Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Nne
Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kunawapa Rehema ya Mungu na
Kwabadilisha Hatima Zao Wenyewe
Je, kulikuwa na kuhitilafiana kokote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu kwa wakati ule ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotajwa kwenye Biblia: "Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ya maovu" na "kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwake."