Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu
Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya
Maneno Husika ya Mungu:
Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu.