XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu
Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo? Ni nini asili yao?
“Naye akaanza kuzungumza nao kwa kutumia mifano. Mtu fulani alipanda shamba la mizabibu, naye akalizingira kwa ugo, naye akachimba mahala pa shinikizo ya zabibu, naye akaunda mnara, naye akalipanga kwa wakulima, na kuenda katika nchi ya mbali. Na kwa majira yake akamtuma mtumishi kwa wakulima wale, ili aweze kupata matunda ya shamba hilo la mizabibu kutoka kwa wakulima. Nao wakamkamata, na kumpiga, na kumtoa humo bila chochote. Na tena akamtuma mtumishi mwingine; nao wakamtupia mawe, na kumjeruhi kichwani, na kumwondoa humo kwa aibu.