Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haitabadilika kamwe
Maneno Husika ya Mungu:
Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? Kazi yake daima inaendelea mbele, na hivyo pia ndivyo tabia yake inafichuliwa kwa binadamu hatua kwa hatua, na kile ambacho kinafichuliwa ni tabia yake ya asilia.