5.23.2018

39. Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

39. Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Wu Xia    Mji wa Linyi , Mkoa wa Shandong
Baada ya kuikubali kazi hii na kula na kunywa neno la Mungu, ilikuwa dhahiri kwangu kwamba ni muhimu sana kwamba mimi nijifahamu. Kwa hiyo, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, nilihakikisha nimejithibitisha tena dhidi ya neno ambalo Mungu humfichua mwanadamu. Katika hali nyingi, niliweza kutambua kasoro zangu na upungufu. Nilihisi kwamba ningekuja kujifahamu kweli.

"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (2) - Namna ya Kumfahamu Mungu Mwenye Mwili



"Siri ya Utauwa: Mfuatano" (2) - Namna ya Kumfahamu Mungu Mwenye Mwili

    Katika siku za mwisho, Mungu amepata mwili kufanya kazi ili kumwokoa mwanadamu. Lakini kwa sababu hatufahamu ukweli wa kupata mwili, tunamchukulia Mungu mwenye mwili kuwa sawa na mwanadamu wa kawaida, hatuwezi kuitambua sauti ya Mungu na tunajua hata kidogo zaidi jinsi ya kumkaribisha Bwana—kufikia kiwango ambacho hata tunaweza kufuata ulimwengu wa dini na nguvu zinazotawala kumkana na kumshutumu Mungu—hali haiwi tofauti na wakati ambapo Mungu alipata mwili kama Bwana Yesu kufanya kazi Yake ya Enzi ya Neema.

Swahili Gospel Movie | “Jina la Mungu Limebadilika?!” (Clip 5/7)

Swahili Gospel Movie | “Jina la Mungu Limebadilika?!” Movie Clip: Ni Kukubali Jina Jipya la Mungu Ndiko Kuwa na Kasi Sawa na Nyayo za Mwanakondoo


    Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa dinimara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa Bwana Yesu alisulubishwa msalabani kwa ajili ya dhambi za kila mmoja na kuwa mwanadamu amekombolewa kutoka kwa dhambi. Wanahubiri kuwa, mtu anapomwacha Bwana Yesu na kuamini Mwenyezi Mungu, ni sawa na kumsaliti Bwana Yesu na kuasi imani. Je, hakika ukweli uko hivi?

5.22.2018

Gospel Movie Clip "Siri ya Utauwa" (6) - Haja ya Mungu Kuifanya Kazi Yake kwa Njia ya Kupata Mwili

Gospel Movie Clip "Siri ya Utauwa" (6) - Haja ya Mungu Kuifanya Kazi Yake kwa Njia ya Kupata Mwili


    Kwa nini inasemekana kwamba ni ya manufaa zaidi Mungu kupata mwili ili kuwaokoa wanadamu? Haja na umuhimu mkuu wa Mungu kupata mwili vinaweza kuonekana wapi? Mwenyezi Mungu asema, "Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana.
Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu. Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kushindana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu" (Neno Laonekana Katika Mwili).

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho

5.21.2018

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (3) - Umuhimu wa Jina la Mungu


    "Yehova" na "Yesu" yalikuwa ni majina ya Mungu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, na imetabiriwa katika Ufunuo kuwa Mungu atakuwa na jina jipya katika siku za mwisho. Ni kwa nini Mungu anaitwa kwa majina tofauti katika enzi mbalimbali? Majina haya mawili ya "Yehova" na "Yesu" yana umuhimu gani? Video hii fupi itakusaidia kukutatulia fumbo hili.

47. Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

47. Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Li Li     Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje?

5.20.2018

71. Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

71. Ambua Barakoa, na Uanze Maisha Upya

Chen Dan    Mkoa wa Hunan
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa sababu sikuweza kuzindua kazi ya injili katika eneo langu, familia ya Mungu ilimhamisha ndugu mmoja wa kiume kutoka eneo jingine ili kuchukua kazi yangu. Kabla ya haya sikuwa nimearifiwa, bali nilisikia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutoka kwa dada mmoja niliyekuwa mbia naye. Nilifadhaika sana.

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?

"Jina la Mungu Limebadilika?!" (2) - Je, ni Kweli kuwa Jina la Mungu Haliwezi Kubadilika?


    Wachungaji na wazee wa ulimwengu wa kidini mara nyingi huhubiri kwa waumini kuwa jina la Bwana Yesuhaliwezi kamwe kubadilika na kuwa ni kwa kutegemea tu jina la Bwana Yesu ndio tunaweza kuokolewa. Je, mtazamo wa aina hii unaambatana na kuweli? Yehova Mungu alisema, "kabla yangu hakukuwa na Mungu aliyeumbwa, wala hakutakuwa baada yangu.

5.19.2018

67. Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

67. Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Yixin    Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei
Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, "Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu." Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

Wimbo za Sifa ""Upendo wa Kweli wa Mungu"" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)"

Wimbo za Sifa ""Upendo wa Kweli wa Mungu"" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)"


Leo naja mbele ya Mungu tena,
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.

5.18.2018

Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana

Swahili Christian Video "Mtoto, Rudi Nyumbani" | Hakuna Wokovu Ila Kupitia Kwa Bwana  


     Li Xinguang ni mwanafunzi wa shule ya upili ya ngazi ya juu. Alikuwa mvulana mwenye busara na mwenye tabia nzuri tangu alipokuwa mdogo. Wazazi wake na walimu wake walimpenda sana. Alipokuwa akienda katika shule ya kati, alipumbazwa na michezo ya kompyuta ya mtandaoni. Angekosa kwenda darasani mara kwa mara ili aende kwenye chumba cha mtandao. Wazazi wake walifanya kila juhudi kumsaidia kuyaondoa mazoea yake ya michezo. Kwa bahati mbaya, uzoefu wa Li Xinguang ulizidi kuwa mbaya zaidi na zaidi.  

5.17.2018

Gospel Movie Clip "Siri ya Utauwa" (4) - Mungu Mwenye Mwili pekee Ndiye Anaweza Kufanya Kazi ya Hukumu Katika Siku za Mwisho

Gospel Movie Clip "Siri ya Utauwa" (4) - Mungu Mwenye Mwili pekee Ndiye Anaweza Kufanya Kazi ya Hukumu Katika Siku za Mwisho


    Umeme wa Mashariki unashuhudia kwamba Mungu amepata mwili katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu Mwenyewe. Lakini kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria ilifanywa kwa kumtumia Musa. Kwa hiyo kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho haiwezi kufanywa kwa namna hiyo hiyo, kwa kuwatumia watu?