Utakatifu wa Mungu (I) Sehemu ya Kwanza
Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni cha tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.)