Maneno Husika ya Mungu:
Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.
kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wakijifanya kuwa watu wasio wakati wako mbele ya wengine, wakitoa muonekano wa unyenyekevu, uvumilivu na upendo, lakini katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila na hawana uaminifu kwa Mungu, watu kama hao ni mfano wa kuigwa wa kawaida wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, wao ni kizazi cha nyoka.
kutoka katika “Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unajitwika sura ya bandia ili wengine waone na wewe kwa upole unajifanya kujidai; hili hufanyika ili ujikinge mwenyewe. Wewe hufanya hilli ili kuyaficha maovu yako, na hata kutafuta njia za kuusukuma huo uovu kwa mtu mwingine. Ni hila gani hukaa ndani ya moyo wako!
kutoka katika “Sura ya 13” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Baadaye, katika njia iliyo mbele, hampaswi kusababisha ulaghai au kushiriki katika udanganyifu na upotovu, vinginevyo matokeo yatakuwa yasiyofikirika! Bado hamwelewi udanganyifu na upotovu ni nini. Matendo yoyote au tabia ambazo hamwezi kuniruhusu Nione, ambazo hamwezi kuziweka hadharani ni udanganyifu na upotovu. Sasa mnapaswa kuelewa hili! Mkishiriki katika udanganyifu na upotovu katika siku zijazo, msijifanye kuwa hamwelewi, huko ni kufanya tu makosa kwa makusudi, kuwa na hatia hata zaidi. Hii itawasababisha tu kuteketezwa na moto, au hata mambo yakiwa mabaya zaidi, kujiangamiza.
kutoka katika “Sura ya 45” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine kila mara hupeperusha bendera ya kanisa haijalishi wanachofanya; kweli ni kwamba hii ni kwa manufaa yao. Mtu wa aina hiyo hana aina nzuri ya nia. Yeye ni mhalifu na mdanganyifu na mambo mengi sana anayofanya ni ya kutafuta manufaa yake mwenyewe. Mtu wa aina hiyo hafuatilii kumpenda Mungu; moyo wake bado ni wa Shetani na hauwezi kumgeukia Mungu. Mungu hana njia ya kumpata mtu wa aina hiyo.
kutoka katika “Upendo Halisi kwa Mungu ni wa Hiari” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake. … Unafaa kujua kama kunayo imani ya kweli na uaminifu wa kweli ndani yako, kama una rekodi ya kuteseka kwa ajili ya Mungu, na kama umemtii Mungu kikamilifu. Kama unakosa hivi Nilivyotaja, basi ndani yako kunabaki kutotii, udanganyifu, ulafi, na kutotosheka. Kwa vile moyo wako si mwaminifu, hujawahi kupokea utambuzi mzuri kutoka kwa Mungu na hujawahi kuishi katika mwangaza. Kile ambacho jaala ya mtu kitakuwa hutegemea kama anao moyo wa uaminifu na wa kweli, na kama anayo nafsi isiyo na doa. Kama wewe ni mtu asiye mwaminifu sana, mtu mwenye moyo wa kijicho na nafsi isiyo safi, basi rekodi ya majaliwa yako bila shaka ipo pale ambapo binadamu huadhibiwa. Kama unadai kwamba wewe ni mwaminifu sana, na bado kamwe hutendi kulingana na ukweli au kuongea neno la ukweli, basi bado unatarajia Mungu kukutuza? Bado unatumai Mungu akuchukue kama kipenzi Chake? Je, kufikiria huku si kwa upuzi? Unamdanganya Mungu katika mambo yote, hivyo nyumba ya Bwana inawezaje kumpa nafasi mtu kama wewe, ambaye mikono yake si safi?
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili
“Iwapo hutaki kabisa kuwaambia wengine siri zako—yaani, ugumu wako—ili kutafuta njia ya mwanga basi Nasema wewe ni mtu ambaye ni mgumu kuokoa, mtu ambaye hawezi kuibuka kutoka kwa giza kwa urahisi.” Hapa Mungu amewapa wanadamu njia ya kutenda, na ikiwa hutendi kwa njia hii, na unasema tu wito na mafundisho kwa sauti, basi wewe ni mtu ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi. Hili kweli linahusiana na wokovu. Kuokolewa ni muhimu sana kwa kila mtu. Je, Mungu ametaja hili mahali pengine popote? Mahali pengine, anataja kwa nadra ugumu wa kuokolewa, lakini Analizungumzia wakati Anaongea kuhusu kuwa mwaminifu: Usipotenda kwa njia hii, basi wewe ni mtu ambaye ni mgumu sana kuokoa “Kutopokea wokovu kwa urahisi” kunamaanisha ni vigumu kwa wewe kuokolewa na huna uwezo wa kuchukua njia sahihi ya wokovu, na hivyo haiwezekani kukuokoa. Mungu husema hili ili kuwapa watu uhuru kiasi wa kutenda tofauti; yaani, wewe si rahisi kuokoa, lakini kwa upande mwingine, ukiweka maneno ya Mungu katika vitendo, kutakuwa na matumaini kwako na unaweza kuokolewa. Usipoweka maneno ya Mungu katika vitendo, na iwapo kamwe huchambui siri ama ugumu wako mwenyewe, ama kamwe humwambii yeyote haya mambo binafsi ama kuwaambia watu kuyahusu, kamwe kuwasiliana na watu kuyahusu, ama kuyachambua na watu ili kujiweka wazi, basi hakuna uwezekano wa wewe kuokolewa. Na mbona hivyo? Iwapo hujiweki wazi ama kujichambua kwa njia hii, tabia yako potovu haitabadilika kamwe. Na iwapo huwezi kubadilika, unaweza kusahau kuhusu kuokolewa. Hivi ndivyo Mungu anavyomaanisha anaposema maneno haya na haya ni mapenzi ya Mungu.
Kwa nini daima Mungu amesisitiza kwamba watu wanapaswa kuwa waaminifu? Kwa sababu ni muhimu sana na kunahusiana moja kwa moja na iwapo unaweza kuokolewa au la. … Mungu anataka watu ambao ni waaminifu. Iwapo wewe si safi—iwapo wewe ni mdanganyifu, mdanganyifu, na mwenye kudhuru kwa siri—basi wewe si mtu mwaminifu, na iwapo wewe si mtu mwaminifu, hakuna uwezekano kwamba Mungu atakuokoa, na haiwezekani wewe kuokolewa.
kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee.
kutoka katika “Sura ya 96” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu hawakamilishi wale walio wadanganyifu. Ikiwa moyo wako si mwaminifu, ikiwa wewe si mtu mwaminifu, basi Mungu hatakupata kamwe. Wewe, pia, hutapata ukweli kamwe, na hutakuwa na uwezo wa kumpata Mungu. Kama huwezi kumpata Mungu, na huelewi ukweli, basi inamaanisha kwamba wewe ni wa uhasama kwa Mungu, hulingani na Mungu, na Yeye si Mungu wako. Na kama Mungu sio Mungu wako, huwezi kupata wokovu. Kama huwezi kupata wokovu, wewe utakuwa adui mkubwa wa Mungu milele, na matokeo yako yameamuliwa.
kutoka katika “Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Watu wadanganyifu hawawadanganyi wengine tu, lakini pia wanamtendea Mungu kwa udanganyifu kwa sababu hiyo ndiyo asili yao. Tunaweza kuona asili yao kutoka kwa mtazamo ambao watu wadanganyifu wanashikilia kwa neno la Mungu: Daima wanahodhi tashwishi kuhusu neno la Mungu, na hawaliamini. Kuhusu hoja hii, watu wadanganyifu na watu waaminifu ni tofauti kabisa. Watu waaminifu hasa hawana hila. Wanaamini chochote anachosema Mungu, wanatii chochote anachosema Mungu, na wanafanya jinsi Mungu anavyohitaji kabisa. Kwa hiyo Mungu huwapenda watu waaminifu na huwabariki watu waaminifu; ni rahisi zaidi kwa watu waaminifu kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Mtu mdanganyifu ni kinyume kabisa. Bila kujali kile anachokisema Mungu, mtu mdanganyifu daima ana shaka kwamba ni hila, kwamba ni hekima, kwa hiyo hawezi kukikubali na kukitenda kwa urahisi. Watu wadanganyifu hawana tu tashwishi kuhusu neno la Mungu, lakini pia ni hodari katika kuchunguza kazi ya Mungu. Daima wao hujaribu kukisia nia za kweli za Mungu ili waweze kufanya maafikiano. Ni dhahiri, watu wadanganyifu ni wastadi zaidi katika kubadilishana. Falsafa yao ni falsafa ya kubadilishana, falsafa ya kutokubali hasara. Hata wamejaribu kufanya maafikiano na Mungu kuhusu imani yao. Daima wanatafakari juu ya iwapo watabarikiwa au kulaaniwa katika imani yao, na ni wenye wasiwasi zaidi kuhusu iwapo wao ni watu wa Mungu au watendaji huduma. Daima wanakusudia, na siku yoyote ambayo hawawezi kupata uwazi kuhusu suala hili ni siku ambayo hawatatulia kutafuta uzima. Watu wadanganyifu ni wajanja, na ndio watu wajanja zaidi ya wote. Kwa sababu hii, Mungu huwachukia watu wadanganyifu zaidi, na Hataki kutumia juhudi zaidi kwao au kuwazungumzia tena. Watu wadanganyifu daima wanatafuta makosa madogomadogo katika mtazamo wao kwa maneno ya Mungu; wanachunguza maneno Yake wakitafuta makosa ya mantiki na sababu za mabishano. Kwa sababu watu wadanganyifu wanachukulia maneno ya Mungu kwa mwelekeo wa shaka, uasi, upinzani, na kutoamini, wanakosa kazi ya Roho Mtakatifu kabisa. Hawapati hata chembe ya nuru wanaposoma maneno Yake, wakionekana wapuuzi na ovyo sana. Kwa kweli, hakuna ukinzani hata kidogo katika maneno ya Mungu, lakini wanatafuta kupata pahali pengi pa ukinzani na kujipata taabani. Hili hasa linaonyesha hali yao ya kusikitisha ya kukosa nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu na ufahamu wa kiroho. Kutoka kwa mwelekeo ambao watu wadanganyifu hutumia kuchukulia neno la Mungu, tunaweza kuona kwamba asili yao bila shaka ni asili ya kishetani inayompinga Mungu. Wale wote wanaochukulia neno la Mungu kwa mwelekeo wa tashwishi na kutoamini kimsingi ni watu wadanganyifu ambao bila shaka hawatapata ukweli kutoka kwa maneno ya Mungu, na wataishia kuondolewa tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni