Kipengele kimoja cha kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi kilikuwa ni kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu, wakati kile kipengele kingine kilikuwa ni kutupa amani na furaha na neema nyingi. Hili linatuwezesha kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye huruma na mwenye upendo. Lakini unashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu hufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kwamba Yeye huonyesha ukweli na humhukumu na kumwadibu mwanadamu, humpogoa na kumshuhgulikia mwanadamu, humfichua mwanadamu na kuziondosha kila aina ya watu waovu, pepo wabaya na wapinga Kristo, jambo linalowaruhusu watu kuona kwamba tabia ya haki ya Mungu haivumilii kosa lolote. Kwa nini tabia iliyofichuliwa katika kazi ya Bwana Yesu ni tofauti kabisa na tabia iliyofichuliwa katika kazi ya Mwenyezi Mungu? Ni vipi hasa tunafaa kuielewa tabia ya Mungu?
Jibu:
Tangu Bwana Yesu alipofanya kazi Yake ya ukombozi katika Enzi ya Neema, tumeona kwamba Yeye ni mwingi wa stahamala na uvumilivu, mwingi wa upendo na huruma. Ilimradi tumwamini Bwana Yesu, dhambi zetu zitasamehewa na tutaweza kufurahia neema ya Mungu. Kutokana na hilo, tumepambanua kwamba Mungu ni Mungu mwenye upendo na mwenye rehema, kwamba Yeye ni mwenye huruma kwa mwanadamu na humsamehe mwanadamu dhambi zake zote milele, na kwamba siku zote Mungu hututendea kama mama anavyowatendea watoto wake, kwa kujali sana, asionyeshe hasira kamwe.