10.18.2019

Kumfuata Mungu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

      Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno halisi ya Mungu: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno halisi ya Mungu. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno halisi ya Mungu, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu.

10.17.2019

Asiyeamini ni nini?





Maneno Husika ya Mungu:

      Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini.

10.16.2019

Unafiki ni nini?







Maneno Husika ya Mungu:
Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli. Hali yake ya kweli imefichwa ndani ya moyo wake; haionekani. Watu wasipofuatilia ukweli, kama hawaelewi ukweli, basi maarifa yao ya kidini na nadharia ambazo wamepata zinakuwa nini? Je, zinakuwa maneno ya mafundisho ambayo watu huzungumzia mara nyingi? Watu hutumia haya yanayodaiwa kuwa mafundisho sahihi kujifanya na kujionyesha kuwa wazuri.

10.15.2019

Kiongozi wa uongo au mchungaji wa uongo ni nini? Je, kiongozi wa uongo au mchungaji wa uwongo anaweza kutambuliwaje?



Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu.

10.14.2019

Kristo wa uongo ni nini? Kristo wa uongo anaweza kutambuliwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.
kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena.

10.13.2019

Mpinga Kristo ni nini? Mpinga Kristo anaweza kutambuliwaje?


Maneno Husika ya Mungu:
Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu.

10.12.2019

Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina.

10.11.2019

Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa





Maneno Husika ya Mungu:
Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu. Bila kujali kama kuna matokeo yoyote, au kama kuna kuelewa kwa kweli, watu hawa hulenga tu kufanya mambo yasiyo ya dhati kwa nje, na hawalengi matokeo ni watu wanaoishi ndani ya mila za dini, na si watu wanaoishi ndani ya kanisa, na hata zaidi wao si watu wa ufalme.

10.10.2019

Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tu kwamba ikiwa unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu akisema ni vizuri na kukupa hongera inahesabika kama kuelewa, neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza mapenzi ya Mungu ni yapi ndani ya maneno hayo na yatafanikisha nini hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa.

10.09.2019

Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Maneno Husika ya Mungu:
Unaweza kuutoa moyo wako na mwili na upendo wako wote wa kweli kwa Mungu, uyaweke mbele Zake, kuwa mtiifu kabisa Kwake, na kufikiria kabisa mapenzi Yake. Si kwa ajili ya mwili, si kwa ajili ya familia, wala si kwa ajili ya matamanio yako mwenyewe, bali ni kwa ajili ya maslahi ya nyumba ya Mungu. Katika kila kitu unaweza kuchukua neno la Mungu kama kanuni, kama msingi. Hivyo, malengo yako na mtazamo wako yote yatakuwa mahali sahihi, na utakuwa mtu ambaye anapata sifa za Mungu mbele Zake.

10.08.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?

Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu.

10.07.2019

Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kutimiza wajibu wako ni ukweli. Kutimiza wajibu wako katika nyumba ya Mungu sio tu kutimiza masharti fulani au kufanya kitu unachopaswa kufanya. Ni kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa anayeishi kati ya mbingu na dunia! Ni kutimiza majukumu na wajibu wako mbele ya Bwana wa uumbaji. Majukumu haya ni majukumu yako ya kweli. Linganisha kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa na kuwa na upendo kwa wazazi wako—ni kipi ndicho ukweli? Kutimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa ndio ukweli; ni wajibu wako unaotarajiwa kutimiza.