5.18.2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza



Utakatifu wa Mungu (I) Sehemu ya Kwanza

Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni cha tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo. Mnaelewa? Rudieni nyuma Yangu: kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu. (Kiini cha kipekee cha Mungu—utakatifu wa Mungu.) Mnahisi vipi katika mioyo yenu baada ya kurudia kirai hiki? Labda baadhi yenu wana wasiwasi kidogo, na wanauliza, "Mbona kushiriki utakatifu wa Mungu?" Msijali, Nitawazungumzia kuuhusu polepole. Punde tu mtakapousikia mtajua mbona ni muhimu Kwangu kushiriki mada hii.

Kwanza wacha tufafanue neno "takatifu." Mkitumia utambuzi wenu na kutoka kwa maarifa yenu mmefunzwa, mnaelewa ufafanuzi wa "takatifu" kuwa nini? Nifafanulieni. ("Takatifu" inamaanisha bila doa, bila upotovu au dosari yoyote ya binadamu. Kila kitu inachonururisha—kiwe kwa mawazo, matamshi ama vitendo, kila kitu inafanya—ni chema kabisa.) Vizuri kabisa. ("Takatifu" ni ya Mungu, haijanajisiwa, isiyokosewa na mtu. Ni ya kipekee, ni ishara ya tabia ya Mungu.) ("Takatifu" haina doa na ni kipengele cha Mungu, tabia isiyokosewa.) Huu ni ufafanuzi wako. Katika moyo wa kila mtu, neno hili "takatifu" lina wigo, ufafanuzi na fasiri. Kwa kiwango cha chini kabisa, mnapoona neno "takatifu" akili zenu si tupu. Mna wigo fulani uliofafanuliwa wa neno hili, na ufafanuzi huu wa watu wengine uko karibu kutumia neno hili kufafanua kiini cha tabia ya Mungu. Hii ni vizuri sana. Watu wengi zaidi wanaamini neno "takatifu" ni neno njema, na hii inaweza kuthibitishwa. Lakini utakatifu wa Mungu Ninaotaka kushiriki leo hautafafanuliwa tu, ama kuelezwa tu. Badala yake, Nitatumia baadhi ya ukweli kudhihirisha ili kukuruhusu kuona kwa nini Nasema Mungu ni mtakatifu, na mbona Natumia neno "takatifu" kuelezea kiini cha Mungu. Kabla ya ushirika wetu kuisha, utahisi kwamba matumizi ya neno "takatifu" kuelezea kiini cha Mungu na matumizi ya neno hili kumrejelea Mungu yanastahili sana na yanafaa. Kwa kiwango cha chini zaidi, kuhusiana na lugha za sasa za binadamu, kutumia neno hili kumrejelea Mungu kunafaa hasa—ni neno pekee kwa lugha ya binadamu linalofaa kabisa kumrejelea Mungu. Si neno tupu linapotumika kumrejelea Mungu, wala si sifa bila sababu au pongezi tupu. Madhumuni ya ushirika wetu ni kumruhusu kila mtu kuutambua ukweli wa kipengele hiki cha kiini cha Mungu. Mungu haogopi uelewa wa watu, bali kutoelewa kwao tu. Mungu anataka kila mtu ajue kiini Chake na kile Anacho na alicho. Hivyo kila wakati tunapotaja kipengele cha kiini Cha Mungu, tunaweza kutumia ukweli mwingi kuwaruhusu watu kuona kwamba kipengele hiki cha kiini cha Mungu kweli kipo.

Kwa sababu sasa tuna ufafanuzi wa neno "takatifu," wacha tuangalie baadhi ya mifano. Katika fikira ambazo watu wanazo, wanafikiria vitu na watu wengi "watakatifu." Kwa mfano, wavulana na wasichana mabikira wanaelezwa kama watakatifu katika kamusi za binadamu? (Ndiyo.) Je, kweli ni watakatifu? (La.) Je, hii inayoitwa "takatifu" na "takatifu" tutakayoshiriki leo ni kitu sawa? (La.) Tukiangalia wale miongoni mwa wanadamu walio na maadili ya juu, na matamshi bora na ya maarifa, wasiomwumiza yeyote na ambao, wanapozungumza, wanawafanya wengine kustareheka na kufurahia—ni watakatifu? Wasomi wa Confucius au waungwana walio na maadili ya juu, na wenye ubora wa maneno na vitendo—ni watakatifu? Wale wanaofanya mazuri mara nyingi, wanaopenda kutoa na kuwasaidia wengine, wanaoleta raha nyingi kwa maisha ya watu—ni watakatifu? (La.) Wale wasio na fikira za kujihudumia, wasioweka madai makali juu ya yeyote, wanaomvumilia yeyote—ni watakatifu? Wale ambao hawajawahi kuwa na mzozo na yeyote wala kujinufaisha na yeyote—ni watakatifu? Basi wale wanaofanya kazi kwa minajili ya uzuri wa wengine, wanaofaidi wengine na kuleta uboreshaji kwa wengine kwa namna zote—ni watakatifu? Wanaowapa wengine akiba zao zote za maisha na kuishi maisha rahisi, walio wakali kwa wao wenyewe lakini wanawashughulikia wengine kwa ukarimu—ni watakatifu? (La.) Mnakumbuka kwamba mama zenu waliwatunza na kuwalinda kwa njia zote zinazoweza kufikiriwa—ni watakatifu? Vijimungu mnaopenda sana, wawe watu maarufu, mashuhuri ama watu wakubwa—ni watakatifu? (La.) Hebu sasa tuangalie wale manabii katika Biblia walioweza kuelezea siku za baadaye ambazo hazikujulikana na wengine wengi—mtu wa aina hii alikuwa mtakatifu? Watu walioweza kurekodi maneno ya Mungu na ukweli wa kazi Yake katika Biblia—walikuwa watakatifu? Musa alikuwa mtakatifu? Ibrahimu alikuwa mtakatifu? (La.) Ayubu je? Alikuwa mtakatifu? (La.) Mbona mnasema hivi? Ayubu aliitwa mtu mwenye haki na Mungu, basi mbona hata yeye anasemekana kutokuwa mtakatifu? Mnahisi wasiwasi kiasi hapa, sivyo? Watu wanaomcha Mungu na kuepukana na maovu kweli si watakatifu? Ni watakatifu ama si watakatifu? (La.) Jibu lenu ni hapana. Basi jibu lenu la hapana limetokana na nini? (Mungu ni wa kipekee.) Huu ni msingi uliopatikana vizuri. Ninagundua kwamba mna uwezo mkubwa wa kuelewa vitu haraka na kutumia mlichojifunza, na kwamba nyinyi nyote mna ujuzi huu maalum. Mna wasiwasi kidogo, hamna uhakika sana, na hamthubutu kusema "La," lakini pia hamthubutu kusema "Ndiyo," kwa hivyo mnasema "La" na ugumu fulani. Wacha Niulize swali lingine. Wajumbe wa Mungu—wajumbe ambao Mungu huwatuma chini duniani—ni watakatifu? (La.) Lifikirie kwa makini. Peana jibu lenu baada ya kulifikiria. Malaika ni watakatifu? (La.) Wanadamu ambao hawajapotoshwa na Shetani—ni watakatifu? (La.) Nyinyi mnasema "La" kwa kila swali. Kwa msingi upi? Je, kirai Nilichosema sasa hivi ndicho sababu mnasema "La"? Mmechanganyikiwa, sivyo? Basi mbona hata malaika wanasemekana sio watakatifu? Mna wasiwasi hapa, sio? Basi mnaweza kugundua ni kwa msingi upi watu, vitu ama viumbe wasioumbwa tuliotaja mbeleni si watakatifu? Nina uhakika hamwezi, sio? (Ndiyo.) Hivyo kusema kwenu "La" basi ni kukosekana kwa uwajibikaji kidogo? Hamjibu bila kujali? Watu wengine wanafikiria: "Unauliza kwa namna hii, kwa hivyo si lazima iwe hivyo hakika." Msijibu tu bila kujali. Fikirieni kwa makini iwapo jibu ni ndiyo au la. Mtajua tutakaposhiriki mada ifuatayo mbona ni "La." Nitawapa jibu hivi punde. Hebu kwanza tusome baadhi ya maandiko.

Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu

Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.

Nyoka Anamshawishi Mwanamke

Mwa 3:1-5 Sasa nyoka alikuwa mwenye hila kuliko wanyama wote wa mwitu ambao Yehova Mungu alikuwa amewaumba. Naye akamwambia mwanamke, Naam, Mungu amesema, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Naye mwanamke akamwambia nyoka, Tunaweza kula matunda ya miti katika bustani: Mungu amesema, Lakini msile wala kuyagusa matunda ya mti ulio katikati ya bustani, msije mkafa. Naye nyoka akamwambia mwanamke, Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu.

Hivi vifungu viwili ni dondoo kutoka kwa kitabu kipi cha Biblia? (Mwanzo.) Je, nyinyi nyote mnavijua vifungu hivi viwili? Hiki ni kitu kilichofanyika mwanzoni wakati binadamu kwanza aliumbwa; lilikuwa ni tukio halisi. Kwanza hebu tuangalie ni amri ya aina gani ambayo Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa, kwani yaliyomo katika amri hii ni muhimu sana kwa mada yetu ya leo. "Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema…." Endelea kusoma kifungu kifuatacho. ("Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.") Amri ya Mungu kwa mwanadamu katika kifungu hiki ina nini? Kwanza, Mungu anamwambia mwanadamu kile anachoweza kula, yakiwa ni matunda ya miti ya aina nyingi. Hakuna hatari na hakuna sumu, yote yanaweza kulika na kulika atakavyo mtu, bila wasiwasi wowote. Hii ni sehemu moja. Sehemu nyingine ni onyo. Onyo hili linamwambia mwanadamu mti ambao hawezi kula tunda kutoka—lazima asile tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nini itafanyika akifanya hivyo? Mungu alimwambia mwanadamu: Ukilila hakika utakufa. Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Iwapo Mungu angekwambia jambo hili lakini hukuelewa kwa nini, ungelichukulia kama kanuni ama amri ya kufuatwa? Linapaswa kufuatwa, sivyo? Lakini iwapo mwanadamu anaweza ama hawezi kulifuata, maneno ya Mungu hayaachi shaka. Mungu alimwambia mwanadamu kwa uwazi kabisa kile anachoweza kula na kile asichoweza, na kile kitakachofanyika akila kile hapaswi kula. Umeona tabia yoyote ya Mungu katika haya maneno machache ambayo Alisema? Haya maneno ya Mungu ni ya ukweli? Kuna udanganyifu wowote? Kuna uongo wowote? (La.) Kuna chochote kinachotisha? (La.) Mungu kwa uaminifu, kwa kweli, kwa dhati Alimwambia mwanadamu kile anachoweza kula na kile asichoweza kula, wazi na dhahiri. Kuna maana iliyofichwa katika maneno haya? Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Je, kuna haja yoyote ya dhana? (La.) Hakuna haja ya kukisia, sivyo? Maana yake ni wazi kwa mtazamo mmoja, na unaelewa punde tu unapoyaona. Ni wazi kabisa. Yaani, kile Mungu anataka kusema na Anachotaka kuonyesha kinatoka katika moyo Wake. Mambo ambayo Mungu anaonyesha ni safi, yanaeleweka kwa urahisi na ni wazi. Hakuna nia za siri ama maana zilizofichwa. Alizungumza moja kwa moja na mwanadamu, Akimwambia kile anachoweza kula na kile asichoweza kula. Hivyo ni kusema, kupitia maneno haya ya Mungu mwanadamu anaweza kuona kwamba moyo wa Mungu ni angavu, kwamba moyo wa Mungu ni wa kweli. Hakuna uwongo kabisa hapa, kukwambia kwamba huwezi kula kile kinacholika ama kukwambia "Ifanye na uone kitakachofanyika" na vitu ambavyo huwezi kula. Anamaanisha jambo hili? (La.) La. Chochote afikiriacho Mungu katika moyo Wake ndicho Anachosema. Nikisema Mungu ni mtakatifu kwa sababu Anaonyesha na kujifichua Mwenyewe ndani ya maneno haya kwa njia hii, unaweza kuhisi kana kwamba Nimefanya jambo lisilokuwa kubwa ama Nimenyoosha ufasiri Wangu mbali kiasi. Kama ni hivyo, usijali, hatujamaliza bado.

Hebu tuzungumze kuhusu "Nyoka Anamshawishi Mwanamke." Nyoka ni nani? (Shetani.) Shetani anashikilia jukumu la foili[a] katika mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na ni jukumu ambalo hatuwezi kosa kutaja wakati tunaposhiriki utakatifu wa Mungu. Mbona Nasema hivi? Iwapo hujui uovu na upotovu wa Shetani ama asili ya Shetani, basi huna njia ya kumtambua, wala huwezi kujua utakatifu kweli ni nini. Katika mkanganyiko, watu wanaamini kwamba kile anachofanya shetani ni chema, kwa sababu wanaishi ndani ya aina hii ya tabia potovu. Bila foili[a], bila chochote cha kulinganisha nacho, huwezi basi kujua utakatifu ni nini, hivyo basi ni lazima mada hii itajwe hapa. Hatujatoa mada hii ghafla kutoka mahali popote, ila badala yake kupitia maneno na matendo yake tutaona jinsi Shetani anavyotenda, jinsi anavyopotosha binadamu, aina ya asili yake na jinsi uso wake ulivyo. Basi mwanamke huyu alimwambia nini nyoka? Mwanamke alimweleza nyoka kile Yehova Mungu alikuwa amemwambia. Kwa kufuata alichosema, alikuwa amethibitisha uhalali wa yote ambayo Mungu alikuwa amemwambia? Hangeweza kuthibitisha haya, angeweza? Kama mtu ambaye alikuwa ameumbwa karibuni, hakuwa na uwezo wa kutambua mema kutoka kwa maovu, wala hakuwa na uwezo wa kufahamu chochote karibu naye. Kwa kutathmini maneno aliyomwambia nyoka hakuwa amethibitisha maneno ya Mungu kuwa kweli katika moyo wake; huu ulikuwa mtazamo wake. Hivyo wakati nyoka aliona kwamba mwanamke huyo hakuwa na mtazamo wa uhakika kwa maneno ya Mungu, alisema: "Bila shaka hamtakufa: Kwa kuwa Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa, nanyi mtakuwa kama miungu, mkijua mema na maovu." Kuna chochote kibaya na maneno haya? (Ndiyo.) Ni nini kibaya? Mlipomaliza kusoma sentensi hii, mlipata hisia ya nia za nyoka? (Ndiyo.) Nyoka ana nia gani? (Kumjaribu mwanadamu kufanya dhambi.) Anataka kumjaribu mwanamke huyu kumfanya aache kusikiza maneno ya Mungu, lakini Je, aliongea moja kwa moja? (La.) Hakuongea moja kwa moja, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba ana ujanja sana. Anaonyesha maana yake kwa njia ya udanganyifu na ya kukwepa ili kufikia malengo anayonuia ambayo anaficha kutoka kwa mwanadamu ndani yake—huu ndio ujanja wa nyoka. Shetani amewahi kuzungumza na kutenda hivi. Anasema "sio kwa uhakika," bila kuthibitisha kwa njia moja au nyingine. Lakini baada ya kusikia haya, moyo wa huyu mwanamke mjinga uliguswa? (Ndiyo.) Nyoka alifurahia kwa sababu maneno yake yalikuwa na matokeo yaliyotarajiwa—hii ilikuwa nia ya ujanja ya Nyoka. Zaidi ya hayo, kwa kuahidi matokeo ambayo mwanadamu aliamini kuwa mema, alimshawishi, akisema, "siku mtakayokula matunda ya mti huo, macho yenu yatafunuliwa." Hivyo mwanamke anafikiria: "Kufumbuliwa macho yangu ni jambo zuri!" Bado nyoka kisha anazungumza maneno ambayo binadamu anaamini kuwa mazuri zaidi, maneno yasiyojulikana na mwanadamu, maneno yaliyo na nguvu kubwa ya majaribu juu ya wale wanaoyasikia: "nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na maovu." Je, maneno haya hayamvutii mwanadamu sana? Ni kama mtu kukwambia: "Uso wako una umbo nzuri. Ni mfupi kidogo katika daraja la pua, lakini ukiirekebisha, utakuwa mrembo wa kupindukia!" Kwa mtu ambaye hajawahi kutaka kufanya upasuaji wa mapambo, moyo wake utaguswa kusikia maneno haya? (Ndiyo.) Kwa hivyo maneno haya ni ya kushawishi? Ushawishi huu unakuvutia? Ni wa kujaribu? (Ndiyo.) Je, Mungu husema mambo kama haya? Kulikuwa na dokezo lolote la haya katika maneno ya Mungu tuliyoyaangalia sasa hivi? (La.) Mbona? Je, Mungu husema Anachofikiria katika moyo Wake? Mwanadamu anaweza kuona moyo wa Mungu kupitia maneno Yake? (Ndiyo,) Lakini wakati nyoka alikuwa amesema maneno haya kwa mwanamke, uliweza kuona moyo wake? (La.) Na kwa sababu ya ujinga wa mwanadamu, walishawishiwa kwa urahisi na maneno ya nyoka, walishikwa kwa urahisi, waliongozwa kwa urahisi. Hivyo uliweza kuona nia za Shetani? Uliweza kuona madhumuni nyuma ya kile alichosema? Uliweza kuona njama na mpango wake wa ujanja? (La.) Ni aina gani ya tabia inayowakilishwa na njia ya mazungumzo ya Shetani? Ni aina gani ya kiini ulichoona ndani ya Shetani kupitia maneno haya? Je, ni mwenye kudhuru kwa siri? Pengine juujuu anakupa tabasamu ama kutofichua maonyesho yoyote. Lakini katika moyo wake anahesabu jinsi ya kufikia lengo lake, na ni lengo hili ambalo huwezi kuliona. Kisha unashawishiwa na ahadi zote anazokupa, manufaa yote anayozungumzia. Unayaona kuwa mazuri, na unahisi kwamba kile anachosema ni cha kufaa zaidi, kikubwa zaidi kuliko asemacho Mungu. Wakati haya yanafanyika, je, mwanadamu basi hawi mfungwa mtiifu? (Ndiyo.) Basi mbinu hizi zinazotumiwa na Shetani si za kikatili? Unajikubali kuzama chini. Bila ya Shetani kusongeza kidole, kwa sentensi hizi mbili unafurahia kumfuata na kumtii. Lengo lake limefikiwa. Nia hii si ya husuda? Huu sio uso wa kimsingi kabisa wa Shetani? Kutoka kwa maneno ya Shetani, mwanadamu anaweza kuona nia zake za husuda, kuona uso wake wenye sura mbaya na kiini chake. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa kulinganisha sentensi hizi, bila uchambuzi pengine unaweza kuhisi kana kwamba maneno ya Yehova Mungu ni ya kuchusha, ya kawaida na ya wote, kwamba hayastahili kuhangaikiwa kuusifu uaminifu wa Mungu. Tunapochukua maneno ya Shetani na uso wake wenye sura mbaya na kuvitumia kama foili[a], hata hivyo, je, haya maneno ya Mungu yanabeba uzito mwingi kwa watu wa leo? (Ndiyo.) Kupitia foili[a] hii, mwanadamu anaweza kuhisi kutokuwa na dosari kwa Mungu. Niko sahihi Nikisema hivi? (Ndiyo.) Kila neno analosema Shetani pamoja na nia zake, malengo yake na jinsi anavyoongea—yote yamepotoshwa. Ni nini sifa muhimu ya njia yake ya kuzungumza? Anatumia maneno yasiyo dhahiri kukushawishi bila kukuruhusu kumwona, wala hakuruhusu kutambua lengo lake ni nini; anakuacha uchukue chambo, akikufanya umsifu na kuimba uzuri wake. Hii siyo hila ya daima ya Shetani? (Ndiyo.)

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.


Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni