5.25.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu II Sehemu ya Kwanza

Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Kwanza

Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee." Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, mmepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamewasaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya "Mamlaka ya Mungu."

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, "Mamlaka ya Mungu" ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii "Mamlaka ya Mungu" inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.

Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini "Mungu anadhibiti kila kitu"? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba "Mungu Anadhibiti kila kitu"? Kutoka kwenye kauli ile ile "Mungu anadhibiti kila kitu" tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa "kila kitu" ambacho Mungu "anadhibiti," na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.

Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.

Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanafanyika, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijiumbe maradhi vibaya au haribifu, na kasi yao, eneo lao, na mbinu ya kuenea kwake haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya binadamu. Ingawaje binadamu huvipinga vijiumbe maradhi hivi kwa kila namna inayowezekana, huwa hauwezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani ambao wanaathiriwa kwa vyovyote vile wakati kunapokuwa na mkurupuko wa magonjwa mlipuko. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua chanzo asilia kinachoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa mlipuko yoyote ya kibinafsi, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magojwa mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba viini vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho binadamu wanakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa mlipuko haya. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa mlipuko haya huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu binadamu wanayo imani tu katika sayansi, unategemea pakubwa kwa sayansi hiyo, lakini hautambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hautawahi kuwa na jibu.

Katika ukuu wa Mungu, mambo yote yapo na huangamia kwa sababu ya mamlaka Yake, kwa sababu ya usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayokuja na kuisha miongoni mwa mambo yote; ingawaje mambo haya yanao mwelekeo kwa binadamu, na ingawaje binadamu hung'amua kupitia kwa yaliyofichika akilini mwake, hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya mara kwa mara au hata hali ya ajabu ya mambo mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu mapenzi ya Muumba na akili Yake ambavyo vinaelezea mambo hayo. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, kuhusu kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kutimiza; uwezo wa binadamu walioundwa hauwezi kushindana nao. Baadhi ya watu husema "Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?" Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo sadiki hutokea wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, "Sadiki inatokana na kiwango na kina cha kuelewa kwa watu kwa, na hali wanayopitia wao, uhalisi na chanzo kikuu cha mambo." Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.

Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba
Nyinyi nyote ni watu wazima. Baadhi yenu ni wa umri wa kati; baadhi mmefikisha umri wa uzee. Kutoka kwa yule asiyesadiki hadi kwa yule anayesadiki, na kuanzia mwanzo wa kusadiki kwa Mungu hadi kukubali neno la Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu, je, ni maarifa kiwango kipi mliyopata kuuhusu ukuu wa Mungu? Ni maono yapi mliyopata kwenye hatima yenu ya kuwa binadamu? Je, mtu anaweza kutimiza kila kitu anachotamani katika maisha? Je, ni mambo mangapi kwenye miongo michache iliyopita katika kuwepo kwenu mliyoweza kutimiza kama mlivyopenda? Ni mambo mangapi hayafanyiki kama yalivyotarajiwa? Ni mambo mangapi hutupata kwa mshangao mzuri? Ni mambo mangapi ambayo ungali unasubiri kutimia—unasubiri bila kufahamu muda sahihi, unasubiria mapenzi ya Mbinguni? Mambo mangapi yanakufanya uhisi kana kwamba huna wa kukusaidia na umezuiliwa? Watu wote wanayo matumaini kuhusu hatima yao, na hutarajia kwamba kila kitu katika maisha yao kitaenda sawa na wanavyopenda, kwamba hawatakosa chakula wala mavazi, kwamba utajiri wao utaongezeka pakubwa. Hakuna anayetaka maisha ya kimaskini na ya taabu, yaliyojaa ugumu, na kuandamwa na majanga. Lakini watu hawawezi kuona mbele au kudhibiti mambo haya. Pengine kwa baadhi ya watu, yaliyopita ni mchanganyiko tu wa yale mambo waliyoyapitia; hawajifunzi katu ni nini mapenzi ya Mbinguni, wala hawajali mapenzi hayo ni yapi. Wanaishi kwa kudhihirisha maisha yao bila kufikiria, kama wanyama, wakiishi siku baada ya siku, bila kujali kuhusu hatima ya binadamu ni nini, kuhusu ni kwa nini binadamu wako hai au vile wanavyostahili kuishi. Watu hawa hufikia umri wa uzee bila ya kufaidi ufahamu wowote wa hatima ya binadamu, na mpaka wakati ule wanapokufa hawana habari yoyote kuhusu maana ya maisha. Watu kama hao wamekufa; ni viumbe bila roho; wao ni wanyama. Ingawaje katika kuishi miongoni mwa mambo haya yote, watu hupata furaha kutoka kwa njia nyingi ambazo ulimwengu hutosheleza mahitaji yao ya anasa, ingawaje wanauona ulimwengu huu wa anasa ukiwa unapiga hatua bila kusita, hali yao binafsi waliyoipitia—kile ambacho mioyo yao na roho zao zinahisi na kupitia—hakina uhusiano wowote na mambo ya anasa, na hakuna kitu chochote cha anasa ambacho kinaweza kuchukua nafasi yake. Ni utambuzi ndani ya moyo wa mtu, kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa jicho vivyo hivyo tu. Utambuzi huu umo katika ufahamu wa mtu wa, na hisia za mtu za, maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Na mara nyingi humwongoza mtu katika kuelewa kwamba Bwana yule asiyeonekana anapanga vitu vyote, Anaunda kila kitu kwa ajili ya binadamu. Katikati ya haya yote, mtu hawezi kuepuka ila kukubali mipangilio na mipango ya hatima ya mambo; wakati uo huo, mtu hawezi kuepuka ila kukubali njia iliyo mbele ambayo Muumba amempangia, ukuu wa Muumba dhidi ya hatima ya mtu. Hii ndiyo hoja isiyopingika. Haijalishi ni maono na mtazamo gani ambao mtu anao kuhusu hatima yake, hakuna anayeweza kubadilisha hoja hii.

Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanavyoendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au ruwaza ambazo yanajitokeza, ni vikumbusho vya kila wakati kwa binadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba njia ya maendeleo inayochukuliwa na mambo haya, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu. Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya binadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti mwenyewe. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayolazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, atatawala na kudhibiti hatima yao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali kwa nadharia yao bila kufahamu kile ambacho hatima yao imesheheni, kukubali kwa uhalisi, kwa mapenzi ya Mbinguni na ukuu wa Muumba. Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba "yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa," ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba "mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi."

Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba? Ingawaje binadamu huona, kwenye sheria zile za malengo, ukuu wa Muumba na utaratibu Wake wa matukio yote na mambo yote, ni watu wangapi wanaweza kung’amua kanuni ya ukuu wa Muumba juu ya ulimwengu? Ni watu wangapi wanaweza kujua, kutambua, kukubali kwa kweli na kujinyenyekeza kwa ukuu na mpangilio wa Muumba dhidi ya hatima zao wenyewe? Nani, ambaye baada ya kusadiki hoja ya ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote, ataweza kusadiki kwa kweli na kutambua kwamba Muumba pia anaamrisha hatima hii ya maisha ya binadamu? Ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli hoja hii kwamba hatima ya binadamu imo kwenye kiganja cha mkono wa Muumba? Aina ya mtazamo ambao binadamu wanafaa kuchukua katika ukuu wa Muumba, wanapokabiliwa na hoja kwamba Anatawala na kudhibiti hatima ya binadamu, ni uamuzi ambao kila binadamu ambaye kwa sasa anakabiliwa na hoja hii lazima ajiamulie mwenyewe.

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni