4.15.2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano"




       Mwenyezi Mungu alisema, “ 1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu ”

       Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa na maisha ya awali ya mtu, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu ya maisha, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba amepangilia mseto maalum wa hali mbalimbali za kuzaliwa kwa mtu, ni wazi na dhahiri shahiri kwamba amepangilia pia mseto wa hali zisizobadilika kwa minajili ya kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu ambacho hakitarajiwi, na si kuzaliwa, si kufa vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa.

4.14.2019

Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe.

Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe


Maneno Husika ya Mungu:

Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia. 

4.13.2019

Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”


Matamshi ya Mungu | “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Moja”


 Mwenyezi Mungu anasema, “Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Kuzaliwa na kufa kwa nani kulitokana na kuchagua kwao? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu.”

4.12.2019

Kwa nini Mungu huitwa majina tofauti katika enzi tofauti? Ni nini umuhimu wa majina ya Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:

       Unapaswa kujua kuwa Mungu mwanzoni hakuwa na jina. Yeye Alichukua tu jina moja, au majina mawili, ama majina mengi kwa sababu Alikuwa na kazi ya kufanya na Alikuwa na jukumu la kumsimamia mwanadamu. Jina lolote ambalo anaitwa Yeye, je, si lile analolichagua kwa hiari yake? Je, Yeye anakuhitaji wewe, kiumbe, kuamua jina lake? Jina ambalo Mungu Anaitwa ni kwa mujibu wa kile ambacho mwanadamu anaweza kufahamu na lugha ya mwanadamu, lakini hili jina haliwezi kujumlishwa na mwanadamu.

4.11.2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”


       Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu.

4.10.2019

Ni vipi kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa wanadamu?

Ni vipi kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa wanadamu?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho" (YN. 12:47-48).

"Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo" (YN. 16:12-13).

4.09.2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza


        Mwenyezi Mungu anasema, "Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu.

4.08.2019

Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu" (LAW. 11:45).

"Na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana" (EBR. 12:14).

"Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho" (YN. 12:47-48).

4.07.2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”


Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote.

4.06.2019

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?


Maneno Husika ya Mungu:

Usimamizi mzima wa Mungu umegawika kwa hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayopatana yanatokana na mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu huongezeka hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na hivyo mahitaji ya mwanadamu huongezeka hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huongezeka hata zaidi. … Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kuzingatia sheria na amri, na alihitajika kuwa mpole na mnyenyekevu.  

4.05.2019

Neno la Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”

 

Neno la Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”


      Mwenyezi Mungu anasema, “Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu. Sijawahi kumpata mmoja ambaye kwa kweli aliweka moyo wake na roho yake kwenye madhabahu Yangu, ambayo hayajawahi kusonga. Kwa hivyo, Singependa kuyamwaga bure maneno yote ambayo Nina nia ya kumwelezea mwanadamu wa aina hii.

4.04.2019

Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu


Maneno Husika ya Mungu:

       Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.