5.16.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Tatu



Kwa sababu sasa tumemaliza kuzungumza kuhusu Shetani, hebu turudie kuzungumza kuhusu Mungu wetu. Wakati wa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, matamshi machache sana ya moja kwa moja ya Mungu yamerekodiwa katika Biblia, na yale yaliyorekodiwa ni rahisi sana. Hivyo wacha tuanzie mwanzoni. Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? (Ndiyo, tunaweza.) Mnaweza kufikiria kwamba sentensi hii kwa kulinganishwa ni pana na tupu, lakini kuzungumza hasa, kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida. Iwe ili mwanadamu ahifadhi kanuni Zake ama ahifadhi sheria Zake, lengo la Mungu ni kwa mwanadamu kutomwabudu Shetani, kutodhuriwa na Shetani; hii ndiyo ya msingi sana, na hii ndiyo ilifanywa mwanzoni. Mwanzoni kabisa, wakati mwanadamu hakuelewa mapenzi ya Mungu, Alichukua baadhi ya sheria na kanuni rahisi na kuweka kauli zilizoshughulikia masuala yote yanayoweza kufikiriwa. Kauli hizi ni rahisi sana, lakini ndani yake kuna mapenzi ya Mungu. Mungu anamthamini, Anamtunza na kwa hakika Anampenda mwanadamu. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba moyo Wake ni mtakatifu? Tunaweza kusema kwamba moyo wake ni safi? (Ndiyo.) Je, Mungu anazo nia zilizofichwa? (La.) Kwa hivyo hili lengo Lake ni sahihi na halisi? (Ndiyo.) Licha ya kauli alizoweka Mungu, katika kazi Yake yote yana athari halisi kwa mwanadamu, na zinaongoza njia. Kwa hivyo kuna fikira zozote za kibinafsi kwa akili ya Mungu? Je, Mungu anayo malengo zaidi kuhusiana na mwanadamu, ama Anataka kumtumia mwanadamu kwa jinsi fulani? (La.) Sivyo hata kidogo. Mungu anafanya Asemavyo, na pia Anafikiria namna hii kwa moyo Wake. Hakuna mchanganyiko wa madhumuni, hakuna fikira za kibinafsi. Hajifanyii chochote, lakini Anamfanyia mwanadamu kila kitu kabisa, bila malengo ya kibinafsi. Ingawa Ana mipango na nia kwa mwanadamu, Hajifanyii chochote. Kila kitu Anachofanya kinafanyiwa mwanadamu tu, kumlinda mwanadamu, kumhifadhi mwanadamu dhidi ya kupotezwa. Hivyo si moyo huu ni wenye thamani? (Ndiyo.) Unaweza kuona dokezo hata kidogo zaidi la huu moyo wenye thamani kwa Shetani? Mnaweza kuliona? (La.) Hamuwezi kuliona dokezo moja la moyo huu kwa Shetani. Kila kitu anachofanya Mungu kinafichuliwa kiasili. Kwa kuangalia njia Mungu anafanya kazi, Anafanyaje kazi? Je, Mungu anazichukua sheria hizi na maneno Yake na kuyafunga pamoja kwa kukaza katika kichwa cha kila mtu kama fingo la pete ya dhahabu[b], Akizilazimisha kwa kila mtu? Je, Anafanya kazi namna hii? (La.) Kwa hivyo Mungu anafanya kazi Yake namna gani? (Anatuongoza.) Hiki ni kipengele kimoja. Kuna vingine? Mungu anawafanyia kazi kwa njia nyingi, inaweza kuwaje mmekosa vitu vya kusema baada ya moja tu? (Anashauri na kutia moyo.) Kuna kipengele cha pili. Vingine zaidi? Je, Anatishia? Je, Anawazungumzia kwa njia inayochanganya? (La.) Wakati huelewi ukweli, Mungu hukuongoza vipi? (Yeye huangaza mwangaza.) Anaangaza mwangaza kwako, akikwambia wazi kwamba haya hayaambatani na ukweli, na kile unachofaa kufanya. Kutoka kwa njia hizi ambazo Mungu anafanya kazi, unahisi kwamba una uhusiano wa aina gani na Mungu? Zinakufanya uhisi kwamba Mungu yuko mbali na ufahamu wako? (La.) Hivyo zinakufanya uhisi vipi? Mungu yuko hasa karibu na wewe, hakuna umbali kati yenu. Wakati Mungu anakuongoza, Anapokukimu, Anapokusaidia na kukutunza, unahisi urafiki wa Mungu, kuheshimika Kwake, unahisi jinsi Anavyopendeza, jinsi Alivyo mwema. Lakini wakati Mungu anaposhutumu upotovu wako, ama Anapokuhukumu na kukufundisha nidhamu kwa sababu ya kuasi dhidi Yake, Mungu anatumia njia gani? Anakushutumu kwa kutumia maneno? Anakufundisha nidhamu kupitia mazingira yako na kupitia watu, masuala na mambo? (Ndiyo.) Nidhamu hii imefika kiwango kipi? (Kwa kiwango ambacho mwanadamu anaweza kuvumilia.) Kiwango Chake cha nidhamu kinafikia mahali sawa ambapo Shetani anamdhuru mwanadamu? (La.) Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, upendo, laini na ya kujali, kwa njia hasa iliyopimwa na ni sahihi. Njia Yake haikufanyi kuhisi hisia kali kama vile, "Mungu lazima aniwache nifanye hivi" ama "Lazima Mungu aniache nifanye vile." Mungu kamwe hakupi mawazo ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika. Sivyo? Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi kwamba Mungu ni mtakatifu na asiyekosewa? (Ndiyo.) Unahisi ukiwa mbali na Mungu nyakati hizi? Unahisi kutishiwa na Mungu? (La.) La, badala yake, unahisi heshima inayomcha Mungu. Je, watu wanahisi haya mambo yote kwa sababu tu ya kazi ya Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo wangekuwa na hisia hizi iwapo Shetani angefanya kazi kwa mwanadamu? (La.) Mungu anatumia maneno Yake, ukweli Wake na uhai Wake kuendelea bila kusita kumtolea mwanadamu, kumtunza mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati mwanadamu anahisi huzuni, Mungu kwa hakika hazungumzi kwa ukali, akisema, "Usihisi huzuni. Mbona unahisi huzuni? Kwa nini uwe mnyonge? Kuna nini ya kuwa mnyonge kuihusu? Wewe ni mnyonge sana, na daima una huzuni. Kuna haja gani ya kuishi? Kufa tu!" Je, Mungu anafanya kazi hivi? (La.) Je, Mungu ana mamlaka ya kutenda namna hii? (Ndiyo.) Lakini Mungu anatenda namna hii? (La.) Mungu hatendi hivi kwa sababu ya kiini Chake, kiini cha utakatifu wa Mungu. Upendo Wake kwa mwanadamu, kuthamini na utunzaji Wake wa mwanadamu haviwezi kuelezwa wazi kwa sentensi moja au mbili. Si kitu kinacholetwa na kujisifu kwa binadamu lakini ni kitu kinacholetwa kwa vitendo halisi; ni ufunuo wa kiini cha Mungu. Je, hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi zinaweza kumruhusu mwanadamu kuona utakatifu wa Mungu? Kwa hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi, zikiwemo nia nzuri za Mungu, zikiwemo athari ambazo Mungu anataka kutimiza kwa mwanadamu, zikiwemo njia mbalimbali Mungu anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu, aina ya kazi Anayofanya, kile Anachotaka mwanadamu kuelewa—umeona uovu ama ujanja wowote katika nia nzuri za Mungu? (La.) Hivyo, kwa kila kitu Mungu anafanya, kila kitu Mungu anasema, kila kitu anachofikiria katika moyo Wake, na pia kiini chote cha Mungu anachofichua—tunaweza kumwita Mungu mtakatifu? (Ndiyo.) Mwanadamu yeyote amewahi kuona utakatifu huu duniani, ama kwake mwenyewe? Mbali na Mungu, umewahi kuuona kwa mtu yeyote ama kwa Shetani? (La.) Kutoka kwa yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, tunaweza kumwita Mungu wa kipekee, Mungu mtakatifu Mwenyewe? (Ndiyo.) Yote ambayo Mungu anampa mwanadamu, yakiwemo maneno ya Mungu, njia tofauti ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu, kile ambacho Mungu anamwambia mwanadamu, kile ambacho Mungu anamkumbusha mwanadamu kuhusu, kile ambacho Anashauri na kutia moyo, vyote vimetoka kwa kiini kimoja: Vyote vimetoka kwa utakatifu wa Mungu. Iwapo hakungekuwa na Mungu mtakatifu kama huyu, hakuna mwanadamu ambaye angechukua nafasi Yake kufanya kazi Anayofanya. Iwapo Mungu angewachukua watu hawa na kuwakabidhi kabisa kwa Shetani, mmewahi kuzingatia mngekuwa katika hali ya aina gani leo? Nyinyi nyote mngekuwa mmeketi hapa? Kamili na wasioharibika? (La.) Kwa hivyo mngekuwa vipi? Pia mngesema: "Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo"? Mngejitamba hivyo, kutokuwa na haya kabisa na kujigamba bila haya mbele ya Mungu, na kuenda dalji mkizungumza kwa njia kama hiyo? (Ndiyo.) Mngeweza kwa asilimia mia moja! Mngeweza kabisa! Mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu unawaruhusu kuona kwamba asili ya Shetani ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kiini chake ni tofauti kabisa na cha Mungu. Kiini kipi cha Shetani ni kinyume cha utakatifu wa Mungu? (Uovu wake.) Asili ya uovu ya Shetani ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Watu wengi zaidi hawatambui maonyesho haya ya Mungu na kiini hiki cha utakatifu wa Mungu ni kwa sababu wanamilikiwa na Shetani, ndani ya upotovu wa Shetani na ndani ya boma anamoishi Shetani. Hawajui utakatifu ni nini ama jinsi ya kufafanua utakatifu. Hata unapoona utakatifu wa Mungu, bado huwezi kuufafanua kuwa utakatifu wa Mungu kwa uhakika wowote. Hii ni tofauti katika maarifa ya mwanadamu ya utakatifu wa Mungu.

      Ni sifa ya uwakilishi gani inaonyeshwa na kazi ya Shetani kwa mwanadamu? Mnapaswa kujua kuhusu hii kutokana na uzoefu wenu wenyewe—sifa ya uwakilishi zaidi ya Shetani, kitu ambacho anafanya zaidi, kitu ambacho anajaribu kufanya na kila mtu. Ana sifa ambayo pengine hamwezi kuona, ili msiweze kufikiria jinsi Shetani anatisha na wa kuchukia. Kuna mtu anayejua sifa hii ni nini? Niambieni. (Kila kitu anachofanya kinafanywa kumdhuru mwanadamu.) Anafanya vitu kumdhuru mwanadamu. Anamdhuru mwanadamu vipi? Mnaweza kunionyesha hasa zaidi na kwa kina? (Anamshawishi, anamlaghai na kumjaribu mwanadamu.) Hii ni sahihi, hii inaonyesha vipengele vingi. Kuna vingine? (Anamdanganya mwanadamu.) Anadanganya, anashambulia na anatuhumu. Ndiyo, haya yote. Kuna mengine zaidi? (Anasema uwongo.) Udanganyifu na uongo hujitokeza kiasili kabisa kwa Shetani, Anafanya hivi mara nyingi hadi uongo unabubujika kutoka kwa mdomo wake bila yeye hata kuhitaji kufikiria. Mengine zaidi? (Anapanda mfarakano.) Hii si muhimu sana. Nitawaelezea kitu ambacho kitawatisha, lakini Sifanyi hivyo ili kuwaogopesha. Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na mwanadamu anathaminiwa katika mtazamo na moyo wa Mungu. Kinyume na hayo, Shetani anamthamini mwanadamu? Hamthamini mwanadamu. Anataka nini na mwanadamu? Anataka kumdhuru mwanadamu, anachofikiria tu ni kumdhuru mwanadamu. Hii si sahihi? Wakati anafikiria kumdhuru mwanadamu, anafanya hivyo katika hali ya dharura ya akili? (Ndiyo.) Kwa hivyo inapokuja kwa kazi ya Shetani kwa mwanadamu, hapa Nina maneno mawili yanayoweza kuelezea vizuri asili yenye nia mbaya na ovu ya Shetani, yanayoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka kumiliki na kumtawala kwa nguvu, kila mmoja wao, ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. "Umiliki wa nguvu" unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anakutawala, kutimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Mnahisi vipi mnaposikia haya? (Tuna hofu na woga katika mioyo yetu.) Mnahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Mnapohisi kuchukizwa, mnafikiria Shetani hana haya? (Ndiyo.) Mnapofikiria Shetani hana haya, mnahisi kuchukizwa na wale watu walio karibu nanyi ambao daima wanataka kuwatawala, wale walio na matarajio yasiyowezekana ya hadhi na maslahi yao? (Ndiyo.) Hivyo ni mbinu gani anazotumia Shetani kumtawala kwa nguvu na kummiliki mwanadamu? Mnaelewa hii vizuri? Mnaposikia virai hivi viwili vya "umiliki wa nguvu" na "utawala," mnapata hisia isiyo ya kawaida na mnahisi maudhi, sivyo? Je, mnapata kionjo cha ladha yao mbovu? Bila kibali ama maarifa yako anakutawala, anakumiliki na kukupotosha. Unaweza kuonja nini kwa moyo wako? Chuki (Ndiyo.) Maudhi? (Ndiyo.) Wakati unahisi hii chuki na maudhi kwa njia hii ya Shetani, una hisia gani kwa Mungu? (Kushukuru.) Kushukuru Mungu kwa kukuokoa. Kwa hivyo sasa, wakati huu, unayo hamu ama matakwa ya kumwacha Mungu kuongoza yako yote na kutawala yako yote? (Ndiyo.) Kwa muktadha upi? Unasema ndiyo kwa sababu unaogopa kumilikiwa kwa nguvu na kutawaliwa na Shetani? (Ndiyo.) Huwezi kuwa na mawazo kama haya, siyo sahihi. Usiwe na hofu, Mungu yuko hapa. Hakuna chochote cha kuhofia, siyo? Ukishaelewa asili mbovu ya Shetani, unapaswa kuwa na uelewa sahihi zaidi ama upendo wa kina wa mapenzi ya Mungu, nia nzuri za Mungu, huruma ya Mungu na stahamala kwa mwanadamu na tabia Yake ya haki. Shetani ni wa kuchukia sana, lakini ikiwa hii bado haitii moyo upendo wako kwa Mungu na utegemezi na uaminifu wako kwa Mungu, basi wewe ni mtu wa aina gani? Uko tayari kumwacha Shetani akudhuru hivyo? Baada ya kuona uovu na ubaya wa Shetani, tunamgeuza na kisha kumwangalia Mungu. Maarifa yako ya Mungu sasa yamepitia mabadiliko yoyote? (Ndiyo.) Mabadiliko ya aina gani? Tunaweza kusema Mungu ni mtakatifu? Tunaweza kusema Mungu hana dosari? "Mungu ni utakatifu wa kipekee"—Mungu anaweza kuvumilia jina hili? (Ndiyo.) Hivyo kwa dunia na miongoni mwa mambo yote, ni Mungu Mwenyewe pekee anayeweza kuvumilia huu uelewa wa mwanadamu? Kuna wengine? (La.) Hivyo, ni nini hasa Mungu anampatia mwanadamu? Je, Anakupa tu utunzaji, wasiwasi na kukutia maanani kidogo wakati huko makini? Mungu amempa nini mwanadamu? Mungu amempa mwanadamu uhai, Amempa mwanadamu kila kitu, na amempa mwanadamu bila masharti bila kudai chochote, bila nia zozote za siri. Anatumia ukweli, Anatumia maneno Yake, Anatumia uhai Wake kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu, kumtoa mwanadamu mbali na madhara ya Shetani, mbali na majaribio ya Shetani, mbali na ushawishi wa Shetani na kumruhusu mwanadamu kuona wazi asili mbovu ya Shetani na uso wake unaotisha. Je, upendo na wasiwasi wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli? Ni kitu ambacho kila mmoja wenu anaweza kupitia? (Ndiyo.)

      Kumbuka maisha yenu hadi sasa kwa yote ambayo Mungu amekufanyia katika miaka yote ya imani yako. Iwapo unaihisi kwa kina au la, haikuwa ya umuhimu sana? Haikuwa kile ulichohitaji zaidi kupata? (Ndiyo.) Huu si ukweli? Huu si uhai? (Ndiyo.) Kwa hivyo Mungu amewahi kukupa nuru kurudisha chochote ama kulipia kitu baada ya Yeye kukupa vitu hivi? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni yapi? Mbona Mungu anafanya hivi? Mungu pia ana lengo la kukumiliki? (La.) Je, Mungu anataka kuwa mfalme katika moyo wa mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini tofauti kati ya Mungu kuwa mfalme na umiliki wa nguvu wa Shetani? Mungu anataka kupata moyo wa wanadamu, Anataka kumiliki moyo wa mwanadamu—hii inamaanisha nini? Je, inamaanisha kwamba Mungu anataka mwanadamu kuwa vikaragosi Vyake? Mashine Yake? (La.) Kwa hivyo madhumuni ya Mungu ni nini? Kuna tofauti kati ya Mungu kutaka kumiliki moyo wa mwanadamu na umiliki wa nguvu wa Shetani na utawala wa mwanadamu? (Ndiyo.) Tofauti ni nini? Unaweza kuniambia wazi? (Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee.) Shetani anaifanya kupitia kwa nguvu ilhali Mungu anaacha mwanadamu ajitolee. Hii ndiyo tofauti? Kwa hivyo usipojitolea, nini kitafanyika basi? Usipojitolea, Mungu anafanya chochote? (Anapeana mwongozo na nuru, lakini kama mwishowe mwanadamu hayuko radhi, Hamlazimishi.) Mungu anataka moyo wako kufanyia nini? Na zaidi ya hayo, kwa nini Mungu anataka kukumiliki? Mnaelewa vipi ndani ya mioyo yenu "Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu"? Ni lazima tuwe na haki kwa Mungu hapa, vinginevyo watu daima hawataelewa, na kufikiri: "Mungu daima anataka kunimiliki. Anataka kunimiliki kwa nini? Sitaki kumilikiwa, nataka tu kuwa mimi mwenyewe. Mnasema Shetani anawamiliki watu, lakini Mungu pia anawamiliki watu: Haya si sawa? Sitaki kumwacha yeyote kunimiliki. Mimi ni mimi mwenyewe!" Tofauti hapa ni nini? Chukua dakika kuifikiria. (Nafikiri Mungu anataka kupata moyo wa mwanadamu na kumiliki moyo wa mwanadamu ili kumwokoa mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu.) Kile unachosema ni lengo la usimamizi wa Mungu wa mwanadamu—kumfanya kuwa kamili. Unaelewa "miliki" inamaanisha nini hapa? (Inamaanisha kutomwacha Shetani kumiliki mwanadamu. Iwapo Mungu yuko katika umiliki, basi Shetani hana njia ya kummiliki mwanadamu.) Unamaanisha Mungu ndiye mmiliki wa kwanza; kama nyumba tupu, yeyote anayeingia wa kwanza anakuwa bwana wa nyumba hiyo. Anayekuja baadaye hawezi kuwa bwana wa nyumba, lakini badala yake anakuwa mtumishi, ama sivyo hawezi kuingia kamwe. Unamaanisha hivi? (Ndiyo, namaanisha kitu kama hiki.) Kuna yeyote aliye na mtazamo tofauti? (Uelewa wangu wa "Mungu kumiliki moyo ya wanadamu" ni kwamba Mungu anatuchukulia kama familia Yake, kututunza na kutupenda, Shetani anamiliki moyo wa mwanadamu ili kutuvunja, kutudhuru.) Huu ndio uelewa wako wa "Mungu hummiliki wanadamu." Kuna uelewa ama maoni tofauti? (Mungu hummiliki wanadamu kwa kutumia neno Lake, kwa matumaini kwamba mwanadamu anaweza kukubali neno la Mungu kama maisha yake, ili mwanadamu aweze kuishi kulingana na neno la Mungu.) Hii ndiyo maana ya kweli nyuma ya "Mungu hummiliki mwanadamu," sivyo? Kuna maoni tofauti? (Mtazamo wangu ni kwamba Mungu ni mfano halisi wa ukweli kwa hivyo Mungu anataka kutupa ukweli mzima, na kwa sababu tunapata ukweli huu na tunaletwa chini ya utunzaji na ulinzi Wake, tunaweza basi kuepuka kukutana na mipango ya ujanja ya Shetani na kudhuriwa na yeye. Kuzungumza kwa vitendo, Mungu anataka kupata moyo wa mwanadamu ili mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida duniani na kupata baraka za Mungu.) Lakini bado hujagusia maana ya ukweli ya "Mungu humiliki moyo wa mwanadamu." (Kwa asili, mwanadamu aliumbwa na Mungu, kwa hivyo mwanadamu anapaswa kumwabudu na kumrudia. Mwanadamu ni wa Mungu.) Nawauliza, je "Mungu hummiliki mwanadamu" ni kirai tupu? Umiliki wa Mungu wa mwanadamu unamaanisha kwamba Anaishi katika moyo wako na anatawala kila neno na kusonga kwako? Akikwambia uketi, huthubutu kusimama? Akikwambia uende Mashariki, huthubutu kwenda Magharibi? Je, ni umiliki unaomaanisha kiti kama hiki? (La.) Kwa hivyo ni nini? (Inaamisha kwa mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha kile Mungu anacho na alicho.) Kwa miaka hii yote Mungu amemsimamia mwanadamu, kwa kazi Yake kwa mwanadamu hadi sasa kwa hatua hii ya mwisho, ni athari ipi imekusudiwa kwa mwanadamu kuhusu maneno yote ambayo Amesema? Je, ni kwamba mwanadamu anaishi kulingana na kile anacho Mungu na alicho? Kwa kuangalia maana halisi ya "Mungu humiliki moyo wa mwanadamu," inaonekana kama Mungu anachukua moyo wa mwanadamu na kuumiliki, Anaishi ndani yake na Hatoki nje tena; Anaishi ndani yake na kuwa bwana wa moyo wa mwanadamu, kutawala na kupanga moyo wa mwanadamu atakavyo, ili mwanadamu lazima aende asemapo Mungu aende. Katika kiwango hiki cha maana, inaonekana ni kama kila mtu alikuwa amekuwa Mungu, amemiliki kiini cha Mungu, amemiliki tabia ya Mungu. Kwa hivyo hapa, mwanadamu pia angeweza kufanya vitendo na matendo ya Mungu? Je, "umiliki" unaweza kuelezewa kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo ni nini? (Watu ambao Mungu anataka si vikaragosi, wana fikira na mioyo yao ni hai. Kwa hivyo, umiliki wa Mungu wa wanadamu ni kwa matumaini kwamba mwanadamu anaweza kuwa na fikira na anaweza kuhisi furaha na huzuni ya Mungu; mwanadamu na Mungu wanaathiriana.) Nawauliza hii: Je, maneno na ukweli wote Mungu anampa mwanadamu ni ufunuo wa kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho? (Ndiyo.) Hii ni ya uhakika. Lakini je, maneno yote Mungu anampa mwanadamu ni ya Mungu Mwenyewe kuweka katika vitendo, ya Mungu Mwenyewe kumiliki? Chukua dakika moja kuifikiria? Wakati Mungu anamhukumu mwanadamu, Anafanya hivi kwa sababu ya nini? Maneno haya yalitoka wapi? Ni nini yaliyomo katika maneno haya ambayo Mungu anazungumza Anapomhukumu mwanadamu? Ni nini msingi wake? Msingi wake ni tabia potovu ya mwanadamu? (Ndiyo.) Kwa hivyo athari iliyofikiwa na hukumu ya Mungu ya mwanadamu imetokana na kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo umiliki wa Mungu wa mwanadamu ni kirai tupu? Kwa hakika sicho. Kwa hivyo mbona Mungu anasema maneno haya? Ni nini madhumuni Yake ya kusema maneno haya? Anataka kutumia maneno haya kwa maisha ya mwanadamu? (Ndiyo.) Mungu anataka kutumia ukweli huu wote ambao amezungumza kwa maisha ya mwanadamu. Wakati mwanadamu anachukua ukweli huu wote na neno la Mungu na kuyabadilisha katika maisha yake, mwanadamu basi anaweza kumtii Mungu? Mwanadamu basi anaweza kumcha Mungu? Mwanadamu basi anaweza kuepuka maovu? Wakati mwanadamu amefika hapa, anaweza basi kutii ukuu na mipango ya Mungu? Mwanadamu sasa yuko katika nafasi ya kutii mamlaka ya Mungu? Wakati watu kama Ayubu, ama kama Petro wanafika mwisho wa barabara yao, wakati maisha yao yanaweza kufikiriwa kuwa yamekomaa, wakati wako na uelewa halisi wa Mungu—Shetani bado anaweza kuwapoteza? Shetani bado anaweza kuwamiliki? Shetani bado anaweza kuwatawala kwa nguvu? (La.) Kwa hivyo huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni mtu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? (Ndiyo.) Katika kiwango hiki cha maana, unamwonaje mtu huyu ambaye amepatwa kabisa na Mungu? Kwa Mungu, katika hali hii tayari Amemiliki moyo wa mtu huyu. Lakini mtu huyu anahisi nini? Je, ni kwamba neno la Mungu, mamlaka ya Mungu, na njia ya Mungu yamekuwa uhai ndani ya mwanadamu, basi uhai huu unamiliki utu wote wa mwanadamu, na unafanya yote anayozidi pamoja na kiini chake kutosha kumridhisha Mungu? Kwa Mungu, moyo wa binadamu wakati huu umemilikiwa na Yeye? (Ndiyo.) Mnaelewaje kiwango hiki cha maana sasa? Je, ni Roho wa Mungu anayekumiliki? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa kinachokumiliki? (Neno la Mungu.) Ni njia ya Mungu na neno la Mungu. Ni ukweli ambao umekuwa maisha yako, na ni neno la Mungu ambayo yamekuwa maisha yako. Wakati huu, mwanadamu basi ana maisha yanayotoka kwa Mungu, lakini hatuwezi kusema kwamba haya maisha ni maisha ya Mungu. Kwa maneno mengine, hatuwezi kusema kwamba maisha ambayo mwanadamu anapaswa kupata kutoka kwa neno la Mungu ni maisha ya Mungu. Hivyo, licha ya muda ambao mwanadamu anamfuata Mungu, licha ya idadi ya maneno ambayo mwanadamu anapata kutoka kwa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa Mungu. Hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hata kama siku moja Mungu aseme, "Nimemiliki moyo wako, sasa unamiliki maisha Yangu," utahisi basi kwamba wewe ni Mungu? (La.) Utakuwa nini basi? Hutakuwa na utii kabisa wa Mungu? Mwili na moyo wako hautajawa na maisha Mungu amekupa? Huu ni udhihirisho wa kawaida wakati Mungu anamiliki moyo wa mwanadamu. Huu ni ukweli. Kwa hivyo kuuangalia kutoka kipengele hiki, mwanadamu anaweza kuwa Mungu? (La.) Wakati mwanadamu amepata maneno yote ya Mungu, wakati mwanadamu anaweza kumcha Mungu na kuepukana na maovu, mwanadamu basi anaweza kumiliki utambulisho wa Mungu? (La.) Mwanadamu anaweza basi kumiliki kiini cha Mungu? (La.) Licha ya kile kitakachofanyika, mwanadamu bado ni mwanadamu wakati yote yamesemwa na kufanywa. Wewe ni kiumbe; wakati umepokea neno la Mungu kutoka kwa Mungu na kupokea njia ya Mungu, unamiliki tu maisha ambayo yanatoka kwa neno la Mungu, na kamwe huwezi kuwa Mungu.

      Tukirudia mada yetu hivi sasa, Niliwauliza swali—je, Ibrahimu ni mtakatifu? (La.) Yeye si mtakatifu, na mnaelewa hii sasa, sivyo? Ayubu ni mtakatifu? (La.) Ndani ya utakatifu huu kuna kiini cha Mungu. Mwanadamu hana kiini cha Mungu ama tabia ya Mungu. Hata wakati mwanadamu amepitia maneno yote ya Mungu na kumiliki kiini cha neno la Mungu, mwanadamu bado hawezi kuitwa mtakatifu; mwanadamu ni mwanadamu. Mnaelewa, sivyo? Kwa hivyo mnakielewaje kirai hiki "Mungu anakaa katika moyo ya mwanadamu" sasa? (Ni maneno ya Mungu, njia ya Mungu na ukweli Wake yanayokuwa maisha ya mwanadamu.) Umekariri maneno haya. Natumai mtakuwa na uelewa wa kina. Watu wengine wanaweza kuuliza, "Kwa hivyo mbona useme kwamba wajumbe na malaika wa Mungu si watakatifu?" Mnafikiria nini kuhusu swali hili? Labda hamjalifikiria mbeleni. Nitatumia mfano rahisi: Unapowasha roboti, inaweza kucheza ngoma na kuongea, na unaweza kuelewa inachosema, lakini unaweza kuiita nzuri? Unaweza kuiita yenye uhai? Unaweza kusema hayo, lakini roboti hii haitaelewa kwa sababu haina uhai. Unapozima uletaji wake wa umeme, bado inaweza kusongasonga? Wakati roboti hii inaamshwa, unaweza kuona ina uhai na ni nzuri. Unaitathmini, iwe tathmini ya kina au ya juujuu, lakini iwe vipi macho yako yanaweza kuiona ikisonga. Lakini unapozima uletaji wake wa umeme, unaona tabia ya aina yoyote kwake? Unaona ikiwa na kiini cha aina yoyote? Unaelewa maana ya kile ninachosema? (Ndiyo.) Hivyo ni kusema, ingawaje roboti hii inaweza kusonga na inaweza kuacha, kamwe hungeweza kuielezea kama kuwa na aina yoyote ya kiini. Huu si ukweli? Hatutazungumzia haya zaidi. Yametosha kwenu kuwa na uelewa wa jumla wa maana. Hebu tutamatishe ushirika wetu hapa. Kwaheri!


Desemba 17, 2013

Tanbihi:

     b. "Fingo la pete ya dhahabu" inarejelea riwaya maarufu ya Kichina "Safari ya Magharibi," ambamo mtawa Xuanzang anatumia fingo kumleta tumbili mfalme chini ya udhibiti kwa kutumia pete ya dhahabu iliyowekwa juu ya kichwa cha tumbili mfalme inayoweza kukazwa kwa uchawi, hivyo kumpa maumivu yasiyovumilika ya kichwa. Baadaye ikawa sitiari ya kuwafunga watu.


Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

     Tufuate: Neno la Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Pili"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni