10.04.2019

Mtu mdanganyifu ni nani? Kwa nini watu wadanganyifu hawawezi kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:
Kama una udanganyifu mwingi, basi utakuwa na moyo wenye hadhari na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi utakuwa mbali hata zaidi na upendo wa kweli. Na ikiwa unaweza kumshuku Mungu na kumkisia utakavyo, basi wewe bila shaka ni mdanganyifu zaidi kati ya wanadamu wengine.

10.03.2019

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.

10.02.2019

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu.

10.01.2019

Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema.

9.30.2019

Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:
Kufanya muhtasari wa kuishika njia ya Petro katika kumwamini Mungu, ni kuishika njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kujijua na kubadilisha tabia ya mtu. Ni kwa kuishika tu njia ya Petro ndio mtu atakuwa anashika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe hasa jinsi ya kuishika njia ya Petro na jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia yake na vitu vyote vya mwili wake. Lazima ajitolee kwa moyo wote, yaani, ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, azingatie kula na kunywa neno la Mungu, azingatie kutafuta ukweli, utafutaji wa nia ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi zaidi na muhimu zaidi ya utendaji.

9.29.2019

Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Maneno Husika ya Mungu:
Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

9.28.2019

Hukumu ni nini?

Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

9.27.2019

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, huonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na bado Yeye hukabiliwa na uasi mkali na uchukuliwaji wa hatua kali wa ukatili wa ulimwengu wa kidini na serikali ya Kikomunisti ya China. Serikali ya CCP hata huhamasisha vyombo vyake vyote vya habari na majeshi kumshutumu Kristo, kukufuru dhidi Yake, kumtia mbaroni na kumwangamiza. Wakati Bwana Yesu alizaliwa, Mfalme Herode alisikia kuwa “Mfalme wa Israeli” alikuwa amezaliwa na akaamrisha watoto wote wa kiume wauawe Bethlehemu na wa chini ya umri wa miaka miwili; ingekuwa afadhali kwake kuwaua watoto elfu kumi kuliko kumwacha Kristo aishi. Mungu amekuwa mwili ili kuwaokoa wanadamu, hivyo kwa nini ulimwengu wa kidini na serikali kana Mungu hushutumu na kukufuru dhidi ya kuonekana na kazi ya Mungu? Kwa nini wanaipinda nguvu ya nchi yote na kutumia jitihada zote kumtundika Kristo msalabani? Kwa nini wanadamu ni waovu sana, na kwa nini wanamchukia Mungu hivyo na kujiweka dhidi Yake?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Jibu:
Swali hili kweli ni muhimu sana na ni wachache sana katika binadamu wote ndio wanaweza kuelewa hili kabisa! Kwa nini binadamu wanamwasi Mungu kwa kichaa imekuwa vichwa vya habari, na tanzia ya kihistoria ya Kristo mwenye mwili kusulubiwa msalabani inajirudia tena; je, huu si ukweli? Hebu tusome vifungu vingine la Maandiko, Bwana Yesu alisema, “Na hii ndiyo shutuma, ya kwamba mwanga umekuja duniani, na wanadamu walipenda kiza badala ya mwanga, kwa kuwa vitendo vyao vilikuwa viovu. Kwa kuwa kila mtu afanyaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwa mwanga, vitendo vyake visije vikashutumiwa” (Yohana 3:19-20), “Ikiwa dunia ikiwachukia, ninyi mnajua ya kwamba ilinichukia mimi kabla iwachukie ninyi” (Yohana 15:18), “Hiki ni kizazi kibaya” (Luka 11:29). Biblia inasema, “Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19).

9.26.2019

Kwa miaka elfu mbili, dunia nzima ya kidini imeamini kwamba Mungu ni Utatu, na Utatu ni nadharia bora zaidi ya mafundisho yote ya Kikristo. Hivyo, tafsiri ya “Utatu” inashikilia kweli? Utatu una uwepo kweli? Kwa nini unasema kwamba Utatu ni uwongo mkuu mno wa ulimwengu wa kidini?

Nyote mnategemeza uthibitisho wenu kwamba Bwana Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu kwa kile kilichorekodiwa katika Biblia, na kisha mnapomwona Bwana Yesu akimwomba Mungu Baba, hili linadhibitisha zaidi kwenu kwamba Bwana Yesu na Mungu wana uhusiano wa Baba na Mwana. Ongezea kwa hilo ushuhuda wa Roho Mtakatifu na ushuhuda na uwekeaji mipaka wa mitume, na basi mna hakika kwamba Mungu ni Utatu. Kwa miaka elfu mbili, dunia ya dini imekuwa na hakika kwamba Mungu mmoja wa kweli aliyeziumba mbingu na dunia na vitu vyote ni Utatu, hasa kwa sababu Mungu alipata mwili ili Aifanye kazi ya ukombozi, na pia kwa sababu ya suitafahamu zilizoibuka kutokana na watu kukosa kuuelewa ukweli wa kupata mwili.

9.25.2019

Katika miaka ya hivi karibuni, makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali katika ulimwengu wa kidini yamekosa matumaini zaidi na zaidi, watu wamepoteza imani yao ya asili na upendo na wamekuwa hasi zaidi na zaidi na dhaifu. Pia tunahisi kunyauka kwa roho na tunahisi kuwa hatuna chochote cha kuhubiri na kwamba sote tumepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Tafadhali tuambie, kwa nini ulimwengu wote wa kidini umekosa matumaini hivyo? Mungu kweli anauchukia na umetelekezwa na Mungu? Tunafaaje kuelewa laana ya Mungu ya ulimwengu wa kidini katika Kitabu cha Ufunuo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Sasa, dunia nzima ya dini inakumbwa na ukiwa ulioenea pote, isiyo na kazi ya Roho Mtakatifu, na imani na upendo wa watu wengi umepungua—hili tayari limekuwa ukweli unaokubalika. Nini hasa ni sababu ya msingi ya ukiwa katika jumuiya ya dini ni swali ambalo sisi wote lazima tulielewe kikamilifu. Kwanza, hebu tuangalie nyuma kwa muda kwa mbona hekalu liligeuka la ukiwa katika siku za baadaye za Enzi ya Sheria, na kisha tutaweza kuelewa kikamilifu sababu ya ukiwa wa dunia ya dini katika siku za mwisho. Katika siku za baadaye za Enzi ya Sheria, viongozi wa Kiyahudi hawakuzifuata amri za Mungu Waliitembea njia yao wenyewe na kumwasi Mungu; hii ndiyo sababu kuu ambayo ilisababisha ukiwa wa hekalu moja kwa moja.

9.24.2019

Ingawa wachungaji na wazee wa kanisa wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na wanaitembea njia ya Mafarisayo wanafiki, tunamwamini Bwana Yesu, sio wachungaji na wazee wa kanisa, kwa hiyo unawezaje kusema kwamba sisi pia tunaitembea njia ya Mafarisayo? Je, hatuwezi kuokolewa kwa kumwamini Mungu ndani ya dini?

Kuna watu wengi katika dini ambao wanaamini na kuabudu bila kufikiria na kufuata Mafarisayo. Kwa hiyo kama njia wanayoenda ni njia ya Mafarisayo ni dhahiri mara tu unapofikiri juu yake. Unathubutu kusema kuwa unaabudu na kuwalinda Mafarisayo katika moyo wako lakini huna uhusiano na dhambi zao? Unathubutu kusema kuwa unawafuata Mafarisayo wanafiki, lakini wewe si kama wao, mtu anayepinga Mungu? Je, bado hatuwezi kung’amua swali rahisi kama hilo? Aina ya mtu unayefuata ni aina ya njia unayotembea. Ikiwa unawafuata Mafarisayo basi uko kwenye njia ya Mafarisayo. Ukitembea njia ya Mafarisayo basi wewe kiasili ni aina hiyo ya mtu kama Mafarisayo.

9.23.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hushikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na watu wengi huwatii na kuwafuata—huu ni ukweli. Unasema kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hawaukubali ukweli wa Mungu kuwa amekuwa mwili, kwamba hawaamini ukweli ulioonyeshwa na Mungu mwenye mwili na kwamba wanaitembea njia ya Mafarisayo, na tunakubaliana na jambo hili. Lakini kwa nini unasema kuwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote ni Mafarisayo wanafiki, kuwa wote ni wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kwamba wataingia katika maangamizo mwishoni? Hatuwezi kukubali jambo hili kwa wakati huu. Tafadhali shiriki unachotegemeza dai hili, kwamba watu hawa hawawezi kuokolewa na kwamba ni lazima wote waingie katika maangamizo.

Asili ya jinsi watu katika jamii ya kidini wanavyomkana Mungu zinaweza tu kufichuliwa na kuchanguliwa baada ya kuja kwa Kristo mwenye mwili. Hakuna wanadamu wapotovu wanaoweza kuutambua ukweli na asili ya jamii ya kidini ya kumkana Mungu, kwa sababu wanadamu wapotovu hawana ukweli. Wanaweza tu kudhibitiwa, kuchanganywa, na kuchezewa na wachungaji wa uwongo na pepo wapinga Kristo ili kujiunga nao katika kufanya uovu, na kuwa watumishi na washiriki wa Shetani katika kumkana Mungu. Hili ni jambo la kawaida. … Hebu tuone jinsi, wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alivyoufichua ukweli na asili ya jinsi pepo wabaya wapinga Kristo katika jamii ya kidini walivyomuasi Mungu daima: