5.19.2018

Wimbo za Sifa ""Upendo wa Kweli wa Mungu"" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)"

Wimbo za Sifa ""Upendo wa Kweli wa Mungu"" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)"


Leo naja mbele ya Mungu tena,
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.
Leo naja mbele ya Mungu tena,
moyo wangu una mengi ya kusema.
Ni maneno Yake mororo yanayoninyunyizia
na kunirutubisha ili nikue.
Ni maneno Yake makali yanayonitia moyo ili nisimame tena.
Ee Mungu! Tunaweza kukusifu kwa kuwa Umetuinua!
Tunaweza kukuimbia leo yote
kwa sababu ya baraka na neema Yako.

Ee Mungu, Unatupenda sana kweli!
Unatufanya tufurahie maneno Yako kila siku!
Ee Mungu, Unatupenda sana kweli! Unatupa nuru kila siku!
Ee Mungu, Unatupenda sana kweli!
Unawanyunyizia na kuwastawisha watu Wako.
Unatuepusha na ushawishi wa Shetani.
Ndugu, fanyeni upesi na muinuke! Tumsifu Mungu wetu!
Hebu tufurahie jinsi ambavyo Ametukusanya hapa leo.
Tuwe huru kabisa kutokana na mizigo ya mwili!
Sifa kwa Mwenyezi Mungu kwa bidii!
Tutimize wajibu wetu kwa moyo wetu wote na nguvu zote,
tuonyeshe upendo wetu kwa Mungu kwa matendo.
Tutakupenda milele, Mwenyezi Mungu wa Kweli!

kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya


Baadhi ya vifaa ni kutoka:

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni