12.30.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Sita


Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Sita
Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. 

12.29.2017

Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

1. Yohana alianza kueneza injili ya ufalme wa mbinguni miaka saba kabla ya ubatizo wa Yesu. Kwa watu, kazi aliyoifanya ilionekana kuwa juu zaidi ya kazi ya baadaye ya Yesu, ilhali yeye alikuwa, hata hivyo, nabii tu. Hakufanya kazi au kuzungumza ndani ya hekalu, lakini katika miji na vijiji nje yake. Hii alifanya, bila shaka, miongoni mwa taifa la Wayahudi, hasa wale waliokuwa maskini.

12.28.2017

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho


Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho


> Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.

12.27.2017

Kwaya za Injili " Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18"



Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 18

Kwaya za Injili :
1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
2. Mwenyezi Mungu Amekuwa Ameketi Kwenye Kiti Kitukufu cha Enzi

1. Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho

Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho.

12.26.2017

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song



Mungu ni upendo | “Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song


Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu

Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki

vinakua ulimwenguni kote,

ikitukuka sana kati ya wanadamu wote. more

Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.

Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?

Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;

jua linaaangaza kotekote.

wakiishi katika mwanga wa Mungu,

wakiwa na amani na kila mmoja.

12.25.2017

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu|Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu
Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu|Umeme wa Mashariki

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu|Umeme wa Mashariki


Mwenyezi Mungu alisema, Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita.

12.24.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Dibaji

Dibaji | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu.

12.20.2017

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )



Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani" ( Filamu za Injili )


      Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba "Biblia ni ufunuo wa Mungu," "Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu." Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Hadi siku moja, alipowazuia waumini kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu mtandaoni, akawa na fursa ya kukutana na wahubiri kutoka katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia majadiliano makali kuhusu ukweli, aliweza hatimaye kuona wazi uhusiano kati ya Biblia na Mungu? Je, aliweza kusonga mbali na Biblia kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima? Je, atachukuliwa kwenda mbinguni mbele ya Mungu?


      Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

12.18.2017

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Je, Kazi na Maneno Yote ya Mungu Yamo katika Biblia?



     Dunia nzima ya kidini yote huamini kwamba kazi na maneno ya Mungu yote yamo katika Biblia, na kwamba isipokuwa Biblia, hakuna maneno yaliyonenwa na Mungu na kazi Yake. Kwa hiyo, ili mradi uko mwaminifu kwa Biblia, hili litahakikisha kwamba utaweza kuingia ufalme wa mbinguni. Je, mawazo haya yanapatana na ukweli wa kazi ya Mungu? Kuna maneno ya Mungu nje ya Biblia? Ni nini hasa kitakachomwongoza mwanadamu kuingia ufalme wa mbinguni? Je, ni kushika Biblia, ama ni kufuata nyayo za Mwanakondoo? Dondoo hii itafichua majibu yote kwako!

12.17.2017

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Ni nini uhusiano kati ya Mungu na Biblia?



Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Ni nini uhusiano kati ya Mungu na Biblia?


      Kwa miaka elfu mbili, tumemwamini Bwana kulingana na Biblia, na wengi wetu sana huamini "Biblia inamwakilisha Bwana, kumwamini Mungu ni kuamini Biblia, kuamini Biblia ni kumwamini Mungu," Je, mawazo haya ni sahihi?

12.16.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Masharik
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Mwenyezi Mungu alisema, Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa. Ni wazi kutokana na hili kwamba watu hawamfahamu Mungu, na hata ingawa wanasema wanaamini katika Yeye, kuhusu kiini chake, kulingana na matendo yao wanaamini katika wao wenyewe, sio Mungu.

12.15.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4)


Mwenyezi Mungu alisema, Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake?

12.12.2017

Unapaswa Kudumisha Ibada Yako Kwa Mungu

Unapaswa Kudumisha Ibada Yako Kwa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Roho Mtakatifu Anafanya kazi vipi katika kanisa sasa? Je, una ufahamu wa hilo? Ni matatizo gani makubwa zaidi yanayowakumba ndugu na dada? Wamepungukiwa na nini zaidi? Kwa sasa, kuna watu ambao wako hasi katikati ya majaribio, na wengine wao hata wanalalamika, na wengine hawasongi mbele tena kwa sababu Mungu Hazungumzi tena. Watu hawajaingia njia sahihi ya imani katika Mungu. Hawawezi kuishi wakijitegemea, na hawezi kudumisha maisha yao ya kiroho.

12.11.2017

Upendo wa Mungu Unaenea Duniani Kote

 Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Upendo wa Mungu Unaenea Duniani Kote

Mwenyezi Mungu, Wewe ni mwenye haki, Wewe ni mtakatifu.
Upendo Wako safi ni kama chembe ya theluji ikicheza hewani,
nyeupe, nzuri, inayonukia, ikiniangukia, ikiyeyuka katika upendo wangu mara moja.
Kupitia uboreshaji Wako upendo wangu Kwako umekuwa halisi kabisa.
Nikuache upange njia ya maisha yangu Wewe binafsi.

12.10.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 3. Baada ya Kupoteza Hadhi Yangu …


Kila wakati nilipoona au kusikia kuhusu mtu aliyekuwa amebadilishwa naye kujisikia mwenye huzuni, dhaifu au mnunaji, na kutotaka kufuata tena, basi niliwaangalia kwa dharau. Nilidhani haikuwa kitu zaidi ya watu tofauti waliokuwa na majukumu tofauti ndani ya kanisa, kwamba hakukuwa na tofauti kati ya juu au chini, kwamba sote tulikuwa uumbaji wa Mungu na hakukuwa na sababu ya kuhuzunikia.

12.08.2017

Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari



     Mwenyezi Mungu alisema:Watu wote wamepitia usafishaji kwa sababu ya maneno ya Mungu. Kama sio Mungu mwenye mwili wanadamu bila shaka hawangebarikiwa kuteseka hivyo. Inaweza pia kusemwa hivi—wale wanaoweza kukubali majaribio ya maneno ya Mungu ni watu waliobarikiwa. Kulingana na ubora wa akili wa watu wa asili, mwenendo wao, mitazamo yao kwa Mungu, hawastahili kupokea aina hii ya usafishaji. Ni kwa sababu wameinuliwa na Mungu ndio wamefurahia baraka hii.

12.05.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi-Mungu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Umeme-wa-Mashariki
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. 

12.04.2017

Sura ya 19. Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,upendo wa Mungu
upendo wa Mungu

Sura ya 19. Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu anapata mwili ili ateseke kwa niaba ya mwanadamu, na kwa kufanya hivyo atasababisha hatima iliyo ya ajabu ambayo itafuata kwa ajili ya mwanadamu. Hatua hiyo ya kazi iliyokamilishwa na Yesu ilikuwa tu kuwa Kwake mfano wa mwili wenye dhambi na kusulubiwa, kuhudumu Kwake kama sadaka ya dhambi na kuwakomboa wanadamu wote, na hii iliweka msingi wa kuingia kwa baadaye kwa mwanadamu katika hatima iliyo ya ajabu.

12.03.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 17. Ufahamu wa Kupata Mwili

Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Umeme-wa-Mashariki

Mwenyezi Mungu alisema: Kumjua Mungu kunapaswa kufanywa kupitia kwa kusoma neno la Mungu na kulielewa neno la Mungu. Watu wengine husema: "Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo nitawezaje kumjua Mungu?" Neno la Mungu kwa kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu. Kutoka kwa neno la Mungu unaweza kuuona upendo wa Mungu kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na jinsi Anavyowaokoa ... kwa sababu neno la Mungu linaonyeshwa na Mungu ikilinganishwa na Mungu kumtumia mwanadamu kuliandika. Linaonyeshwa na Mungu binafsi. Ni Mungu Mwenyewe Akielezea maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini tunayaita maneno ya dhati?

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Mwenyezi-Mungu, Kanisa -La-Mwenyezi Mungu, Umeme-wa-Mashariki
  
Mwenyezi Mungu alisema: Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi.

12.01.2017

Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani


Mwenyezi Mungu alisema: Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli.