Mamlaka ya Mungu (II) Sehemu ya Sita
Kifo: Awamu ya Sita
4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu
Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya.