Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu
Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi?