4.30.2019

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Kwanza



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Kwanza
     Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

4.29.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Pili




Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Pili


       Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingeweza kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo.

4.28.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote III Sehemu ya Tatu




Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) Sehemu ya Tatu

Mungu anaweka Uwiano Kati ya Vitu Vyote ili Kumpatia Binadamu Mazingira Imara kwa ajili ya Kuendelea Kuishi
       Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Tumemaliza kusema juu ya jinsi ambavyo Mungu anatawala sheria za vitu vyote vilevile jinsi ambavyo Anawakimu na kuwalea binadamu wote ndani ya sheria hizo. Hiki ni kipengele kimoja. Kinachofuata, tutazungumza juu ya kipengele kingine, ambacho ni njia moja ambayo Mungu ana udhibiti wa kila kitu. Hivi ndivyo, baada ya kuumba vitu vyote, Akaweka uwiano wa uhusiano kati yao.

4.27.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Kwanza



         Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Kwanza


Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde.

4.26.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Pili



Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Pili

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho



1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

       Kwa roho yoyote, kupata kwake mwili mpya na nafasi anayochukua—nafasi yake ni ipi katika haya maisha—atazaliwa katika familia gani, na maisha yake yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yake ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanakuja kulipa deni.

4.25.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Tatu


     

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Tatu
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho


3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu

Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache.

4.24.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote IV Sehemu ya Nne




Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Nne
Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu
1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe

Tumefikia mwisho wa mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," vilevile na ile ya "Mungu ni wa kipekee Mungu Mwenyewe." Baada ya kufanya hivyo, tunahitaji kufanya muhtasari. Muhtasari wa aina gani? Unaomhusu Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa ni kumhusu Mungu Mwenyewe, basi lazima ugusie kila kipengele cha Mungu, vilevile aina ya imani ya watu kwa Mungu. Na kwa hiyo, kwanza lazima Niwaulize: Baada ya kusikia mahubiri, Mungu ni nani katika jicho la mawazo yako? (Muumbaji). Mungu katika jicho la mawazo yako ndiye Muumbaji. Kuna kitu kingine chochote? Mungu ni Bwana wa vitu vyote.

4.23.2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza


Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

4.22.2019

Neno la Mungu | Sura ya 21


Machoni pa Mungu, watu ni kama wanyama katika ulimwengu wa wanyama. Wao hupigana, huchinjana, na huwa na ushirikiano wa pekee mmoja kwa mwingine. Machoni pa Mungu, wao pia ni kama sokwe, wakipangiana hila bila kujali umri au jinsia. Kwa hivyo, yote ambayo wanadamu wote hufanya na kuonyesha hayajawahi kuupendeza moyo wa Mungu. Wakati ambao Mungu hufunika uso Wake ndio hasa wakati ambao watu duniani kote wanajaribiwa. Watu wote wanapiga kite kwa uchungu, wote wanaishi chini ya tishio la msiba, na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuepuka kutoka kwa hukumu ya Mungu. 

4.21.2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Tatu


Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Tatu


Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa sababu Mungu hana upotovu wowote wa mwanadamu na hana chochote sawa na, au kinachofanana na tabia potovu ya mwanadamu ama kiini cha Shetani, kutoka mtazamo huu tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu hafichui upotovu wowote, na ufunuo wa kiini Chake katika kazi Yake yote ni thibitisho tunalohitaji kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu.

4.20.2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu


   Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure. Katikati ya maumivu yake na kutokuwa na tumaini, ni maneno ya Munguyaliyomwokoa, yakimsaidia kupata kiini cha maumivu yake, kuelewa maana ya maisha, na hatua kwa hatua kutoka kwenye fadhaa ya mateso yake.

4.19.2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Nne


1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake

Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbo yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi. Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni.