1.23.2019

Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"


Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"


       Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii kwa moyo wake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi inayofanywa na Mungu daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya vitendo kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha inakua hata juu zaidi, hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya hivi ili kupinga na kubadilisha dhana za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, kwa ulimwengu wa juu zaidi wa imani kwa Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yanafanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Kwa kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kusalimisha na kuweka kando dhana zenu. Kila hatua inapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu. Kama nyinyi ni wazembe, hakika mtakuwa wamoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayevuruga kazi ya Mungu. Kabla ya kufanyiwa hatua hii ya kazi, kanuni na sheria za mwanadamu za zamani zilikuwa nyingi sana hadi akawa na msisimko zaidi, na mwishowe, akawa wenye majivuno na kujisahau. Hivi vyote ni vikwazo kwa njia ya mwanadamu kuikubali kazi mpya ya Mungu na ni adui kwa mwanadamu kuja kujua Mungu. Iwapo mwanadamu hana utii kwa moyo wake wala tamaa ya kujua ukweli, basi atakuwa hatarini. Ukitii tu kazi na maneno yaliyo rahisi, na huwezi kukubali yoyote yaliyo na ugumu zaidi, basi wewe ni yule anayeendelea na njia ya zamani na hawezi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa kwa awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wanatii Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima kwa utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haijakubaliwa na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na kuendelea kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Katika kazi ya Mungu, Anakuletea kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja. Wengine wanaweza kuwa waasi na kusema, “Sitafanya tu usemavyo,” Basi Nakwambia kwamba sasa ni mwisho wa njia. Umenyauka na huna maisha zaidi. Hivyo, kwa kupitia mabadiliko ya tabia yako, ni muhimu kabisa kwenda sambamba na mwangaza wa sasa. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi kwa mtu mwingine ajaye. Fuata kwa makini; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndipo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua ndani uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Ukifanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu wa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui kupitia mtu wa aina gani Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, hii inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Unapotembea kwenye njia sawa, utapewa ufunuo kwa mambo yote. Bila kujali yale Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kwa uzoefu wako kwa msingi wa maarifa yao, kupitia mambo wewe mwenyewe, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwasambazia wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaosambazia wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu; itakulazimu kujifunza kupata, kupitia mwangaza na kupatiwa nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta akili ya Mungu kwa vitu vyote na kujifunza masomo kwa vitu vyote, ukijenga ukuaji kwa maisha yako. Vitendo hivyo vitamudu ukuaji wa haraka zaidi.

kutoka kwa Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu

       Soma zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni