5.21.2018

47. Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, Umeme wa Mashariki

47. Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji

Li Li     Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje? Matokeo yake yalikuwa, tulipozungumzia mada fulani pamoja, almradi nilikuwa na ufahamu kidogo wa mada hiyo, basi ningejaribu kuwa wa kwanza kusema kitu, hata hivyo wakati sikuwa na ufahamu wa mada iliyojadiliwa na sikuweza kusema chochote, nilijipata nikiwa na wasiwasi. Katika siku hizo chache za mikutano, nilihisi nimechoka sana na kuwa na wasiwasi hasa, kana kwamba nilikuwa katika uwanja fulani wa kupambana. Baadaye, nilitafakari juu ya kile nilichofichua na nilitambua kuwa hali ya aina hii ilikuwa ilisababishwa hasa na majisifu yangu na hakukuwa na matatizo halisi.
Halafu siku moja, viongozi waliniarifu juu ya mkutano, nilihisi msisimko hasa nilipoambiwa kwamba msimamizi angeitisha mkutano huo, na nikafikiri: Inaonekana kama nitafunzwa ili kupanda cheo, nikifanya vizuri na kuacha picha nzuri basi labda nitapandishwa cheo, na wakati uwajibikaji wangu unapoongezeka, basi sio wafanyakazi wenzangu tu watakaonipenda lakini pia ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kwa hiyo katika mkutano huo, nilizungumza kwa majaribio sana, kwa kuogopa kwamba maneno yoyote yasiyofaa yangeacha picha mbaya kwa viongozi wangu. Wakati mkutano ulipomalizika hatimaye, nilihisi furaha ingawa nilikuwa na wasiwasi na kuchoka siku zilizopita, na nilihisi kuwa wakati ujao ulikuwa na ahadi nyingi. Kuanzia hapo kuendelea, "ukimbizaji" wangu ulikuwa umeongezeka sana kwa nguvu.
Mpaka baadaye, aliyetajwa hapo juu alitoa mahubiri "Kuelewa Kiini Chetu Kipotovu Kabla Tuwe na Uwezo wa Kuingia kwa Njia Sahihi ya Imani katika Mungu," ambamo niliona kuna haya ya kusema: "Zamani watu walilenga tu makosa yao ya awali milele, au upotovu upi waliokuwa wamefichua,huku wakitelekeza kuchangua kila neno na tendo lao: ambalo linamilikiwa na upotovu wa Shetani, ambalo linamilikiwa na sumu ya joka kubwa jekundu, ambalo linamilikiwa na eneo la mawazo na dhana za watu, na ambalo linamilikiwa na mikengeuko au dhana. Na mtu lazima pia achangue hali yake ya akili na nafsi ya ndani, akamate mambo yaliyofichika katika uketo wa moyo, na aje mbele ya Mungu na kutumia ukweli kuyachunguza, ili ajue upotovu wake wenyewe, na kuona tatizo halisi la upotovu. Kwamba hakuna kuonekana kwa makosa makuu hakumaanishi kuwa hakuna tatizo ndani ya nafsi. Ni uovu uliofichika, tabia, na asili ambayo ni ngumu zaidi kutatua. Watu huwa hawafariki kutokana na kuvuta kamasi, ni magonjwa makubwa ambayo hufisha." Baada ya kusoma hili, sikuweza kujizuia kufikiria saikolojia yangu mwenyewe kutoka mikutano miwili iliyopita, na kwa ndani nilifikiria: Ni asili gani iliyoitawala? Wakati huo, nilianza kutafuta ukweli uliotangamana kwa hali yangu mwenyewe ili nipate kuichunguza na kuichangua.
Chini ya mwongozo wa Mungu, niliona neno la Mungu: “…watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja na kuongea; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, kuwazingira. Wanapenda kuwa na kimo katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Je, tunagundua nini kuhusu asili ya mtu kutokana na aina hii ya mwenendo? Hebu tuchanganue asili yake: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia kama hii ana asili ya aina gani? Je, ingewezaje kusemwa kwa ufupi? Watu wa kawaida hawawezi kuelewa hili lakini wanaweza tu kuona mwenendo. Uhusiano kati ya tabia na asili ya mtu ni upi? Je, asili yake ni gani? Huwezi kuitambua, sivyo? Kama kweli anatennda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni mfidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwambudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, kuwa na kimo akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Je, hii si asili yake? Unaweza kuelewa wazi asili yake kutoka kwa mienendo hii” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilijaribu tena na tena kulielewa kila neno la Mungu, na kuyalinganisha na mawazo yangu mwenyewe, maneno na matendo, ni hapo tu nilipoona ukweli. Sababu yangu hasa ya kuwa na wasiwasi na wa kupaswa kutii mamlaka ya kuongoza kwa mkutano haikuwa ni kuwaacha watu wengine wanisikilize au kunitilia thamani? Si ilikuwa tu ni kupata hadhi ya juu na kuwa na watu zaidi kuniheshimu sana? Nilipohisi kwamba viongozi waliniheshimu, nilifikiri kwamba maisha yangu ya baadaye yalijaa matumaini, na nilijihisi kuridhika nafsi zaidi na mwenye nguvu. Kutoka kwa hilo niliona hali ya kiburi changu mwenyewe, daima nilitaka kupanda ngazi, kuwatawala watu, kuwa na nafasi katika mioyo ya watu, nilitafuta sawa na Paulo aliyotafuta. Kimsingi, kile nilichofuatilia hakikuwa kumwabudu au kumridhisha Mungu, bali kutumia hadhi iliyotolewa na Mungu ili kuridhisha tamaa na malengo yangu mwenyewe. Si hivi ndivyo hasa jinsi malaika mkuu alivyoonyesha kiburi chake? Si nilishika njia ya mpinga Kristo?
Awali nilipohudhuria mikutano nilikuwa nikizuiwa kwa urahisi, lakini nilifikiri tu kwamba nilikuwa ovyo mno, na sikuvichangua vitu vilivyokuwa nyuma. Sasa baada ya uchambuzi nilitambua kwamba hili lilikuwa linaendeshwa na asili ya kiburi na ya majivuno, ambamo nyuma yake kulikuwa mipango ya kibinafsi na malengo ya kiburi. Nilitawaliwa na kiburi changu mwenyewe, na nilifanya mengi dhidi ya Mungu: Niliharakisha nikitekeleza wajibu wangu na nilikuwa na hamu ya kujionyesha mwenyewe ili kupata hadhi ya juu na kupata upendezwaji wa ndugu zangu wa kiume na wa kike; nilipojiweka wazi mbele ya ndugu wa kiume na wa kike, kwa kweli sikuwahi kamwe kuchambua mambo yaliyofichika ndani kwa kina, badala yake nilizungumza juu ya vitendo vyangu vya nje ili kujipandisha cheo na kujishuhudia mwenyewe; nilipokula na kunywa neno la Mungu, haikuwa kuinua ufahamu wangu au kupokea ukweli, bali kujionyesha kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike. … Wakati nilifikiria jambo hili nilijikunyata: Sikuwa nikimtumikia Mungu, nilikuwa nimejihusisha kabisa na mambo yangu mwenyewe na kumpinga Mungu. Sasa, kama Mungu hakuwa ameniruhusu kuitambua asili yangu ya kiburi, na kujiona kama mfano halisi wa Shetani, basi ningeendelea na njia zangu za kiburi, na huenda nikafanya mambo maovu ambayo humpinga na kumsaliti Mungu na hivyo kuwa na uelekeo wa adhabu ya Mungu.
Ninamshukuru Mungu kwa kunipatia nuru Kwake kwa wakati wa kufaa na mwongozo ambao uliniongoza kutambua kiini cha asili yangu ya kiburi, na kuniruhusu nione kwamba nilikuwa ninashika njia ya mpinga Kristo; uzoefu huu umenifanya hasa kutambua kwamba, katika uzoefu wangu sipaswi kutambua ufunuo wangu mwenyewe na makosa tu lakini kuyalinganisha na ukweli na kuchunguza mambo yaliyofichika ndani sana ili kupata ufahamu bora wa asili yangu mwenyewe na kufanya mabadiliko katika tabia yangu. Katika siku zijazo, ningependa kuchangua kwa makini hali yangu ya akili na hali ya ndani, na kuielewa asili yangu potovu, kutafuta na kupata njia sahihi kwa wokovu wa Mungu.
 Utukufu wote Uwe kwa Mwenyezi Mungu!
kut Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni