yeye ndiye Anayeianzisha kazi Yake, na ni Yeye anayeikamilisha.
Ni Yeye anayeipanga kazi.
Ni yeye ndiye anayeisimamia, na zaidi kuifanikisha kazi hiyo.

7.13.2018

3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu.

3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:   
Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani.

7.12.2018

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo.

7.11.2018

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

Umeme wa Mashariki,Kristo,hukumu

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

1. Hakuna Ambaye Angeokolewa iwapo Mungu Angeangalia Tu Maonyesho ya Asili ya Watu
Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile.

7.10.2018

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili.

7.09.2018

38. Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Kristo

38. Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang'anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa "bwana ndiyo" sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa "bwana ndiyo."

Kazi na Kuingia (10)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Yesu, upendo wa Mungu

Kazi na Kuingia (10)

Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu.

7.08.2018

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”

1. Tangu watu waanze kukanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho.

20. Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

20. Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Qingxin    Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu.

7.07.2018

13. Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Umeme wa Mashariki,Mungu,Injili

13. Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Xiao Rui    Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa madhehebu ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza.

7.06.2018

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.
Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu.