10.12.2019

Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina.

10.11.2019

Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa





Maneno Husika ya Mungu:
Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme.

10.10.2019

Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tu kwamba ikiwa unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu akisema ni vizuri na kukupa hongera inahesabika kama kuelewa, neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza mapenzi ya Mungu ni yapi ndani ya maneno hayo na yatafanikisha nini hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa.

10.09.2019

Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Maneno Husika ya Mungu:
Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake.

10.08.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?

Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu.

10.07.2019

Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kutimiza wajibu wako ni ukweli. Kutimiza wajibu wako katika nyumba ya Mungu sio tu kutimiza masharti fulani au kufanya kitu unachopaswa kufanya. Ni kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa anayeishi kati ya mbingu na dunia! Ni kutimiza majukumu na wajibu wako mbele ya Bwana wa uumbaji. Majukumu haya ni majukumu yako ya kweli. Linganisha kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa na kuwa na upendo kwa wazazi wako—ni kipi ndicho ukweli? Kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa ndio ukweli; ni wajibu wako unaotarajiwa kutimiza.

10.06.2019

Mtu anafaaje kutenda kuingia kuwa mtu mwaminifu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi
Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole.
kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu.

10.05.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtu mwaminifu na mtu mdanganyifu?

Maneno Husika ya Mungu:

Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu. Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.

10.04.2019

Mtu mdanganyifu ni nani? Kwa nini watu wadanganyifu hawawezi kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:
Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.

10.03.2019

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.

10.02.2019

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu.

10.01.2019

Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi


Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema.