Bibilia inasema: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10). Tunaamini kwamba Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki kupitia imani. Aidha, tunaamini kwamba mtu akiokolewa mara moja, basi ameokolewa milele, na Bwana atakaporudi tutanyakuliwa na tutaingia katika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo kwa nini unashuhudia kuwa tunapaswa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kabla ya kuweza kuokolewa na kuletwa katika ufalme wa mbinguni?
Jibu:
Waumini wote katika Bwana hufikiria: Bwana Yesu alitukomboa Alipokufa msalabani, hivyo tayari tumeondolewa dhambi zote. Bwana hatuoni tena kama wenye dhambi. Tumekuwa wenye haki kupitia kwa imani yetu. Mradi tuvumilie hadi mwisho, tutaokolewa. Bwana atakaporudi tutanyakuliwa moja kwa moja kuingia katika ufalme wa mbinguni. Naam, huo ndio ukweli? Je, Mungu aliwahi kamwe kutoa ushahidi katika maneno Yake wa kuunga mkono madai haya? Kama mtazamo huu hauambatani na ukweli, matokeo yatakuwa ni yapi? Sisi ambao tunamwamini Bwana tunapaswa kutumia maneno Yake mwenyewe kama msingi wa mambo yote.