10.06.2019

Mtu anafaaje kutenda kuingia kuwa mtu mwaminifu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi
Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole.
kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako.
kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye.
kutoka katika “Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kikwazo kikubwa zaidi kwa kuwa mwaminifu ni kudhuru kwa siri kwa watu, udanganyifu wao, uovu wao, na nia zao za aibu. Je, mshawahi kujifunza kuwa waaminifu? Na hali yenu wakati mlikuwa mkijifunza ilikuwa ipi? … Kwa mfano, ulimfanyia mtu kitu, ulimdanganya, ama ulisema maneno ambayo yalikuwa na madoa ama ambayo nia zako mwenyewe, na hivyo unapaswa kuenda na kumtafuta mtu huyo na kujichambua na kusema: “Maneno niliyoyasema wakati huo yalikuwa na nia zangu binafsi. Iwapo unaweza kukubali kuomba radhi kwangu, tafadhali nisamehe.” Hivyo basi unajichambua na kujiweka wazi. Inahitaji ujasiri kujichambua na kujiweka wazi. Wakati hakuna mwingine yeyote karibu, iwapo unaomba mbele za Mungu, au unakiri makosa yako, kutubu au kuchambua tabia yako potovu kwa Mungu, unaweza kusema chochote unachotaka, kwa kuwa macho yako yakiwa yamefumbwa, huwezi kuona chochote, ni kama kuzungumzia hewa, na hivyo unaweza kujiweka wazi; unaweza basi kuzungumza kuhusu chochote ulichofikiri, au chochote ulichosema wakati huo, na vile vilenia zako, na udanganyifu wako unaweza. Lakini iwapo lazima ujiweke wazi kwa mtu mwingine, unaweza kupoteza ujasiri wako, na unaweza kupoteza uamuzi wako kufanya hivyo, kwa sababu hutaki aibu, na hivyo ni vigumu sana kuweka vitu hivi katika vitendo. Ukiambiwa uzungumze kwa ujumla, unaweza kusema kuwa wakati mwingine kuna nia binafsi katika mambo unayoyafanya ama kusema, kwamba maneno yako na matendo yana udanganyifu, uchafu, uongo na udanganyifu na pia malengo yako mwenyewe. Lakini kitu kinapokufanyikia, iwapo lazima ujichambue, na kufichua jinsi kilichofanyika kwako kilitendeka kutoka mwanzo hadi mwisho, ni yapi katika maneno uliyoyasema yalikuwa madanganyifu, yalikuwa na nia za aina gani, kile ulichofikiri katika moyo wako, jinsi ulivyokuwa mwovu na wa kudhuru kwa siri, basi unaweza hata kuogopa, na hivyo hutakuwa na hiari ya kujifichua kwa kiwango hicho cha maelezo au kuwa mahususi sana kwa kile unachosema. Kutakuwa hata na watu wanaoisitiri na kusema: “Ilikuwa tu mojawapo ya mambo hayo. Inatosha kusema kwamba mwanadamu ni mdanganyifu mkubwa, mwenye kudhuru kwa siri na asiyetegemewa.” Huku ni kutoweza kukabili kiini chako potovu, udanganyifu na kudhuru kwa siri kwa usahihi; hali yako daima ni ile ya kuepuka, hali yako daima ni ya kuepuka, daima unajisamehe, na huna uwezo wa kuteseka ama kulipa gharama katika suala hili. …
… Usipojiweka wazi, unawezaje kudhibitisha kwamba unakubali kwamba wewe kweli ni mdanganyifu? Usipojiweka wazi, na mtu mwingine asipofanya hivyo pia, nyote mkibaki mmejificha, mkihodhi mipango yenu binafsi mioyoni mwenu, na kila mtu akiendelea kudumisha nafasi ya siri mioyoni mwao, basi unawezaje kuzungumza kuhusu uzoefu halisi? Inawezekanaje yeyote kati yenu awe na uzoefu wa kweli kuwasiliana na mwingine? “Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu” kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako. Na baada ya hayo, wengine wanatambua mambo haya, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli. Hakumaanishi tu kuwa na umaizi katika maneno ya Mungu ama sehemu ya wimbo wa kidini, na kuwasiliana upendavyo na kisha kutofanya mengine zaidi, na kutosema chochote kuhusu maisha yako halisi. Kila mtu huongea kuhusu maarifa ya mafundisho na ya nadharia, na hawasemi chochote kuhusu maarifa yaliyotoka kwa uzoefu halisi. Nyote mnaepuka kuzungumza kuhusu vitu kama hivyo, kuhusu maisha yenu binafsi, kuhusu maisha yenu katika kanisa pamoja na ndugu zenu, na kuhusu dunia yenu ya ndani. Kwa kufanya hili, kunawezaje kuwa na kuwasiliana kwa kweli kati ya watu? Kunawezaje kuwa na imani ya kweli? Hakuwezi kuwa hata kidogo! … Bila aina hii ya mawasiliano na mabadilishano miongoni mwa ndugu katika kanisa, hakungewahi kuwa na upatanifu miongoni mwa ndugu. Hii ni mojawapo ya mahitaji ya kuwa mwaminifu.
Watu wengine husema: “Ni vigumu kuwa mwaminifu. Ni lazima niseme vyote ninavyofikiri katika moyo wangu kwa wengine? Je, haitoshi kuwasiliana kuhusu mambo mazuri? Sihitaji kuwaambia wengine kuhusu upande wangu mwovu ama mpotovu, nahitaji?” Iwapo huzungumzi mambo haya, na hujichambui, basi hutawahi kujijua, na hutawahi kujua wewe ni kitu cha aina gani, na hakutakuwa na uwezekano wa wengine kukuamini. Huu ni ukweli. Iwapo unawataka wengine wakuamini, kwanza lazima uwe mwaminifu. Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako ili kila mtu aweze kuuona moyo wako, kuona vyote unavyofikiri, na kuuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujaribu kujificha. Hapo tu ndipo watu watakuamini na kukuchukua kuwa mwaminifu. Hili ndilo tendo la msingi kabisa, na sharti, la kuwa mwaminifu. Daima unajifanya, daima unasingizia utakatifu, uadilifu, ukubwa na kusingizia sifa za juu za maadili. Huwaruhusu watu kuona upotovu na kushindwa kwako. Unaonyesha taswira ya uongo kwa watu, ili waamini kwamba wewe ni mwadilifu, mkuu, anayejitolea, asiyependelea na asiye na ubinafsi. Huu ni udanganyifu. Usijifanye na usijionyeshe usivyo; badala yake, jiweke wazi na uweke wazi moyo wako ili wengine waone. Iwapo unaweza kuweka wazi moyo wako ili wengine waone, yaani, ikiwa unaweza kuweka wazi yote unayofikiri na kupanga kufanya ndani ya moyo wako—bila kujali iwapo ni nzuri ama mbaya—basi wewe huwi mwaminifu? Iwapo unaweza kujiweka wazi kwa wengine waone, Mungu pia atakuona, na kusema: “Umejiweka wazi kwa wengine wakuone, na hivyo mbele Yangu bila shaka wewe ni mwaminifu pia.” Iwapo unajiweka wazi kwa Mungu wakati wengine hawaoni pekee, na daima unajifanya kuwa mkuu na mwadilifu ama mwenye haki na asiye na ubinafsi mbele yao, basi Mungu atafikiri nini na Mungu atasema nini? Mungu atasema: “Kwa kweli wewe ni mdanganyifu, wewe ni nafiki kabisa na anayejishughulisha na mambo madogo madogo, na wewe si mwaminifu.” Mungu atakuhukumu hivi. Iwapo unataka kuwa mwaminifu, basi bila kujali kile unachofanya mbele ya Mungu ama watu, unapaswa kuweza kuufungua na kuufichua moyo wako kwa wengine. Je, hili ni rahisi kutimiza? Linahitaji muda, ili kuwe na vita ndani ya mioyo yetu, na ili sisi tuendelee kutenda. Kidogo kidogo, mioyo yetu itafunguliwa, na tutaweza kujiweka wazi.
kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iko kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Mungu atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishugulisha na kuitimiza kazi yako. …
… Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hiyo ni, maisha yako ya kawaida ya kiroho, maombi yako, ukaribu wako na Mungu, kula na kunywa neno la Mungu, ushirika na ndugu na dada zako, kuishi maisha yako katika kanisa, na hata huduma yako katika ushirikiano wako ni vitu vyote ambavyo lazima viletwe mbele za Mungu na kuchunguzwa na Yeye. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha. Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi, kadri unavyokuwa katika uwiano na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutasikia wito wa uasherati na ubhadhirifu, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda. Haijalishi kile unachokifanya, hata katika ushirika na ndugu na dada zako, ukiyaleta matendo yako mbele za Mungu na kutafuta uchunguzi wa Mungu, na kama nia yako ni kumtii Mungu Mwenyewe, unachotenda ni sahihi zaidi. Kama tu wewe ni mtu anayeleta kila kitu anachofanya mbele za Mungu na kukubali uchunguzi wa Mungu ndipo utakapokuwa mtu anayeishi kwa hakika katika uwepo wa Mungu.
kutoka katika “Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Ukitaka kuwa na uwezo katika kuutimiza wajibu wako—na sio tu kufanya kitu kwa njia isiyokuwa ya dhati na kumdanganya Mungu—basi lazima ulitatue suala la kuwa mtu mwaminifu. Wakati wa kutimiza wajibu wako lazima ukubali upogoaji na ushughulikiaji, uchunguzaji wa Roho Mtakatifu, na lazima uyatende mambo haya hasa kwa mujibu wa matakwa ya Mungu. Ukigundua kwamba u mzembe, mwombe Mungu. Ukijigundua kuwa mwenye kujaribu kumdanganya Mungu, lazima ulikiri kosa hili. Huwezi kulificha hili, kujisingizia, sembuse kupotosha ukweli ili kuwalaumu mwingine. Unahitaji kuwa makini jinsi hii kuhusu mambo unayoyatenda, na kushughulikia kila neno na tendo lako kwa moyo. Fanya maneno yako yafae uhalisi, tafuta ukweli kutoka kwa ukweli, na usiyatumie maneno ya kuongezea utamu kwa kujisingizia. Ukiligundua kosa, licha ya kumwomba Mungu, lazima pia ulikiri waziwazi kwa wengine. Usijitanibu kwa kuijali sifa yako. Unapaswa kusema ukweli kwa ujasiri. Utendaji kama huu ni wenye maana, na unaahidiwa kuwa wenye manufaa kwako. Kwanza, unaweza kuzidisha imani yako katika kuwa mtu mwaminifu. Pili, unaweza kukufundisha usiogope fedheha, na kuacha majisifu na kutojiona kuwa bora kwako. Tatu, unaweza kukupa ujasiri kusema na kuheshimu kweli. Nne, unaweza kukuza ndani mwako nia ya kuyafikiria kwa makini mambo unayoyatenda. Baada ya kufanya mazoezi jinsi hii kwa muda watu watakuwa waaminifu zaidi katika kutimiza wajibu wao, wenye uhalisi zaidi katika kutenda mambo, na wasiokuwa wenye hila. Miaka michache karibuni watakuwa watu waaminifu ambao wanakichukulia kile wanachokitenda kwa uaminifu na kwa bidii na wanawajibika wanapoyashughulikia mambo. Watu kama hao kwa kwa kulinganisha ni wenye kutegemewa katika kutimiza wajibu na kutenda kazi yao. Nyumba ya Mungu inapowatumia watu kama hao, inaweza kuahidiwa kwamba hakuna litakaloharibika.
kutoka katika “Kuwa Mtu Mwaminifu Pekee Ndiko Toba ya Kweli” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha
Sasa hivi, mko katika mchakato wa kujifunza kuwa watu waaminifu. Katika mchakato wa kujifunza, mnapaswa kuzingatia nini zaidi? Mnapaswa kuzingatia kumjua Mungu, kuzingatia kuelewa ukweli, na lazima mtimize kuingia kwa kweli kutoka kwa upande chanya. Mkiingia kutoka upande chanya, upotovu kutoka kwa upande hasi utapunguka kwa kawaida, na hili ni muhimu. Kwa mfano, ili kuwa mtu mwaminifu, kwanza unahitaji kujiandaa na uhalisi na ukweli wa kuwa mtu mwaminifu. Baada ya kufanya hivi, sehemu yako aminifu itaongezeka na uongo na ujanja utapungua kwa kawaida, siyo? Kama tu kikombe kilichojazwa maji machafu. Huwezi kuyamwaga, kwa hiyo utafanya nini? Lazima umwage maji safi mazuri kiasi ndani ya kikombe hicho, na maji mazuri kwa kawaida yataondoa maji machafu. Sasa lazima mjiandae kwa ukweli, na punde ukweli unapoingia ndani yenu, mambo hasi ndani yenu yatatoweka kwa kawaida.
kutoka katika “Jinsi ya Kutatua Tatizo la Kudanganya Kutoka kwa Chanzo Kwenda Juu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni